Translate

Ijumaa, 30 Novemba 2018

17. Shaykh al-Albaaniy anatakiwa kufahamika hivi

Tano amesema:

“Wakati tutapoyakumbuka haya, basi ni wajibu kufanya bidii kusimamisha nchi hii ya Kiislamu. Kama mnavyojua husema siku zote kwamba hayo hayawezi kupatikana kwa fujo, hamasa na kelele, isipokuwa ni kwa kupambana.”

Kwa uhakika wote anamaanisha kwamba ni wajibu kwa waislamu kujifunza mambo ambayo Allaah amewawajibishia. Anaona kwamba inatakiwa kuwarekebisha mtu mmojammoja ambaye ataijengea jamii ambayo itaijenga nchi ya Kiislamu. Fikira hii ni ya Kiislamu na ni ya sawa.

Ni wajibu kwetu kumfahamu Shaykh (Rahimahu Allaah) namna hii, ya kwamba anaonelea kusimamisha nchi itayosimamisha Shari´ah ya Allaah mahali ambapo hakufanywi hivo. Hapana shaka yoyote kwamba hakusudii kusimamisha nchi ndani ya nchi nyingine, kama wanavofanya Hizbiyyuun. Wala hakusudii kusimamisha nchi ndani ya nchi ambayo tayari inahukumu kwa Shari´ah ya Allaah. Huku ni kuharibu na sio kutengeneza.

Aidha ni wajibu kutambua kwamba usulubu wa mtu huyu umedhibitiwa na ´Aqiydah yake na yale aliyothibitisha katika vitabu vyake vingi. Haijuzu kuyafuta yote hayo kwa sababu ya neno au sentesi moja aliyoisema katika mazingira fulani. Hivi ndivo Shaykh (Rahimahu Allaah) anavyotakiwa kufahamika. Hayo yanafahamishwa na maneno yake mwenyewe pale aliposema:

“Pindi kwa masikitiko itapodhihiri kwamba hakuna ambaye anasimamisha adhabu za Kishari´ah, haina maana kwamba mlango wa Kishari´ah hautakiwi kufunguliwa.”

Shaykh ni mwenye kutambulika juu ya kufuata na kupita juu ya Sunnah. Huenda mara fulani akapondoka kwa Ijtihaad aliyoifanya, lakini haya ni katika mambo yasiyohusiana na ´Aqiydah.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2P9Vr3G
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...