Abu Bakar Swidiq (Radhwiya Allahu Anhu) ndiye Swahaba aliyeamrisha Qur'an ikusanywe na kuwekwa kwa Maandishi katika Mswahafu.
Surat An-Naswr Ndiyo Surah ya Mwisho Kuteremshwa.
Surat Asw-Swaff ndio Surah pekee iliyotaja Jina la Ahmad kumkusudia Mtume Muhammad( Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam).
Swali Je,Jina la Mtume Muhammad( Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam) limetajwa mara ngapi katika Qur'an likiwepo pia jina la Surah...?
Jibu Limetajwa Mara 4 , (Surat Aal-Imraan , Surat Al-Ahzaab, Surat Muhammad na Surat Al-Fat-h )
Swali Swahaba gani aliamrishwa Qur'an iandikwe kwa lahja moja ya Kiquraysh...?
Jibu Uthman Bin Affaan (Radhwiya Allahu Anhu).
Swali Je,Qur'an iliteremshwa kwa Herufi (Lahaja) ngapi za Ki Quraysh ...?
Jibu Herufi 7
Swali Qur'an iliteremshwa kwa miaka mingapi kwa Mtume Muhammad( Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam)..?
Jibu Miaka 23
Swali Kuna Maeneo mangapi ya Sajdah ya Kisomo katika Qur'an ....?
Jibu Maeneo 15
Surat Al-Baqarah Ndiyo Surah Ndefu kuliko Zote katika Qur'an.
Katika Qur'an Kuna jumla ya Ayah 6236 na Katika Qur'an Kuna Surah 114 na Qur'an ina jumla ya Juzuu 30.
Surah zilizoteremshwa MAKKAH ndio zilizo nyingi Kuliko Surah zilizoteremshwa MADIYNAH.
Surat Al-Kawthar Ndio Surah Fupi kuliko Surah zote ndani ya Qur'an Tukufu.
Swali Nini Maana ya Qur'an...?
Jibu KINACHOSOMWA
Surat At-Tawbah Ndiyo Surah Pekee ndani ya Qur'an isiyoanza na BISMILLAAH.
Aayah Tano za Mwanzo Surat 'Alaq ndio Ayah za Mwanzo kuteremshwa kwa Mtume Muhammad( Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam)
Swali Mara ngapi Bismillaah imerudia katika Qur'an..?
Jibu Mara 114
Swali Surah ipi ambayo Allaah Ameiapia kuhusu Wakati ,ambayo Imaam Shaaffiiy amesema: "Kama isingeteremshwa Surah nyingine ila hii ingeliwatoshelewa watu.."?
Jibu Surat Al-Aswr
Surat An-Naml Ndiyo SURAH ambayo BismilLaah imejirudia mara mbili
Surat Al-Kahf Ndiyo SURAH ambayo inakiwa Kusomwa katika Siku ya Ijumaa.
Ayaah Ndefu kuliko Zote zinajulikana kwa jina la Ayyaatul-Mudayyanah au Ayyaatud-Dayn
Mwezi wa Ramadhwaan Ndiyo Mwezi pekee katika Miezi 12 ya Kiislamu uliotajwa katika Qur'an
Surat Al-Hadiyd Ndiyo Surah Pekee iliyokusanya Majina na Sifa za Allaah( Subhaana wa Taala) zipatazo 27.
Surat Al-Ikhlaasw Ndiyo Surah Pekee ambayo Ukiisoma utapata Thawabu (1/3) ya Qur'an.
Surat Al-Faatiha ndiyo surah inayojulikana kama "Mama wa Qur'an"
Shirk Ndiyo Dhambi kubwa iliyotajwa kuwa haitosehemewa katika Qur'an ikiwa Mtu hatotubia(Hatofanya Tawbah)
Al-Qiyaamah Ndiyo Surah ambayo ALLAAH ameitaja kuwa WAUMINI watamuona Allaah Al-Jaannah (Peponi).
Surat Al-Hujuraat na Surat Al-Humazah Ndiyo Surah ambazo zinazomkemea Msengenyaji.
Surat Al-Baqarah Aya 281 Ndiyo Ayah ya Mwisho Kuteremshwa katika Qur'an.
Malaika wa Msimamizi wa Moto ametajwa katika Qur'an kwa jina la Maalik
Swali Malaika wangapi wametajwa katika Qur'an kuwa wataibeba 'Arsh ya Allaah(Subhaana wa Taala) na wametjwa katika Surah gani..?
Jibu Malaika 8 wametajwa katika Surat Al-Haaqah.
Kuna Jumla ya Surah 37 katika Juzuu 30.
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2QvJOZD
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni