Translate

Ijumaa, 30 Novemba 2018

HIJABU YA MWANAMKE WA KIISLAMU NA MASHARTI YAKE

                                Assallaam   Aleykum  WarahmatulLaah  Wabarakatuh



Kwa hakika mwenye kufuatilia na kuchunguza aya za Qur an na sunna za mtume Muhammad وسلم عليه هللا صلى na athari za wema wa zama zilizopita katika mandhari hii inadhihirika kwamba mwanamke anapotoka nyumbani kwake inamwajibikia kustiri mwili wake wote na kwamba asidhihirishe chochote katika mapambo yake isipokuwa uso wake na viganja vyake kama atataka kwa aina yeyote au nguo yeyote katika vivazi ili mradi yatekelezeke masharti yafuatayo;-



SHARTI ZA HIJAB 


1. Ihifadhi mwili wote ila kilichovuliwa

2. Isiwe nipambo nguo yenyewe

3. Iwe ni nzito haitakashifu

4. Iwe ni pana haibani

5. Isiwe imefukizwa na kutiwa manukato

6. Isifanane na nguo ya mwanamme

7. Isiwe ni nguo ya umashuhuri


Zingatia;-Baadhi ya sharti haziwahusu wanawake tu bali wanashirikiana wanaume na wanawake kama isivyofichikana.


Vilevile basi baadhi wanaharamisha kiujumla, ni sawa akiwa yupo nyumbani au nje, kama shuruti tatu za mwisho lakini kwa maudhi yya upekuzi wetu ni kivazi cha mke pindi anoapotoka yakafika mazungumzo yetu hapo.hivyo usindhaniwe ni kufanya taklisi kwayo.

Na haya hapa ni uchumbuzi wake na dalili juu ya kile tulichokitaja



                                                                UTANGULIZI


 Shukrani zote njema zinamstahiki Allah mola wa walimwengu wote. Msemaji katika kitabu kitukufu,

“Enyi wanaadam, kwa hakika tumeteremsha juu yenu mavazi yanayoficha tupu zenu, na nguo za pambo. Na nguo za uchamungu ndio bora. Hii ni katika ishara za Allah ili mpate kukumbuka” .


Na sala na amani ziwe juu yake mtume aliyetumwa kuwa ni rehma kwa watu wote.

Tumekitunga kitabu hiki (au risala) kwa lengo la kuwabainishia dada zetu wa kiislam ni upi wajibu wa vazi la mwanamke pindi anapotoka nyumbani kwake na yapi masharti yanayoambatana na vazi hilo na adabu zake.


Hakuna litokalo akilini mwetu bali tumeyakusanya kwa ufupi tu yale yaliyomo katika kitabu cha HIJABU YA MWANAMKE WA KIISLAM KATIKA KITABU NA SUNNAH cha Sheikh Muhammad Naaswiruddin Albaniy (Allah amrehemu) ili kukurubisha faida yake kwa ndugu wa kiislam. Tumekamata yaliyo muhimu zaidi kwa lengo la kufupisha.


Namuomba Allah mtukufu anufaishe kwa kitabu hiki au risala hii wengi katika dada zetu khasa khasa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kwani wao ndio imekuwa sababu ya kitabu hiki baada ya kuombwa wengi katika mabinti kuhudhuria swala tano au pia maeneo ya msikiti bila ya kuzichunga adabu za mavazi na uhakika wake.


 Allah aliye juu awape kila la kheri na atuongoze sisi na wao katika njia iliyonyooka kwani hakuna uwezo wala nguvu illa kwake.



                                                        SHARTI LA KWANZA 


                                KUHIFADHI MWILI WOTE ILA KILICHOVILIWA: 


 Ni baadhi ya maeneo madogo to yaliyovuliwa na sharia. Amesema Allah aliyetukuka



 َ ف ْ ََي َ ن و َّ ِّ ـِّره َ ْص أَب ْ ن ِّ م َ ْ ُض ْضن غ َ ِّت يـ ـ َ ن ِّ م ْ ؤ ُ ْلم ِّ ُل ل ق َ ن َّ ُ ﴿و َُه َتـ َ ِِّزينـ َ ين ِدِّ ْ ْب ُ يـ َالَ َ ن و َّ ُ ُه َ وَج ُ ُر ُفـ َ َ ْظْن ا ُْه نـ ِّ م َ ر َ ا ظَُه َ م َِّالَّ إ ن َّ وِبِِّّ ُ ي ُ لَى َج َ ن ع َّ ِّ ِّره ُ ُم ِبِّ َ ْن َ ْضِّرب لْي َ و َ ين ِدِّ ْ ْب ُ يـ َالَ َ َِّالَّ ن إ َّ و ُ َُه َتـ َ ِِّزينـ َ ء ْ ن أَو َّ ُِّه ِّ ولََت ُ ع ُ ْبـ ِّ ُِّه ل ِّ ولََت ُ ع ُ بـ ِّ ء َ اَب َ ء ْ ن أَو َّ ُِّه ِّ ئ َ ن اَب َّ ا َ و ْ ِّخ إ ْ ن أَو َّ ُِّه ِّ ولََت ُ ع ُ بـ ِّ آء َ ن ْ أَبـ ْ ن أَو َّ ُِّه ِّ آئ َ ن ْ أَبـ ْ أَو َ و َ ِِّن أَخ َ ب ْ ن أَو َّ اِنِِّّ َ و ْ ِّخ ِِّن إ َ ب ْ ن أَو َّ ن ِِّّ ِن َّ ن ِتِِّّ َّ ُِّه ِّ آئ َ س ِّ ن ْ ا أَو َ م ْ أَو ن َّ ُ ُُه ـنـ َ ْْي ْت أَ لَ َك َ َني م ِّ ع ِّ َّـْب ِِّل ا ِّل أَِّو الَت ْ أُو ِّ ْ ِّل َغْي ا َ َِّج الر َ ن ِّ م ِّ ة َ ب ْ ر ْ َل َ ين ذِّ َّ ِّل ال ْ ف ِّ ِّت أَِّو الط َ ر ْ و َ لَى ع َ ْ ع وا ُ ر َ ْظُْه َ ي َالَ َ و ِّ آء َ س ِّ الن َ ُوَن لَع ن ِّ م ْ ؤ ُ الْم َ ه ُّ ً أَي يعا ََجِّ َِل ا ََّّللِّ ِّ إ ْ وا ُ ُوب ت َ و وَن﴾ ُ ح ِّ ل ْ ُف تـ ْ ُكم َّ ِّ ......... .... ل ل ُ َْج ِِّبَر َ ْن َ ْضِّرب ن ي َّ ُِّه


“Na sema kuwaambia waumini wakike waiinamishe macho yao na wahifadhi tupu zao na wala wasidhihirishe mapambo yao ila yale yaliyodhihiri, na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao ila kwa waume zao au baba zao au baba wa waume zao au watoto wao au watoto wa waume zao au ndugu zao au watoto wa ndugu zao au watoto wa dada zao au wanawake wenzao au wale inayowamiliki nikono yao ya kiume, au wafuasi wanaume wasio na matamanio au watoto ambao hawajajua mambo ya uke. Na wasipige chini miguu Yao ili kujulikana yale waliyoyaficha katika mapambo yao, Na rejeeni kwa Allah nyote enyi waumini ili mpate kufaulu” ………Surat an nuur: 31


Na kauli yake Allah Mtukufu


“Ewe Mjumbe, Sema kuwaambia wake zakona watoto wako wa kike na wake wa waumini wateremshe nguo zao, hilo litapelekea kujulikanwa na wala hawataudhiwa, na Allah amekuwa ni mwenye kusamehe na huruma” Katika aya hizi kuna uwazi na wajibu wa kusitiri mapambo yote ila yaliyodhihiri pasi na makusudio, wajibu wa kusitiriwa kwake mbele ya wanaume wanaofaa kuwaoa..."


Na katika maana  “…ila yaliyodhihiri….”, kwa hakika zimetofautiana sana kauli za wema waliopita katika tafsiri yake. Wapo waliosema “Hizo ni nguo za wazi yaani walizovaa juu wanammke” na wapo waliosema “Huo ni wanja, pete, Bangili, na uso” katika kauli za baadhi ya maswahaba na matabiina.

Bali makusudio kwa kile kilichovuliwa ni USO na VIGANJA VIWILI.


Hii ni sehemu yenye mzozo mbele ya wanazuoni kuwa Je uso ni Uchi au sio uchi? Je ni wajibu mwanamke kufunika au la?

 Hatupendi kurefusha maneno katika suala hili, kwani linahitaji muda na uwanja mpana lakini kilichowafikiwa na pande zote mbili ni kuwa INASUNNIWA kwa mwanamke kusitiri uso wake kwa kuvaa niqaab.


Hivyo ni haramu kwa mwanamke kudhihirisha chochote katika mwili hata nyayo ILA USO NA VIGANJA VIWILI.


Bali mtume (Swalallahu ‘alayhi wasallam) aliwataka wanawake waburuze nguo zao kwa lengo la kustiri dhiraa nzima.


JILBAAB: Ni nguo anayojifunika mwanamke juu ya nguo zake, na mara nyingi hutumika pindi anapotoka katika nyumba yake.

 Hivyo itafahamika kwamba jilbaab yatakiwa wakati wa kutoka na wala asitoke ambae hana JILBAAB.




                                                                  SHARTI LA PILI 



                                               ISIWE NI PAMBO NGUO YENYEWE.


 Kwa kauli yake Allah aliyetukuka


“…….na wala wasidhihirishe mapambo” ……. Suratun nuur:31 

Kwa hakika ujumla wake inakusanya nguo zilizodhahiri ikiwa zimepambwa na kushughulisha macho ya wanaume na inatiliwa mkazo na kauli yake Allah mtukufu

وَِل﴾ ٍّ اَال ِّ َّة ي ِّ ُِّهل ـ َ ا ْْل َ ج ُّ ر َ ْبـ َ تـ َ ْن َج َّ ر َ ْبـ َ تـ َالَ َ ن و ُك َّ ِّ وت ُ ي ُ َن ِِّف بـ ْ َر قـ َ ﴿و

“Na mbaki katika majumba yenu na wala msijishauwe mijishauwo ya kujahilia ya zamani” ……. Suratul Ahzaab:33


 Na kauli ya Rasuulallah (Swalallhu ‘alayhi wasallam),

“Watatu katika watu usiwaulizie, (ni katika walioangamia) mtu aliyefarakisha umoja na kumuasi Imam wake na akafa ni ‘asi, na mjakazi au mtumwa aliyetoroka na akafa, na mwanamke aliyeondoka mumewe akiwa amemtimizia matumizi ya dunia basi akajishauwa baada yake. Hawa usiwaulizie” ……. Ameitoa al imamul hakim (1/119)


 Na kujishauwa ni kudhihirisha mwanamke katika mapambo yake na mazuri yake yaliyo wajibu kusitiriwa kwake ambayo huibua matamanio kwa wanaume.


 Na makusudio ya kuamrisha JILBAAB ni kusitiri mapambo ya mwanamke, haitoingia akilini tena kuwa JILBAAB yenyewe ni pambo. Na hili kama unavyoliona halifuniki lipo wazi.


Amesema Adh-dhahabbiy allah amerehemu:.. “na katika vitendo ambavyo mwanamke hulaaniwa kwavyo ni kudhihirisha mapambo, na dhahabu na lulu chini ya niqaab na kujitia manukato ya miski na manukato mengine pindi anapotoka, na kuvaa nguo za rangi za mvuto na makuba mafupi pamoja na kurefusha nguo na kutanua sana mikono ya nguo na kuirefusha huko ni kujishaua ambako Allah anamkuchukia mfanyaji wake katika dunia na akhera na matendo haya yameelezwa mengi juu ya wanamke wengi ambao mtume amewasema ” nimeangalia motoni nikawaona wengi kati ya watu wake ni wanawake: hadithi sahihi


Na umefika mbali uislam katika kutahadhrisha kujishaua kwa wanawake mpaka kufikia daraja ya kuambatanishwa na shirki na zinaa na wizi na mengineyo katika mambo ya haram na hilo pale walipombai (vote) wanawake kuwa hawatofanya hilo. : Amesema Abdullah bin Amru(Allah amridhie) amekuja Umaymah bint Ruqayqah kwa mtume ( وسلم عليه هللا صلى ( akim’bai(kumpa mkono wa utiifu) juu ya uislam.


Akasema na kubali ya kuwa hatomshirikisha Allah aliyetukuka na chochote , na wala kutoiba na wala kuzini, na kutomuuwa mtoto wako wala kutoleta uzushi utakaouzua mbele yako na wala hutoomboleza na wala kutojisheuwa na majishauo ya kijahiliya ya kizamani:


Na tambua ya kuwa inaingia katika hili namna ya vivazi vinavyovaliwa na wanamke juu ya JILBABU zao baada ya kujisitiri kwao, vishungi vidogo vinavyozunguka kichwa chao. vijulikanvyo kama” HAKI YA MUNGU” kwa lengo la kuonyesha shoo Fulani na staili katika hilo na wamche Allah wale wenye kulitenda hilo.


ANGALIZO Na wala halijaingia katika mapambo kuwa nguo ya mwanamke ambayo kajifunga nayo kuwa ni yenye rangi isiyokuwa ni rangi nyeusi au nyeupe kama wananyotuhumu katika hilo baadhi ya wanawake wenye kujihifadhi kwa mambo mawili.


Mwanzo kauli ya Mtume Muhammad (Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam):-

Manukato ya wanawake ni yale yenye kudhihiri rangi yake na kuficha harufu yake; [sahihi]

Nyingine; ni kupita tendo hilo katika wanawake wa kiswahaba kama yalivyoelezwa haya katika vitabu vya hadithi




                                                             SHARTI LA TATU


                                                     IWE NZITO HAIONYESHI


Kwa sababu stara haiwi ila kwayo ama nyepesi{transparent} humzidishia mwanamke fitna na pambo na katika hilo amesema Mtume;

“Kutakuwa mwisho wa umma wangu wanawake wamevaa bado wako uchi juu ya vichwa vyao kama nundu la ngamia walaa nini hao kwani hao wamelaaniwa” 


Akazidisha mwisho wa hadithi

“Hawatoingia peponi na wala hawataipata harufu yake na kwa hakika harufu inapatikanwa katika masafa fulani na Fulani” 


Amesema ibn Abdu Barri amekusudia mtume وسلم عليه هللا صلى wanawake ambao wanavaa nguo nyepesi ambazo zinasifu umbile lake na wala hazisitiri hivyo wamevaa kwa jina wapo uchi kiuhakika.


Na pia zipo athari zenye kuashiria ya kuwa nguo inavyoonesha au kusifu mwili ni jambo amballo halifai na kwamba ile inavyoonesha ni mbaya kuliko inayosifu umbo. Kwa hilo akasema bibi Aisha (Allah amridhie) alipoulizwa kuhusu ushungi akasema”ni ile yenye kusitiri ngozi na nywele”


Ni wajibu kusitiri utupu kwa zile nguo zisizosifu rangi ya ngozi………. Katika nguo au ngozi………… ama stara kwa kile kinachodhihiri ndani yake rangi ya ngozi katika nguo nyepesi HAIFAI kwani stara haipatikani kwa hilo.




                                                                  SHARTI LA NNE 


                              IWE PANA SI YENYE KUBANA IKASIFU KITU KATIKA MWILI 


 Kwa sababu lengo la nguo ni kuondosha fitna na wala halipatikani hilo ila kwa ile pana yenye kuenea ama nyembamba hata ikisitiri rangi ya ngozi, kwani inasifu umbo la mwili wake au baadhi yake na inatengeneza picha katika macho ya wanaume. Na hilo ni katika ufisadi na kuvutia yale yasiyofichikana kutoka kwake hivyo ikawajibika kuwa pana.


Amesema Usamah bin Zayd(Allam amridhie)

“Alinivisha mtume (Swalallahu ‘alayhi wasallam) nguo nzito ya kikab’twi, katika zile alizopewa na Dali-yatul-Kallbiy nikamvisha mke wangu, akasema, Kwa nini hukuvaa nguo za kabtwi. Nikasema, nimemvisha (nimempatia) mke wangu. Akasema muamrishe aweke chini yake Ghalala. {nguo nzito ya ndani}, mimi nachelea kuja kusifu umbo la viungo vyake.”

 Amesema Al-Imam Shawkaniy

“Na hadithi inajulisha ya kwamba wajibu wa mwanamke kusitiri mwili wake kwa nguo inayokuwa haisifu na hii ni sharti kwa mwenye kustiri utupu na imeamrishwa nguo ndani yake kwa sababu Kibtwiyyu ni nguo laini haistiri kwa mtazamo wa muangaliaji bali inasifu umbo”


Na hii hadithi imekuja kwa nguo nzito ambayo bado inasifu umbo la mwanamke, bali mtume (Swalallahu ‘alayhi wasallam) alikhofia kwa nguo hii kusifu umbo la mwanamke, hivyo akaamrisha nguo ya ndani kwani nguo inaweza kusifu mwili hata kama ikawa nzito, ikiwa katika mambo yake kuna ulaini na ule uanamke.


