Aayah Na Mafunzo
Al-Baqarah
Mfano Wa Anayetoa Swadaqah Kwa Ikhlaasw Hulipwa Maradufu
وَمَثَلُ الَّذِينَ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمُ ابْتِغَاءَ مَرْضَاتِ اللَّـهِ وَتَثْبِيتًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ كَمَثَلِ جَنَّةٍ بِرَبْوَةٍ أَصَابَهَا وَابِلٌ فَآتَتْ أُكُلَهَا ضِعْفَيْنِ فَإِن لَّمْ يُصِبْهَا وَابِلٌ فَطَلٌّ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿٢٦٥﴾
265. Na mfano wa wale wanaotoa mali zao kutafuta radhi za Allaah na kujithibitisha nafsi zao ni kama mfano wa bustani iliyoko pahala paliponyanyuka; ikafikiwa hiyo bustani na mvua kubwa, ikatoa mazao yake maradufu, na hata kama haikufikiwa na mvua kubwa basi mvua ndogo huitosheleza. Na Allaah kwa muyatendayo ni Mwenye kuona.
Mafunzo:
Pia anayetoa kwa ikhlaasw na kwa kuficha kabisa swadaqah yake atakuwa miongoni mwa watu saba watakaokuwa katika kivuli cha Allaah ('Azza wa Jalla) Siku ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake.
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ ((سَبْعَةٌ يُظِلُّهُمْ اللَّهُ فِي ظِلِّهِ يَوْمَ لا ظِلَّ إِلا ظِلُّهُ: الإِمَامُ الْعَادِلُ، وَشَابٌّ نَشَأ فِي عِبَادَةِ رَبِّهِ، وَرَجُلٌ قَلْبُهُ مُعَلَّقٌ فِي الْمَسَاجِدِ، وَرَجُلَانِ تَحَابَّا فِي اللَّهِ اجْتَمَعَا عَلَيْهِ وَتَفَرَّقَا عَلَيْهِ، وَرَجُلٌ طَلَبَتْهُ امْرَأَةٌ ذَاتُ مَنْصِبٍ وَجَمَالٍ فَقَالَ إِنِّي أَخَافُ اللَّهَ، وَرَجُلٌ تَصَدَّقَ بِصَدَقَةٍ فَأَخْفَاهَا حَتَّى لا تَعْلَمَ شِمَالُهُ مَا تُنْفِقُ يَمِينُهُ، وَرَجُلٌ ذَكَرَ اللَّهَ خَالِيًا فَفَاضَتْ عَيْنَاهُ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (((Watu saba Allaah Atawafunika katika kivuli Chake, siku ambayo hakutokuwa na kivuli ila kivuli Chake; Imaam muadilifu, kijana ambaye amekulia katika ‘Ibaadah ya Rabb wake, mwanamume ambaye moyo wake umesehelea [au umeambatana] katika Misikiti, watu wawili wanaopendana kwa ajili ya Allaah; wanakutana kwa ajili Yake na wanafarikiana kwa ajili Yake, na mwanamme aliyetakwa na mwanamke mzuri mwenye kuvutia akasema: Mimi namkhofu Allaah, na mwanamme aliyetoa sadaka yake akaificha hata mkono wa kushoto usijue nini ulichotoa mkono wa kulia, na mwanamme aliyemkumbuka Allaah pekee macho yake yakatokwa machozi)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
from Alhidaaya.com https://ift.tt/2FQM0GY
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni