SWALI
Je, inajuzu kwa mwanamke ambaye hajaolewa kwenda Msikitini wakati wa futari, kisha abakie Msikitini mpaka ifike wakati wa Taraawiyh? Na je inajuzu kwake kufanya I’tikaaf siku 10 za mwisho Msikitini?
JIBU
Lililo asili na bora zaidi ni kuwa Swalaah ya mwanamke aswali nyumbani. Lakini kwenda (mwanamke) Msikitini, kama haitosababisha fitnah inajuzu.
Anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
"Ikiwa mmoja wenu mke wake atamuomba ruhusa ya kwenda, asimkatalie".
Na anasema 'Aaishah (Radhwiya Allaahu 'anhaa):
"Alikuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akiswali Swalaatul-Fajr, wakihudhuria naye Swalaah waumini wanawake, wakirudi (majumbani kwao) hakuna aliyekuwa akiwajua kutokana na giza".
Kwa hiyo wanaweza kwenda kuswali Msikitini ikiwa kama haitosababisha fitnah, na wajisitiri vizuri, na wasichanganyike na wanaume.
Hali kadhalika wanaweza kwenda kufanya I’tikaaf Msikitini kama hakutokuwa fitnah.
http://bit.ly/2YA2SGA i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni