Swali 425: Ni ipi ya mfungaji kujitia baridi kidogo?
Jibu: Mfungaji kujiweka baridi ni jambo linalofaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akijimwagia maji kichwani mwake kwa sababu ya joto kali au kwa sababu ya kiu ilihali amefunga[1]. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) alikuwa akiilowesha nguo yake kwa maji ilihali amefunga kwa ajili ya kupunguza ukali wa joto au kiu. Unyevunyevu hauathiri. Kwani maji hayafiki tumboni.
[1] Abu Daawuud (2365).
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2JFwdLH
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni