Translate

Alhamisi, 16 Mei 2019

19-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake Aliipa Dunia Mgongo Akawa Analalia Mkeka

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

19-Unyeyekevu Wake Aliipa Dunia Mgongo Akawa Analalia Mkeka

 

www.alhidaaya.com

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa anaishi katika nyumba ya fakhari, wala kumiliki fenicha au vitu vya fakhari. Alifikia kulalia mkeka kama ilivyothibiti katika Hadiyth ndefu  ya ‘Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) ambayo alisema:

 

فَدَخَلْتُ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ مُضْطَجِعٌ عَلَى حَصِيرٍ فَجَلَسْتُ فَأَدْنَى عَلَيْهِ إِزَارَهُ وَلَيْسَ عَلَيْهِ غَيْرُهُ وَإِذَا الْحَصِيرُ قَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ فَنَظَرْتُ بِبَصَرِي فِي خِزَانَةِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَإِذَا أَنَا بِقَبْضَةٍ مِنْ شَعِيرٍ نَحْوِ الصَّاعِ وَمِثْلِهَا قَرَظًا فِي نَاحِيَةِ الْغُرْفَةِ وَإِذَا أَفِيقٌ مُعَلَّقٌ – قَالَ: فَابْتَدَرَتْ عَيْنَاىَ قَالَ: ((مَا يُبْكِيكَ يَا ابْنَ الْخَطَّابِ)).‏ قُلْتُ: يَا نَبِيَّ اللَّهِ وَمَا لِي لاَ أَبْكِي وَهَذَا الْحَصِيرُ قَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِكَ وَهَذِهِ خِزَانَتُكَ لاَ أَرَى فِيهَا إِلاَّ مَا أَرَى وَذَاكَ قَيْصَرُ وَكِسْرَى فِي الثِّمَارِ وَالأَنْهَارِ وَأَنْتَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَصَفْوَتُهُ وَهَذِهِ خِزَانَتُكَ.‏ فَقَالَ: ((يَا ابْنَ الْخَطَّابِ أَلاَ تَرْضَى أَنْ تَكُونَ لَنَا الآخِرَةُ وَلَهُمُ الدُّنْيَا)).‏ قُلْتُ: بَلَى

Nikaingia kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  (nikamkuta) akiwa amelala kwa ubavu juu ya mkeka. Nikakaa, na (Rabaah) akamsogezea izari yake, na hana nyingine zaidi ya hiyo. Nikashtuka kuona alama za mkeka zimeacha athari kwenye ubavu wake. Halafu nikapembua kwa jicho langu kwenye khizaanah (stoo) ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  na nikashtuka kuona shayiri kiasi cha pishi moja ya kujaa kiganja cha mkono na kiasi kama hicho hicho cha gundi upande wa chumba ambako kuna ngozi mbichi imetundikwa (upande mmoja). Hapo hapo macho yangu yakatiririka machozi. Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Kinakuliza nini ee Ibn Al-Khattwaab?)). Nikasema: “Ee Nabiy wa Allaah, kwanini nisilie ilhali huu mkeka umekufanyia alama mwilini mwako na khizaanah yako sioni kilichomo ila kile ninachokiona na ilhali kule kuna (Wafalme) Qayswar (Kaisari) na  Kisraa  wana matunda na mito (wanaishi kifakhari), basi vipi iwe wewe Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye Allaah Amekuchagua (huna lolote)  hii ndio khizaanah yako?” Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Ee Ibn Al-Khattwaab,  je, huridhii sisi tukawa na Aakhirah na wao wakawa na dunia?)). Nikasema: “Naam!” (nakubaliana nawe).

 

Pia katika Hadiyth ifuatayo inadhihirisha unyenyekevu wake wa maisha duni na kuipa dunia mgongo:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ ابن مسعود (رضي الله عنه) قَال: نَامَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى حَصِيرٍ فَقَامَ وَقَدْ أَثَّرَ فِي جَنْبِهِ، فَقُلْنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ! لَوْ اتَّخَذْنَا لَكَ وِطَاءً. فَقَالَ: ((مَا لِي وَمَا لِلدُّنْيَا؟ مَا أَنَا فِي الدُّنْيَا إِلاَّ كَرَاكِبٍ اسْتَظَلَّ تَحْتَ شَجَرَةٍ ثُمَّ رَاحَ وَتَرَكَهَا))  الترمذي وقال: حَدِيثٌ حَسَنٌ صَحِيحٌ

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه)  amesema: “Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alilala kwenye jamvi la mtende likamfanyia alama ubavuni mwake tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Tukufanyie godoro laini? Akasema: ((Mimi na dunia wapi na wapi? Mfano wangu na dunia ni kama mpandaji [anayesafiri kwa mnyama] aliyepumzika kivulini chini ya mti, [muda mfupi tu] kisha akaondoka na kuuacha (huo mti na kivuli chake))). [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

 



http://bit.ly/2Qa6MD5

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...