Swali: Mimi ni msafiri na sijaswali Maghrib wala ´Ishaa. Nikaingia msikitini na wao ndio wanaanza kuswali ´Ishaa. Nikajichelewesah Rak´ah moja katika swalah ya ´Ishaa na nikakamilisha zilizobaki kwa nia ya Maghrib. Ndugu mmoja ananikataza na kwamba eti kitendo changu kinapingana na Sunnah na kwamba ni kosa. Ni yepi maoni yako juu ya swalah yangu?
Jibu: Mtu akija hali ya kuwa ni msafiri na akaingia msikitini akakuta watu wanaswali ´Ishaa, akiwakuta katika Rak´ah ya pili basi anuie Maghrib na atoe Tasliym pamoja na imamu. Kwa sababu katika hali hiyo atakuwa ameswali Rak´ah tatu. Akiwakuta katika Rak´ah ya tatu, anuie Maghrib na kuswali pamoja nao Rak´ah mbili kisha imamu akitoa Tasliym asimame katika Rak´ah ya tatu. Akijiunga nao katika Rak´ah ya kwanza aingie nao kwa kunuia Maghrib. Pindi imamu ataposimama kwa ajili ya Rak´ah ya nne basi yeye abaki chini na anuie kujitenga, asome Tashahhud, atoe Tasliym kisha ajiunge pamoja na imamu katika yale yatayokuwa yamebaki katika swalah ya ´Ishaa.
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2ZMPhx1
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni