Usiseme ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’ Baada ya kusoma Qur-aan
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa Aswhaabihil Kiraam, wa ba’ad.
✅Naam,Watu wengi katika jamii wana mazoea baada ya kumaliza kusoma Qur-aan, kusema ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’.
➡Watu wengi wakiwa wameathirika kwa mazoea ima ya kusikia kwenye radio au ya kuona video mbalimbali au Misikitini kutoka kwa wasomaji Qur-aan mbalimbali walio mashuhuri.
➡Kawaida au Mazoea hayo, haina dalili yoyote katika shariy’ah.
✅Bali ni kinyume na ilivyothibiti kutoka kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na waja wema waliotangulia).
✅Baada ya kumaliza kusoma Qur-aan usiseme ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’, lakini sema hivi⤵
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أشهد أن لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك
“Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika, Ash-hadu Allaa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa Atuwbu ilayka.”
✅Ni jambo la ki-Sunnah ambalo wanaghafilika nalo watu wengi baada ya kumaliza kusoma Qur-aan.
Dalili
➡Ushahidi juu ya hilo ni Hadiyth kutoka kwa mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) aliposema⤵
“Hajapatapo kukaa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kikao chochote na wala hajawahi kusoma chochote kwenye Qur-aan , na wala hajaswali Swalaah yoyote ila alikhitimisha (alimalizia kikao hicho) kwa maneno (fulani).
Nikasema:
“Ee Rasuli wa Allaah, ninakuona hukai kikao chochote, wala humalizi kusoma Qur-aan, wala humalizi kuswali Swalaah yoyote ila unakhitimisha (unamalizia) kwa kusema maneno hayo?
⏩Akasema Mtume Muhammad ( Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)⤵
“Ndio, yeyote ambaye atasema khayr atakhitimishiwa khayr hiyo. Na ambaye atazungumza maovu basi maneno (haya) yatakuwa ni kafara kwake (kwa yale maovu aliyoyasema katika kikao chake hicho).
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، أشهد أن لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْك
“Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika, Ash-hadu Allaa ilaaha illa Anta, Astaghfiruka wa Atuwbu ilayka.”
[Umetakasika Ee Rabb wangu, na Himidi ni Zako, Nashuhudia kwa hapana muabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Nakuomba maghfirah na natubia Kwako.]
↪Hadiyth hii Isnaad yake ni sahihi kaitoa Imaam An-Nasaaiy kwenye ‘Sunan Al-Kubraa.’
⏩Na amesema Al-Haafidhw Ibn Hajr katika ‘An-Nukat’, mj. 2, uk. 733, kuwa Isnaad yake ni sahihi.
⏩Na amesema Imaam Al-Albaaniy katika ‘Silsilat Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah, mj. 7, uk. 495, kuwa Isnaad hii ni sahihi vilevile kwa sharti ya Imaam Muslim.
⏩Na amesema Shaykh Muqbil Al-Waadi’iy katika ‘Al-Jaami’ Asw-Swahiyh Mimmaa Laysa Fiy Asw-Swahiyhayn, mj. 2, uk. 128, kuwa Hadiyth hii ni sahihi.
⏩Imaam An-Nasaaiy kaikusanya Hadiyth hii kwenye Sunan yake na akaiwekea mlango aliouita, “Chenye (Maneno) Kukhitimishiwa Kisomo Cha Qur-aan.”
✅Hivyo basi, baada ya ushahidi huo juu, na kukosekana ushahidi wa yale yaliyozooleka na watu wengi, kusema ‘Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym’ baada ya kumaliza kusoma Qur-aan ni bid’ah; jambo lililozushwa katika Dini, na hivyo, watu wajiepushe na matumizi ya neno hilo katika mahali hapo.
➡Kwahiyo Ndugu zangu katika Imaani, kulijaalia neno (Swadaqa Allaahu Al-‘Adhwiym) na mfano wake kuwa ndio la kukhitimishia kisomo cha Qur-aan ni bid’ah (uzushi).
✅Kwa sababu haijathibiti kutoka kwa Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliyasema hayo maneno baada ya kumaliza kisomo cha Qur-aan.
➡Na lau yangekuwa maneno hayo yapo kishariy'ah basi angeyasema mwisho wake ( wakati anapomaliza kusoma Qur-aan).
➡Na kwa hakika imethibiti kutoka kwake kwamba amesema⤵
"Yeyote atakayezua katika jambo (Dini) letu, lile ambalo halimo humo, basi atarudishiwa.”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy na Muslim
Wa bi-LLaahit-Tawfiyq wa Swalla Allaahu ‘alaa Nabiyyinaa Muhammad wa aalihi wa Swahbihi wa sallam.
Rejea Kitab Al-Lajnatu Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilmiyyah Wal-Iftaa [Fatwa Namba 7306
Na Allaah anajua zaidi
Nawatakia Usiku Mwema Ndugu zangu katika Imaani.Nawapenda sana kwa ajili ya Allaah.
Allaah Awahifadhi Wote.
http://bit.ly/2W5exzo i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni