SWALI
Ipi hukumu ya kufanya I´tikaaf mwezi mzima wa Ramadhwaan?
JIBU
Ni Sunnah. Kufanya I´tikaaf ni Sunnah sawa iwe kafanya I´tikaaf mwezi wa Ramadhwaan mzima au siku kumi, ishirini au kumi. Sawa katika mwezi wa Ramadhwaan au mingineyo akipenda kukaa I´tikaaf ikiwa ni kulipa, au naafil, zote ni mustahab.
Na bora ni kumi la mwisho katika Ramadhwaan ili kupata Laylatul-Qadr na kujihifadhi kwa utiifu na kudumisha ´amali njema na kuwa na subira kwa hilo.
Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alifanya I´tikaaf katika Shawwaal. Na pia alimruhusu ´Umar bin Al-Khattwab (Radhwiya Allaahu 'anhu) kukaa I´tikaaf usiku alipe. Inafanywa katika kila Msikiti kutokana na kauli ya Allaah (´Azza wa Jalla):
"Na hali mnakaa I´tikaaf Msikitini."[02: 187]
"Na hali mnakaa I´tikaaf Msikitini."[02: 187]
Katika Ramadhwaan yote kwa mwenye kupenda na akikaa I´tikaaf, au baada ya Ramadhwaan baadhi ya wakati, si haraam kwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimruhusu ´Umar kukaa I´tikaaf. Na huenda baadhi ya ‘Ulamaa hukaa miaka na miaka katika Msikiti wa Makkah wakifanya I´tikaaf.
http://bit.ly/2QaDkgn i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni