ASSALAAMUALAYKUM NDUGU ZANGU,
MIMI SIKU ZOTE NAAMKA SAA NANE ZA USIKU --- YAANI NA AMSHWA NATURALLY.
NINA SALI KWA MPANGO UFUATAO:
i. SUNNATIL-UDHUU RAKAA 2
ii. SUNNATI RASULULLAH (S.A.W.) RAKAA 2
iii. THAJJUD RAKAA 2
iv. SUNNA YA USIKU ULE RAKA ....KAMA ILVYOANDIKWA
v. SUNNATI HAJJAT RAKAA 2 ,2,2, MUJIBU WA HAJA
ZANGU.
vi. SUNNATI TAWBA RAKAA 2
vii. SALAATUL WITR RAKAA 3.
BY THE TIME NIMEWAHI ZOTE SWALAH YA FAJR NI TAYARI. NA ENDELEA KUFANYA ZIKRULLAH BAADA YA SWALAH YA FAJR MPAKA TIME YA ISHRAAQ NA TENA NAENDELEA KUWEPO KWENYE MSALA KWA ZIKRULLAH MPAKA SWALAH YA DHUHAA.
JEE NI FAFANULIENI WAPI NIMEKOSEA NA NIFANYE SAHIHI NAMNA GANI
JAZAAKALLAHUKHEIR FIIAMAANILLAH
Jibu
Wa Aleykum Sallaam WarahmatulLaah Wabarakatuh
Naan,Tunamshkuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuona dada zetu wako katika hima ya kufanya ibada ya Mola wao kiasi kama hikii cha ndugu yetu huyu Masha-Allah. Vile vile tunashukuru kuona kwamba dada yetu ana hamu ya kutaka kujua mafunzo sahihi ya ibada zake.
Hakika hili ni jambo muhimu sana kwa kila Muislamu kwani katika kufanya ibada yoyote ikiwa ya vitendo au kauli, lazima masharti mawili yapatikane ndipo ibada hiyo ikubaliwe nayo ni:
1) Ikhlaas – Iwe kwa kutaka Ridhaa ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na sio yenye Riyaa au sio yenye kutendeka kwa ajili ya maslahi ya kidunia.
2) Iwe inatokana na mafundisho ya Qur-aan na Sunnah. (kufanyika kwa mujibu wa mafunzo ya Qur-aan na Sunna sahihi).
Bila ya shaka sharti la kwanza dada yetu na wengi wetu tunalitimiza. Ama sharti la pili ndio baadhi yetu hatukulitambua ndipo tunapofanya ibada bila ya kupata dalili kutoka katika Qur-aan na Sunnah.
Tunakutajia hapa zilizo sahihi na zisizo sahihi kutokana na maelezo yako:
1.Sunnatul- Wudhuu Inaswali kwa Rakaa mbili Swalah ni Sahihi Ama Dalili kuwa Bilaal (Radhiya Allahu 'anhu) akiswali hata Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akaota nyao zake ziko peponi kwa kufanya hivyo.
2.Sunnatul-Rasuul (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Swalah hii si Sahihi na Wala hakuna Dalili yoyote
3.Tahajjud Swalah hii ni Sahihi Dalili zipo nyingi sana unaweza kusoma katika darsa mbalimbali kuhusu swalah za Sunnah ndani ya Blog hii Na Swalah hii Unaweza kuswali mbili, au nne, au sita au nane ukamalizia na tatu za Witr
4.Sunnah ya Usiku Swalah hii ni Sahihi Ni sawa tu na Tahajjud usiongeze zaidi ya hizo.
5.Sunnah ya Haja Swalah hii ni Dhaifu Imepingwa na Maulamaa kuwa ni Hadiyth dhaifu. Muislamu anaomba haja zake kwa kuomba du'aa kama kawaida.
6.Sunnati Tawbah Swalah hii ni Sahihi inaswaliwa Rakaa 2 Dalili nimezitaja katika DARSA la Tawbah katika Uislam soma katika Blog hii,Anapofanya mja dhambi anaswali Rakaa mbili kuomba maghfira.
7.Salaatul Witr Swalah hii ni Sahihi Rakaa 3 unamalizia baada ya kuswali 8 au chini yake za Tahajjud.
Unavyomalizia kuwa inafika Alfajiri kisha unaendelea kufanya dhikru-Allah hadi litoke jua kisha unaswali Swalah ya Dhuhaa ni sawa kabisa na fadhila zake ni kupata thawabu kama vile umetimiza Hajj na Umra kamili kutona na Hadiyth ifuatayo:
((عن أنس عن النبي صلى الله عليه وسلم ، أنه قال : من صلى الفجر في جماعة ثم قعد يذكر الله حتى تطلع الشمس ثم صلى ركعتين كانت له كأجر حجة وعمرة تامة تامة تامة) ) أخرج الترمذي صححه الألباني .
Imetoka kwa Anas kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeswali Alfajiri katika Jama'ah kisha akakaa anamkumbuka Allaah mpaka likachomoza jua kisha akaswali Raka'ah mbili, atapata ujira kama ujira wa kwenda Hajj na 'Umrah ulio kamili kamili kamili)) [Imetolewa na At-Tirmidhy na kaisahihisha Al-Albaaniy]
Tanbihi: Fadhila hizi anazipata pia mwanamke sawa sawa atakaposwali nyumbani kwake.
Tunakuombe dada yetu Allaah Azidi kukuelimisha upate kuona yaliyo haki uyafuate na ujiepushe na mambo ya uzushi yote.
Na Allaah Anajua zaidi
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2RwDiyU
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni