Swali: Baadhi ya watu wanaoweza kusimama wanakaa katika Rak´ah ya pili ya Fajr mpaka pale imamu anapokaribia kwenda katika Rukuu´ hapo ndipo wanasimama na kurukuu pamoja naye. Je, swalah zao sahihi?
Jibu: Hapana. Ameacha nguzo ambayo ni ya kusimama. Ni lazima asimame kabla ya Rukuu´ chinichini kwa kiasi angalau cha kusoma al-Faatihah. Akisimama chini ya hapo pasi na udhuru, basi swalah yake si sahihi, kwa sababu ameacha nguzo. Zindukeni juu ya hili.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2VbSx6k
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni