Swali
Asalam Alaikum warahmatu Allahi wabarakat. Swali langu . Hiv endpo wanandoa wamefanya tendo landoa ndani ya usiku we Ramadhan baadayakumalza wakapitiwa na usingizi bila ya kuoga na wakaka asubuhi je fungayao itakaje .
Jibu
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
Ila Swali lako nitalijibu kwa kirefu kidogo ili niweke msisitizo kwasababu hapo kuna mambo mawili.
Jambo la Kwanza Ni Swawm na jambo la pili ni Swalah ya Faradh ya Alfajir.
Napenda kuwapa nasaha kuwa haipasi kufanya mchezo na amri za Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na Mjumbe Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Amri za kufunga Swawm, kuitimiza ipasavyo, kwa wakati wake na ruhusa ya kufanya yote anayojizuia mja kwa wakati wake yanapaswa yote yatekelezwe bila ya kwenda kinyume au kudharau.
Swalah ya Alfajiri hata bila ya kuwa na Swawm inampasa Muislamu aitekeleze kwa wakati wake nao ni kuanzia Alfajiri hadi kabla ya jua kuchomoza.
Sasa vipi Muislamu asiswali asubiri hadi jua lichomoze ndio atake kuswali....*
Huo utakuwa sio tena wakati wa Swalah hiyo, kwa hivyo utakuwa hukutimiza Swalah hiyo ya Alfajiri kamakamakama ilivyothibiti katika Hadiyth ifuatayo: kupitiwa na usingizi au kusahau ilivyowekewa muda wake maalumu.
Isipokuwa tu ikiwa umefikwa na udhuru wa mambo yaliyoruhusu sheria
((من نسي صلاة أو نام عنها ، فكفارتها أن يصليها إذا ذكرها، لا كفارة لها إلا ذلك)) رواه مسلم
((Atakayesahau Swalah au ikampita akiwa amelala basi kafara yake ni kuiswali atakapokumbuka, hakuna kafara isipokuwa hiyo))
↪Imepokelewa na Imaam Muslim
Ikiwa hali yako ilikuwa baina ya mambo hayo mawili; kulala au kusahau hizo mbili basi unatakiwa haraka ufanye ghuslu na uswali, na uendelee na Swawm yako.
Na ikiwa umefanya makusudi basi unatakiwa uombe Tawbah kwa Mola wako na uazimie kutokurudia tena, na undelee na Swawm yako na itakuwa imesihi ila itakuwa imepunguka thawabu zake kwa dharau ya kutokutimiza amri.
Fahamu kuwa pamoja na kuwa umepewa udhuru wa kulala, lakini wewe na Mola wako ndio mnaojua nia haswa na ukweli wa kutoweza kwako kuamka, kwani kuna njia nyingi za kumwezesha mtu kuamka anapotaka, nazo ni kuweka alamu ya saa, kumuomba mtu amwamshe na njia zinginezo nyingi.
Hivyo, hakikisha umetumia njia zote hizo ikiwa kweli unamcha Mola wako na unajali Dini yako.
Ama ingelikuwa umewahi kufanya ghuslu/Kuoga Asubuhi kabla ya jua kuchomoza basi kusingelikuwa na ubaya wowote kwani hivyo imeruhusiwa na hakuna dhambi kufanya hivyo. Dhambi ni kujiachia hadi jua lichomoze na kukosa kutimiza fardhi.
Na Allaah anajua zaidi.
http://bit.ly/2DP4Gn0 i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni