Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Israfu ya Chakula wakati wa Futari

SWALI

Je, mtu hupata thawabu ndogo (ya Swawm) ikiwa atakithirisha kukata Swawm (Futari) kwa masahani ya vyakula mbali mbali?


JIBU

Hapana, hupati thawabu ndogo ya Swawm. Mtu kufanya kitendo cha haraam baada ya kumaliza Swawm, (kitendo kile) hakiathiri thawabu (za Swawm). Bali inaingia katika neno Lake Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
وَكُلُوا وَاشْرَبُوا وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ ﴿٣١﴾
“Na kuleni na kunyweni; na wala msifanye israfu. Hakika Yeye (Allaah) Hapendi wanaofanya israfu. [Al-A’raaf 7: 31]

Huku kufanya israfu ndiyo haraam. Na iktisadi ni nusu ya maisha.  Ikiwa bila kukusudia kutabaki chakula, ni afadhali kitolewe swadaqah.


[Fiqhu Al-'Ibaadah, uk. 252]


http://bit.ly/2HxJuTB i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...