Nini Hukmu Ya Mu’takif Kutoka Katika I’tikaaf?
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
Ama kutoka kwake kutoka Masjid, ‘Ulamaa wameigawa katika sehemu tatu:
- Inafaa: nayo ni kutoka kwa jambo lisokuwa na budi kutendwa linalokubalika ki-shariy’ah mfano kutoka kuswali jamaa’ah au jambo la kimaumbile kama kukidhi haja kama vile kwenda msalani kukojoa na chooni.
- Kutoka kwa ajili ya utiifu isiyomwajibika kama kumtembelea mgonjwa, au kuhudhuria janaazah basi hiyo ikiwa alijiwekea sharti mwanzo wa I’tikaaf yake, basi haina ubaya. Lakini ikiwa hakujiwekea sharti basi haipasi.
- Kutoka katika jambo linalopinga hukmu ya I’tikaaf kama vile kufanya biashara, na kujamiiana na ahli yake na kadhaalika. Haya hayajuzu ikiwa kwa kuweka sharti au kutokuwekea sharti (I’tikaaf yake).
[Majmuw’ Al-Fataawaa (20/157)]
http://bit.ly/2YA34pi i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni