Tafswiyr-ul-Anaam bi Sharh Nawaaqidh-il-Islaam
Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Assalaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Dibaji ya "Nawaaqidh-ul-Islaam"
Himdi zote zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na salaam zimwendee Nabii na Mtume bora kabisa Mtume wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote.
Amma ba´d:
Huu ni ufafanzui wa kijitabu "Nawaaqidh-ul-Islaam" kilichokusanya Imaam na Shaykh msafishaji Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah).
Haya ndio mambo kumi muhimu zaidi yanayotengua Uislamu. "Mambo yenye kutengua" ni wingi wa "kitenguzi". Kitu chenye kutengua maana yake ni kitu chenye kubatilisha na kuharibu. Mambo yenye kutengua Uislamu maana yake ni mambo yenye kuuharibu na kuubatilisha Uislamu. Kwa msemo mwingine ina maana ya kwamba mtu akifanya moja katika mambo haya Uislamu na dini yake vinabatilika. Matokeo yake anatoka katika dini ya Uislamu na kwenda katika dini ya washirikina - tunaomba Allaah atukinge.
Badala ya kuwa muislamu anakuwa mshirikina. Isipokuwa ikiwa kama atatubu kabla ya kufa. Asipotubu kabla ya kufa baada ya kufanya moja katika mambo haya anatoka katika Uislamu na anakuwa mshirikina. Kwa hivyo mambo yenye kutengua maana yake ni mambo yenye kubatilisha na kuharibu. Ni kama mfano wa mambo yenye kutengua wudhuu´.
Moja katika mambo hayo ni chenye kutoka kupitia ima tupu ya mbele au ya nyuma. Mtu akitawadha kisha akatokwa na mkojo au kinyesi wudhuu´ wake unabatilika na kuharibika. Hivyo anatoka katika hali ya kuwa na wudhuu´ na kwenda katika hali ya hadathi. Vivyo hivyo mambo haya yenye kutengua Uislamu. Mtu atapofanya moja katika mambo haya yenye kutengua Uislamu anatoka katika Uislamu na kwenda katika ukafiri.
Imaam (Rahimahu Allaah) amefupisha juu ya haya mambo kumi kwa sababu ndio mambo muhimu zaidi yenye kutengua Uislamu. Sababu nyingine ni kwa kuwa mambo mengi yanayoutengua Uislamu yanarejea katika mambo kumi haya.
01. Uwajibu wa kuyajua mambo kumi yanayotengua Uislamu
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
"Tambua ya kwamba mambo yanayotengua Uislamu ni kumi."
MAELEZO
Haya ni maamrisho ya elimu. Elimu maana yake ni mtu kuwa na uyakinifu. Kwa msemo mwingine tambua na uwe na yakini ya kwamba Uislamu unatenguka kwa kufanya moja katika mambo haya kumi yenye kutengua Uislamu.
Kuwa na elimu kinyume chake ni kuwa na dhana. Elimu kwa maana nyingine ni yakini. Kuwa na yakini na utambue kuwa mtu akifanya moja katika mambo haya kumi yenye kutengua Uislamu anatoka katika Uislamu.
Kuwa na utambuzi wenye azma pasi na shaka na ubabaikaji. Usidhanie. Bali kinyume chake unatakiwa kuazimia na utambue kweli kweli ya kwamba Uislamu unatenguka kwa kufanya moja katika mambo haya kumi.
02. Mosi: Kushirikisha katika ´ibaadah
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah (Ta´ala). Allaah (Ta´ala) amesema:
َّن اللَّ ِ إ ُ َ َشاء ن ي َ م ِ َك ل ِ ل َٰ وَن ذَ ُ ا د َ م ُ ر ِ ْف غ َ يـ َ و ِ ه ِ َك ب َ ُ ْشر أَن ي ُ ر ِ ْف غ َ ََل يـ َ ـه
"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae."04:47
النَّ ُ اه َ أْو َ م َ َ و نَّة َ ا ْْل ِ ه ْ َي ل َ ع ُ ـه اللَّ َ َّم ر َ َ ْد ح َق فـ ِ ـه اللَّ ِ ُ ْشِرْك ب ن ي َ م ُ نَّه ِ إ ُ ۖ ا ر ار َ أَنص ْ ن ِ َني م مِ ِ ال لظَّ ِ ا ل َ م َ و "
Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni - na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”05:72
MAELEZO
Hili ndio jambo la kwanza linalovunja Uislamu. Nalo ni kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah (Ta´ala).
Dalili ya kwanza kuhusu hukumu ya mshirikina duniani ni maneno Yake (Ta´ala):
ُ َ َشاء ن ي َ م ِ َك ل ِ ل َٰ وَن ذَ ُ ا د َ م ُ ر ِ ْف غ َ يـ َ و ِ ه ِ َك ب َ ُ ْشر أَن ي ُ ر ِ ْف غ َ ََل يـ َ ـه َّن اللَّ ِ إ
"Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa, lakini anasamehe yasiyokuwa hayo kwa Amtakae."
Kwa hiyo dhambi yake haisamehewi. Makusudio hapa ya neno "shirki" kunamaanishwa shirki kubwa. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amefanya kuwa ni maalum na kulifungamanisha. Amefanya shirki kuwa ni maalum ya kwamba haisamehewi na akafungamanisha yaliyo chini ya shirki na utashi Wake.
Dalili ya pili ni kuhusu hukumu yake Aakhirah. Hukumu yake Aakhirah ni kwamba Pepo ni haramu kwake na atadumishwa Motoni milele. Amesema (Ta´ala):
ُ النَّار ُ اه َ أْو َ م َ َ و نَّة َ ا ْْل ِ ه ْ َي ل َ ع ُ ـه اللَّ َ َّم ر َ َ ْد ح َق فـ ِ ـه اللَّ ِ ُ ْشِرْك ب ن ي َ م ُ نَّه ِ ۖ ا ر إ َ أَنص ْ ن ِ َني م مِ ِ ال لظَّ ِ ا ل َ م َ و
"Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah atamharamishia Pepo na makazi yake yatakuwa ni Motoni - na madhalimu hawatopata mwenye kunusuru yeyote.”
03. Yanayopelekea kwa kufanya mambo kumi haya
Mambo yakishakuwa namna hii ya kwamba hukumu yake duniani ni kuwa hasamehewi na Aakhirah ni mwenye kudumishwa Motoni milele na Pepo ni haramu kwake, kuna hukumu kadhaa zinazopelekea hapa duniani. Baadhi ya hukumu hizo ni hizi zifuatazo:
1- Mke wake anatengana naye - ikiwa ni muoaji. Inatakiwa kumtenganisha baina yake yeye na mke wake. Isipokuwa ikiwa kama atatubu. Wanatenganishwa kwa sababu yeye mke wake ni muislamu na mume ni kafiri. Haifai kwa mwanamke wa Kiislamu akabaki chini ya usimamizi wa kafiri. Allaah (Ta´ala) amesema:
َُّن وَن ََّل ُّ ل ََيِ ْ ُم ََل ه َ و ْ ُم ََّّل لٌّ ُ َّن حِ ََل ه
"Wao si [wake] halaal kwao [hao makafiri] na wala wao si [waume] halaal kwao." 63:10
Bi maana makafiri.
َّن ِ م ْ ؤ ُ يـ ََّّتَٰ َ ِت ح ْشِرَكا ُ وا الْم ُ ح نكِ َ ََل ت َ و
"Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini."02:221
2- Haitakiwi kumswalia wala kumuosha wakati atapokufa.
3- Hazikwi kwenye makaburi ya waislamu.
4- Asiingie Makkah. Haijuzu kwa mshirikina kuingia Makkah. Allaah (Ta´ala) amesema:
ََٰذ ـ َ ه ْ ِهم ِ ام َ َ ع ْد ع َ بـ َ ام َ ر َ ا ْْل َ د ْجِ َس وا الْم ُ ب َ ْر ق َ ََال يـ ف ٌ َس ْشِرُكوَن ََن ُ ََِّّنَا الْم ُوا إ ن َ آم َ ين ِ ا الَّذ َ ه ُّ ا أَيـ َ ي ا
"Enyi mlioamini! Hakika washirikiana ni najisi, basi wasikaribie al-Masjid al-Haraam baada ya mwaka wao huu."09:28
5- Hana haki ya kurithi wala ya kurithiwa. Ikiwa mke na watoto wake ni waislamu wasimrithi. Mali yake inaenda kwenye sanduku la waislamu. Isipokuwa ikiwa kama ana mtoto ambaye ni kafiri, ana haki ya kumrithi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
"Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi muislamu." al-Bukhaariy (6764) na Muslim (1614).
Kwa hivyo tunapata kuona kuwa akifanya moja katika mambo haya kumi yanayotengua Uislamu inapelekea katika hukumu kadhaa; haoshwi, haswaliwi, hazikwi makaburini pamoja na waislamu, harithi na wala harithiwi, mke wake anatenganishwa naye na haingii Makkah. Jengine ni kuwa akifa juu ya hilo dhambi yake haisamehewi na Pepo ni haramu kwake. Ni katika watu wa Motoni ambaye atadumishwa humo milele.
04. Nini maana ya ´ibaadah?
Mwandishi (Rahimahu Allaah) amesema:
"Kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah (Ta´ala)."
Ili tuweze kutambua shirki ni lazima kwetu kwanza kujua shirki ni kitu gani.
´Ibaadah ni yale maamrisho na makatazo yote yaliyokuja katika Shari´ah. Yale yote yaliyoamrishwa na Shari´ah, sawa iwe ni maamrisho ya uwajibu au maamrisho ya kupendekeza au imeyakataza, sawa iwe ni makatazo ya uharamu au makatazo ya kuchukiza.
Maamrisho ikiwa ni ya wajibu basi ni lazima kuyatekeleza na ikiwa yamependekezwa imependekezwa kuyatekeleza. Kadhalika inapokuja katika makatazo; ikiwa ni makatazo ya uharamu ni wajibu kuyaacha na ikiwa ni makatazo ya kuchukiza imechukizwa kuyafanya.
Vilevile unaweza kusema ´ibaadah ni jina lililokusanya kila ambacho Allaah anakipenda na kukiridhia, sawa katika maneno au matendo, ya ndani na ya nje.
Kwa hivyo ´ibaadah ni kila amrisho au katazo lililokuja katika Shari´ah. Kwa mfano swalah ni ´ibaadah. Zakaah ni ´ibaadah. Swawm ni ´ibaadah. Hajj ni ´ibaadah. Uwekaji nadhiri ni ´ibaadah. Kuchinja ni ´ibaadah. Du´aa ni ´ibaadah. Kutegemea ni ´ibaadah. Shauku ni ´ibaadah. Woga ni ´ibaadah. Kupigana Jihaad katika njia ya Allaah ni ´ibaadah.
Kuamrisha mema na kukataza maovu ni ´ibaadah. Kuwafanyia wema majirani ni ´ibaadah. Kuwaunga ndugu ni ´ibaadah. Kadhalika makatazo. Muislamu anatakiwa kuacha makatazo kwa ajili ya kumuabudu Allaah. Anatakiwa kuacha shirki, kuacha kuua watu na kushambulia mali zao na kukiuka heshima zao na kupinga haki. Anafanya ´ibaadah kwa kuacha maovu haya ikiwa ni pamja vilevile na uzinzi, kunywa pombe, kuwaasi wazazi wawili, kusengenya, kueneza uvumi na kufanya ribaa. Yote haya ni ´ibaadah.
Kwa hiyo ´ibaadah ni maamrisho na makatazo. Inapokuja katika maamrisho unayafanya. Na inapokuja katika makatazo unayaacha. Yote mawili kwa ajili ya kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall).
05. Aina mbili za maamrisho na makatazo
Maamrisho yamegawanyika aina mbili.
a) Maamrisho ya uwajibu.
b) Maamrisho ya kupendekeza.
Maamrisho ya uwajibu ni kama swalah. Kwa kuwa swalah ni wajibu. Maamrisho ya kupendekeza ni kama kutumia Siwaak. Imependekezwa.
Makatazo yamegawanyika aina mbili:
a) Makatazo ya uharamu.
Kwa mfano makatazo ya uzinzi.
b) Makatatazo ya kuchukiza.
Ni kama mfano wa makatazo ya kuzungumza baada ya swalah ya ´Ishaa. Ni mamoja katika hayo matendo yawe ya nje, kama mfano wa swalah na swawm; au yawe ya ndani, kama mfano wa nia, Ikhlaasw, ukweli na mapenzi. Kadhalika makatazo ni mamoja yawe ya nje, kama mfano wa uzinzi; au ya ndani, kama mfano wa majivuno, kiburi, kujionyesha, vifundo, chuki na hasadi. Yote hayo yamekatazwa na hivyo mtu anatakiwa kuyaacha.
Kwa hivyo ´ibaadah imekusanya maamrisho na makatazo ya maneno na matendo, sawa ya nje na ya ndani ambayo yamethibiti katika Shari´ah. Mtu akifanya aina moja wapo miongoni mwa ´ibaadah hizi akamfanyia asiyekuwa Allaah anamtubukia katika shirki.
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
"Katika hayo ni pamoja vilevile na kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah. Kwa mfano mtu anayechinja kwa ajili ya jini au kaburi."
MAELEZO
Mwandishi (Rahimahu Allaah) amepiga mfano kwa kusema:
Mwandishi (Rahimahu Allaah) amepiga mfano kwa kusema:
"... kama mfano wa kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah."
Kuchinja ni ´ibaadah. Allaah (Ta´ala) amesema:
ُ َك لَه َني ََل َشِري الَمِ َ الْع ِبِّ َ ر ِ ـه لَّ ِ اِِت ل ََ َم َ و َ اي َ ََْمي َ ي و كِ ُ ُس ن َ َالِِت و َ َّن ص ِ إ ْ ُل ق
"Sema: “Hakika Swalaah yangu na kichinjwa changu na uhai wangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Allaah Pekee, Mola wa walimwengu - hana mshirika."06:162-163
ر ِ ل ِّ ِل َ َص ف ْ ر َ ا ْْن َ ِّ َك و بِ
"Basi swali kwa ajili ya Mola wako na chinja kwa ajili Yake." 108:02
Endapo mtu atafanya ´ibaadah akamfanyia asiyekuwa Allaah atahesabika amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah. Kwa hiyo anakuwa mshirikina. Mwandishi amepigia mfano hilo na kusema kama kuchinjia kwa ajili ya jini.
Mtu akilichinjia jini au akamchinjia aliyemo ndani ya kaburi amefanya shirki. Kadhalika akilichinjia kaburi, nyota au walii anakuwa mshirikina.
Mfano mwingine ni du´aa. Akimuomba asiyekuwa Allaah, kwa mfano mtu akamuomba uokozi asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah, mtu akaomba ponyo kutoka kwa asiyekuwa Allaah, mtu akaomba kuyaondosha matatizo kutoka kwa asiyekuwa Allaah, mtu akaomba msaada kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah, mtu akaomba kinga kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah au mtu akaomba uokozi kutoka kwa asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah. Yote haya ni shirki.
Miongoni mwa ´ibaadah vilevile ni kuwatii viumbe katika kuhalalisha na kuharamisha. Kwa mfano mtu akamtii kiongozi, waziri, mwanachuoni, mja, baba, mke au bosi katika kuhalalisha haramu au kuharamisha halali. Hii pia inakuwa shirki kwa sababu amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah.
Kwa sababu Allaah (Ta´ala) ndiye mwenye haki ya kuhalalisha na kuharamisha:
ُ ـه اللَّ ِ ه ِ أْذَن ب َ ي ْ ا ََل َ ي ِن م ِّ ِ الد َ ِّن ِ ُم م وا ََّل ُ ع َ َشر ُ َكاء َ ْ ُشر ُم ََّل ْ أَم
"Je, wanao washirika waliowaamuru Dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea kwayo idhini?" 42:21
Mfano mwingine ni mtu kumfanyia Rukuu´ asiyekuwa Allaah, akamfanyia Sujuud asiyekuwa Allaah, akafanya Twawaaf kusipokuwa Ka´bah hali ya kuwa ni mwenye kujikurubisha, akaweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, akanyoa kichwa chake kwa ajili ya asiyekuwa Allaah - kama mfano wa Suufiyyah ambapo wamkuta mmoja wao amenyoa kichwa chake kumnyolea Shaykh wake hali ya kuwa ni mwenye kumuabudu na anamfanyia Rukuu´ na Sujuud - akatubu kwa ajili ya asiyekuwa Allaah - kama mfano wa Suufiyyah ambao wanatubu kwa ajili ya Mashaykh zao, Shiy´ah ambao wanatubu kwa ajili ya viongozi wao au manaswara ambao wanatubu kwa ajili ya wachungaji.
Tawbah ni ´ibaadah. Amesema (Ta´ala):
ُ ـه ََِّل اللَّ َب إ ُو ذن ُّ ال ُ ر ِ ْف غ َ ن يـ َ م َ و
"Na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah."03:135
Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) vilevile amepokea kupitia kwa al-Aswad bin Sariy´a ambaye ameeleza kuwa Biasiyr alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akamwambia: "Ee Allaah! Hakika mimi natubu Kwako na natubu kwa Muhammad." Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwambia:
"Mpe haki Mwenye nayo." Ahmad (03/435)
Allaah (Ta´ala) ndiye mwenye kusamehe. Allaah (Ta´ala) ndiye mwenye kustahiki kufanyiwa Tawbah. Kwa hivyo endapo mtu atatubu kwa asiyekuwa Allaah ametumbukia katika shirki kwa sababu amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah. Kwa hivyo mwandishi (Rahimahu Allaah) anasema kuwa kitenguzi cha kwanza ni kufanya shirki katika ´ibaadah ya Allaah.
Tumejua kuwa ´ibaadah ni jina lililokusanya kila anachokipenda Allaah na kukiridhia katika maneno na vitendo, sawa ya ndani na ya nje. Mtu akifanya aina yoyote ile ambayo imethibiti katika Shari´ah kuwa imeamrishwa, sawa iwe ni maamrisho ya uwajibu au ya kupendekezwa, au iwe imethibiti katika Shari´ah kuwa imekatazwa, sawa iwe ni makatazo ya uharamu au ya kupendekezwa, akifanya kitu katika hayo kumfanyia asiyekuwa Allaah anatumbukia katika shirki.
Ambaye anamfanyia maamrisho asiyekuwa Allaah au akaacha makatazo kumfanyia asiyekuwa Allaah ametumbukia katika shirki. Mwandishi amepiga mfano wa kuchinja. Mifano mingine ni kama du´aa, kuomba kinga, kuomba uokozi, kuweka nadhiri, Rukuu´, Sujuud, Twawaaf, kutegemea, khofu, matarajio, kunyoa kichwa na mengineyo katika aina za ´ibaadah. Mtu akifanya moja katika mambo haya kumfanyia asiyekuwa Allaah ametumbukia katika shirki na hilo litampelekea katika hukumu zifuatazo:
a) Hasamehewi.
b) Mke wake anatengana naye endapo hatutubia papo hapo.
c) Haingii Makkah.
d) Harithi wala harithiwi.
e) Haoshwi.
f) Haswaliwi.
g) Akifa hazikwi pamoja na waislamu kwenye makaburi yao.
h) Kuhusu Aakhirah ni katika watu wa Motoni na Pepo ni haramu kwake.
Usikose Sehemu ya 2, Tutaendela In Shaa Allaah............
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2RcIQ1r
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
SWALI: Assalaam alaykum Naomba maana ya majina yeyote tuwapao watoto wetu AU mnielekeze wapi naweza kupata labda katika kitabu cha fas...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni