Translate

Jumamosi, 18 Mei 2019

Anayempikia Chakula Mume Wake Asiefunga Katika Ramadhwaan


SWALI


Mume wangu hataki kufunga zaidi ya miaka ishirini. Kipindi chote hicho nilikuwa nikimpikia chakula wakati mimi mwenyewe nimefunga. Je ninapata madhambi?


JIBU


Ndiyo, ni dhambi. Lazima utubu kwa Allaah  kwa kitendo hicho.  Wakati wewe unampikia chakula mchana wa Ramadhwaan, unamsaidia kumuasi Allaah (’Azza wa Jall). Allaah (Jalla wa 'Alaa) Anasema:
  وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ ۚ
Na shirikianeni katika wema na taqwa, na wala msishirikiane katika dhambi na uadui. [Al-Maaidah : 2]


Kumpikia chakula au kumtengea chakula na kumpa mchana wa Ramadhwaan au kumpa sigara au pombe n.k. ni dhambi, na ni maovu juu ya maovu. 

Hupaswi kabisa kumsaidia kutofunga sawa ikiwa ni (kwa kumpa) chakula, kinywaji, sigara au pombe. Yote haya ni madhambi juu ya madhambi, Tunamuomba Allaah Al-‘Aafiyah. Bali ni juu yako kumnasihi na kukataa kumtii na kumwambia huwezi kumsadia kwa hilo, na arudie kubeba madhambi mwenyewe.



http://bit.ly/2HCx1xU i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...