Na wakaleta fitna baadhi ya wasomi waliposema

“Kama nguo itastiri rangi na kusifu umbile la viungo vya mwili hakuna ubaya kama mfano akivaa suruali inayobana”


Na kwa rai hii inajuzu kwa mwanamke leo kuvaa hizi nguo zinazobana ambazo zinashikana na mwili wake na ikamsifu kwa namna yalivyo maumbile yake kiundani, mpaka akadhani aliyembali kuwa yeye yupo uchi, kama haya majinzi yanayobana mwili kama soksi vile, ambayo yanasifu umbo la miundi yake na mapaja yake na vinamzidishia uzuri. Hivyo mwanamke akivaa mfano wa nguo hizi itajuzu kwao wao! Eti kwa kusitiri rangi!!!!!!!... (Sharhu Muhadhab)


Na kwa mnasaba huu ninasema: Wengi katika vijana wa kike wa kiislam wanafika mbali katika kusitiri juu ya miili yao nakusudia kichwa basi, wanasitiri nywele na kichwa, kisha wanakuwa hawajali sehemu nyingine za mwili kinyume na hizo basi wanavaa nguo za kubana na fupi ambazo hazikiuki nusu muundi? au wanasitiri nusu iliyobaki kwa soksi zinazoshikana na nyama (mwili) ambazo zinazidisha uzuri, na kwenda kuswali baadhi yao namna hii, na hii haifai.


Na ni wajibu juu yao kuharakia katika kutimiza stara kama alivyoamrisha Allah (Subhaanahu Wataala) kujigeza na wanawake wa muhajirina wa mwanzo pale ilipoteremka amri ya kuvaa shungi , wakachana mashuka yao na vitambaa vyao , wakajifanyia ushungi , lakini sisi hatuwataki kuchana chochote katika nguo zao! Bali si vinginevyo wazirefushe na kuzitanua mpaka iwe nguo yenye kusitiri yote ambayo Allah amewaamrisha kusitiriwa kwake.


Na kwa hakika tumewaona wengi katika vijana wa kike wanaodanganyika kwa baadhi ya wale wanaojidai kwamba wao ni katika walinganiaji, wakawafanya wao ndo nembo yao kwa kupunguza nguo zao mpaka nusu muundi, pamoja na kuweka kijilemba (HAKI YA MUNGU) pasi na JILBAAB juu ya kishungi kama maelezo ya quran tukufu yaliyotangulia bayana yake. Na wao katika hilo hawajui kwamba wao wanazikusanya nafsi zao katika kundi la wale Allah aliowasema;

 “Na wao wanadhania kwamba wanafanya mazuri”


Kwa wenye ikhlaas miongoni mwao naelekeza nasaha zangu hizi, kwamba wasiathirike kwa kuacha kufuata kitaab na sunnah eti tu kwa kufuata kikundi Fulani au sheikhat (Sheikh wa kike) na hali Allah aliye juu ya arshi yake anasema;

 ْ وا ُ ع ِّ ْب َّ ات َالَ َ و ْ ُكم ِّ رب َّ ن ِّ ُكم م ْ لَي ِّ نِّزَل إ ُ آ أ َ م ِّ ل َ ق َ آء َ ي ِّ ل ْ أَو ِّ ه ِّ ون ُ ن ُد ِّ ْ م وا ُ ع ِّ ْب َّ َت وَن تـ ﴾ َ ُ ََذَّكر ما ت يالً َّ

“Fuateni yale yaliyoteremshwa kwenu kutoka kwa mola wenu na wala msifuate (hao mnaowaitakidi kuwa) walinzi wenu badala yake. Ni machache mnayokumbuka” …. Aaraf:3




                                                                 SHARTI LA TANO 


                                ISIWE IMEFUKIZWA WALA KUNUKISHWA MANUKATO 


Kwa hadithi nyingi ambazo zinazokataza wanawake kujitia manukato pindi wanapotoka katika majumba yao, na sisi tunazichunga baadhi ya hizo mbele yako zilizosihi mategemezi yake:


1-Kutoka kwa Abii Mussa Al-ash-ariiy Allah amridhie: amesema amesema صلى هللا عليه وسلم Mtume

“mwanamke yeyote atakaejitia manukato kisha akawapitia watu ili wapate harufu yake basi huyo ni MZINIFU. [ Ameitoa An-Nasai هللا رحمه]


2-Kutoka kwa Zainab Thaqafiyyah.Hakika mjumbe wa ALLAH وتعالى سبحانه amesema “atakapotoka mmoja wenu kwenda msikitini basi asiyakurubie manukato” Ameitoa Muslim.


3-Kutoka kwa Abi Hurayrah: amesema Mtume وسلم عليه هللا صلى amesema “mwanamke yeyote aliyegusa bakhuri(aliyejifukiza) basi asishuhudie nasi swala ya Inshaa.


4-Kutoka kwa Mussa bin Yassir kutoka kwa Abuu hurayrah

“Hakika ya mwanamke mmoja ilivuma harufu yake, Akasema “Ewe mjakazi wa (mola) tabbari msikiti umemkusudia? Akasema: Ndiyo, Akasema” Na kwa ajili yake amejipaka manukato. Akasema Ndiyo, Akasema Basi rejea na ukakoge kwa hakika mimi nimemsikia mtume وسلم عليه هللا صلىanasema” Hakuna mwanamke anayetoka kwenda msikitini na unavuma(tapakaa) harufu yake Allah akaikubali sala yake mpaka arejee nyumbani kwake na akakoge.” Ameitoa Bukharهللا رحمه

Na njia ya kutegemea dalili kwa hadithi hizi juu ya yale tuliyotaja. Ujumla wa yale yalokuwemo.


Kwani hutumkia manukato na mafuta mazuri kama yanavyotumika katika miili kadhalika hutumika katika nguo. Hasa hasa katika hadithi ya tatu imetajwa na bukhari kwani hiyo kwa nguo hutumika zaidi na huhusika.


Na sababu ya kuzuiliwa iko wazi nayo ni kutikisha na kutibua matamianio na wamelikutanisha nalo wanavyuoni yale yaliyo katika maana yake.Kama kuvaa nguo nzuri na mapambo yanayodhihiri na mapambo ya fakhari na kadhalika mchanganyiko wa wanawake na wanaume.


Amesema Ibni Daqiyqul’ydi هللا رحمه“:na ndani yake kuna uharamu wa kupaka manukato kwa mwenye kutaka kutoka kwenda msikitini kwa kule kuwa ndani yake kuyatibua na kutikisha matamanio ya wanaume”


Basi itakapokuwa hilo ni haram kwa mwenye kutaka kwenda msikitini, Basi vipi itakuwa hukumu kwa mwenye kulikusudia soko, sehemu za dhiki na majiani? Hapana shaka ya kwamba hilo ni haram zaidi na dhambi kubwa sana na akataja Al-Haythamiyyهللا رحمه katika (Zawajir) kwamba kutoka mwanamke nyumbani kwake amejitia uturi, amejipamba ni katika madhambi makubwa hata kama ataruhusiwa na mumewe.

Kasha hizi hadithi ni za jumla zinakusanywa nyakati zote na khusisha kwa kutaja wakati wa Inshaa katika hadithi ya tatu. Kwa kuwa fitna wakati huo ni kali hivyo asijituhumu mtu kwamba kutoka kwake katika wakati usio huu ni JAIZ.

Amesema Ibn Malik هللا رحمه“: na lililowazi ya kwamba umekhusishwa kwa katazo kwa kuwa ni wakati wa giza na ufaragha wa njiaNa uturi unatibua na kuamsha matamanio.Hivyo hatosalimika mwanamke katika wakati huo wa fitna.Kinyume na asubuhi na magharib kwani hizo ni nyakati za wazi.Na imeshatangulia kwamba kujipaka manukato inamzuia mwanamke kuhudhuria msikitini moja kwa moja.


Na litakapobainika hilo, hapana kwa nguo ya kiume na kike tofauti inayopambana baina ya wanaume na wanawake na ziwe nguo za wanawake zenye kuathiri na kuhifadhi………………. hivyo ikiwa nguo mara nyingi huvaliwa na wanaume atakatazwa mwanamke hata kama inastiri, kama nguo Fulani zinazovaliwa kidesturi na mwanaume katika mji Fulani.Na katazo mfano wa hili hutofanyika kwa kutofautiana na desturi. Ama ikiwa tofauti inarudi katika yenyewe.




                                                                 SHARTI LA SITA 


                                           ISIFANANE NA KIVAZI CHA MWANAMME


Kwa yale yaliokuja katika hadithi sahihi kuhusu laana ya mwanmke ambaye anajifananisha na mwanmmme katika mavazi au mengineyo. Na katika tunayoyafumbua ni haya:


1)Kutoka kwa abuu hurairah anasema: ‘’Amemlaani  Mwanmme anaevaa kivazi cha kike” abuu dawuud


2)Kutoka kwa Abdullahi bin Amru : ‘’Nimemsikia Mtume وسلم عليه هللا صلى (anasema;Siyo katika anaejishabihisha na wanaume katika hatowatizama(rehma)siku ya qiyama;Mwenye kuwaasi wazazi wawili,Mke kidumedume mwenye kujifananisha na wanaume na Dayuthi(Mwanaume asiye na wivu kwa mkewe).


3)Kutoka kwa Ibn Abbas Maliykali jina lake ni Abdullah bin Ubayyah amesema:

Aliulizwa bibi Aisha(Allah amridhie) Hivi Mke anavaa viatu (Vya kiume).Akasema``Mtume(وسلم عليه هللا صلى (amekataza Udume katika Wanawake. Na katika dalili hizi kwa hadithi ya wazi juu ya uharamu wa mke wanawake, Na wala wenye kujishabihisha na wanawake katika mimi” Ameitoa Ahmed هللا رحم


4)Kutoka kwa Ibnu Abbas ansema: ‘’Mjumbe (وسلم عليه هللا صلى (anasema; amewalaani makhanithi katika wanaume na madumedume katika wanawake na akasema watoeni katika majumba yenu: Mtume وسلم عليه هللا صلى akamtoa Fulani na Omar akamtoa Fulani”na katika tamshi jingine Mtume wa ALLAHوتعالى سبحانه amewalaani wenye kujishabihisha na wanawake katika wanaume na wanawake wenye kujishabihisha na waaume.


5)Kutoka kwa Abdullah bin Omar عنهما هللا رضيanasema: ‘’Amesema Mtume (وسلم عليه هللا صلى (watatu katika watu hataingia peponi na wala ALLAH kujifananisha na wanaume na kinyume chake. Nazo ni za ujumla zinakusanya nguo na mengineyo, ila hadithi ya kwanza ni hoja ktk mavazi peke yake.

Amesema Adh-dhahabiyy (katika al Kabair):``Pindi atakapo vaa mke nguo za kiume ktk maqalib(nguo)…………..na mikono ua nguo iliyo membamba atakuwa amejigeza na wanaume katika mavazi yao,Zimepita laana za Allah na Mtume wake”

Ikathibiti katika yale yaliotangulia kwamba haifai kwa mke kuwa nguo zake zinafanane na nguo za mwanmme hivyo si halali kwake kuvaa ridaa na shuka na mfano wake.kama wanaofanya baadhi ya mabinti wa kiislam katika zama hizi katika yale mavazi yao yanayujulikana kama JACKET na SURUALI.

Hata kama hili kihali halisi ni stara zaidi kuliko nguo zao zengine,


                                                      Zingatieni Enyi wenye akili.


Na hapa kinadhihiri kidhibiti ktk katazo lake Mtume وسلم عليه هللا صلى la kijishabihisha wanaume kwa wanawake na wanawake kwa wanaume na kwamba ktk hilo siyo kurejea katika upeo wa yaliyochaguliwa na mwanmme na mwanamke na wakayatamani na kujizoesha kwayo hadi kuwa kama desturi


Tofauti katika nguo za kiume na za kike inanarudi ktk yale yanayofaa kwa mume na yanayofaa kwa mke nayo ni katila yenye kunasibiana nay ale walio amrishwa wanaume na yale walioamrishwa wanawake hivyo wanawake wameamrishwa kujistiri na kujitanda pasi na kujisheua na kujidhalilisha kimapambo.


Mwanamme anaejishabihisha na mwanamke huchuma tabia zao kwa kadri ya kujishabihisha kwake mpaka humpelekea akawa KHANITHI na huwa kama mwanamke na zama ilipokuwa nyimbo ni vitangulizi vya hilo na ilikuwa ktk matendo ya mwanamke,wakawa wanawaita wanaume waimbaji MAKHANITHI:


Na mwanamke mwenye kujishabihisha na wanaume anachuma katika tabia zao mpaka anajisheua na kujidhalilisha mpaka impelekee kudhalilisha mwili kama wanavofanya wanaume na akataka awe juu ya wanaume kama vile wanavokuwa juu wanaume kwa wanawake.




                                                                  SHARTI LA SABA 


                                              ISIFANANE NA NGUO ZA MAKAFIRI 


Kwa lile linalokubaliwa katika sheria ya kwamba haifai kwa waislamu wanawake na wanaume,ni kujishabihisha na makafiri sawa katika ibada zao na Iddi zao au nguo zao maalum na hii ni Qaidah (msingi) mkubwa katika sharia ya kiislam,wametokea katika hilo kwa masikitiko wengi katika waislam mpaka wale wenye kujihimiza katika mambo ya dini na ulinganizi kwa kutoelewa dini yao na kufuata matamanio yao au kuathiriwa na desturi au tamaduni zilizopo na kuwaiga makafiri wa Europe,mpaka ikawa ni katika sababu za waislamu kuwa wanyonge na madhaifu na maadui kua juu yao na kutawala.

 َّت َّ َ ح ٍ م ْ َقو ِ ا ب َ م ُ ّيِ َِ غ ُ َّللَ الَ ي ن ا َّ َّ ِ إ ُ ي ْ ِسِهم ف ُ ِِبَن ا َ ْ م وا ُ ّيِ َِ ...... غ

“Hakika ya Allah habadili yaliyo kwa watu mpaka wao wabadili yaliyo katika nafsi zao” (Raad:11) Lau kama wangetambua

“……………..kisha tukakuweka juu ya sheria (njia),basi ifuate wala usifuate matamanio ya wasiojua.”

Na aya nyingi na hadith nyingi zilizokuja zinazogombeza waislam kujifananisha na makhafiri au kuiga nyenendo zao.



                                                               SHARTI LA NANE 


                                                ISIWE NI NGUO YA UMASHUHURI 


Nayo ni nguo hukusudiwa umashuhuri kwa watu, ni sawa ikiwa nzuri inayovaliwa katika ufakhari wa dunia na mapambo yake au ambayo inayovaliwa kujionyesha uchamungu au kujionyesha.


Amesema Ibun Abbas.

”Umashuhuri ni kukidhihirisha kitu na inakusudiwa hapa kuwa nguo yake iwe mashuhuri mbele za watu kwa kutofautiana rangi yake na rangi za nguo za watu wengine,ili watu wamkodolee macho yao na apande………………..kwao wao kwa dharau na maringo.


Kwa hadithi ya Ibnu Omar(Allah amridhie)amesema; (صلى هللا عليه وسلم) Mtume amesema ” Mwenye kuvaa nguo ya umashuhuri katika duniani Allah atamvisha nguo dhalili siku ya Qiyama, Kisha Allah aliyetukuka atamuingiza ndani ya moto”(Abuu Daudi هللا رحمه(


Na kufikia hapa yanamaliza kwetu maelezo juu ya masharti na wajibu yanayofungamana na kivazi au nguo ya mwanamke; na kwa muhtasari:


Iwe yenye kustiri mwili wote ila uso wake na viganja kwa uchambuzi uliotangulia(.niqab ni bora) na isiwe pambo yenyewe, wala yenye kuonyesha, wala nyembamba inayosifu mwili wake,wala imetiwa manukato na wala isiwe inafanana na nguo za mwanaume na nguo za makafiri na wala nguo za umashuhuri.


Hivyo la wajibu kwa muislam kuhakikisha katika kumtengeneza mke wake, na kila atakayekuwa chini ya uongozi wake. Na ALLAH amesema:

“Enyi mlioamini ziokoeni nafsi zenu na za watu wenu na moto ambao kuni zake ni watu na mawe juu yake kuna malaika wakali wenye nguvu, hawamuasi ALLAH anayo waamrisha na wanatenda wanayoamrishwa.''


Namuomba Allaah atuwafikishe kwa kufuata maamrisho yake na kujiepusha na makatazo yake.

Ikiwa nimepatia ni kutoka kwa Allaah na kama nimekosea ni kutokana na nafsi yangu shaitwani.


Faqiri mbele ya ALLAH subhanahu wata’ala. ابو عمير آدم سفي هللا )حفظه هللا تعالى ورعاه(

Abuu Umayri Adam Safiyyyullah.

from fisabilillaah.com https://ift.tt/2Qy0gc4
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...