Translate

Ijumaa, 30 Novemba 2018

KOSA LA KUPANGA SWAFU BAINA YA NGUZO ZA MISIKITI.



Assallaam  Aleykum  WarahmatulLaaah  Wabarakatuh



                                                                   UTANGULIZI 



Kila shukrani njema anastahiki ALLAH ambaye huwaongoza waja wake katika kuifahamu dini yake na lau kama si yeye basi waja hao wasingelipata muongozo wa kuifahamu dini yake.

الحمد هلل الذي بنعمته تتم الصالحات

Na sala na salamu za ALLAHU ziwe juu ya Bwana Mtume (salallahu Alayhi Wasallam) na jamaa zake walioamini pamoja na sahaba zake.


Hiki ni kitabu kinachobainisha hukumu ya kupanga swafu baina ya nguzo za misikiti ni kuwa ni katika makosa wanayofanya wenye kusali na hii ni kutokana na kuwa mbali watu na kuisoma dini yao katika njia sahihi aliyokuja nayo Mtume wa ALLAAH na kupokelewa njia hiyo na sahaba zake na kuieneza pembe za dunia.


Kwa hiyo kutokana na kosa hili la watu kupanga swafu baina ya nguzo za misikiti kua ni kosa hili kufanywa mara kwa mara kwa sababu ya ujinga wa watu wa kutoelewa usahihi wa jambo hili, tumeonelea kuandika kitabu hiki na tumekipa jina ZAWADI YA MISIKITI KWA AJILI YA KUWAJULISHA WANAOSALI JUU YA KOSA LA KUPANGA SWAFU BAINA YA NGUZO ZA MISIKITI. 


Tunaomba ALLAHU (Subuhaanahu Wataala) akifanye kitabu hichi kiwanufaishe waislamu wote na iwe ni muangaza kwao katika mas-ala haya Aaamin


Abuu Muhammad Hasnuu Amour Kombo Azzinjibariy Attanzaniy. 




DALILI ZILIZOKUJA KUKATAZA KUPANGA SWAFU BAINA YA NGUZO ZILIZOMO MISIKITINI.


Naam,Zimekuja haddithi kukataza kusali (kupanga swafu) baina ya nguzo za msikiti miongoni mwa hadithi hizo ni hizi zifuatazo: -

) ۱ )

عن قرة بن إياس المزني قال: ) كنا ننهى أن نصف بين السواريى على عهد رسول هللا صلى هللا عليه وسلم ونطرد عنها طردا(. رواه ابن ماجة )۱۰۰۲ )والطيالسي )۱۰۷۳ .)والبزار في "مسنده" وابن خزيمة )۱۵٦۷ )وابن حبان )۲۲۱٦ )والطبراني في "المعجم الكبير" )۱۹\۲۱:رقم ۳۹ )والحاكم )۱\۲۱۸ )والبيهقي )۳\۱۰۶ ، )والدوالبي في "الكنى واألسماء" )۲\۱۱۳ )والمزي في "تهذيب الكمال" )۳\ق۱۶۳۱ )وصححه األلباني في "صحيح ابن ماجة " )۸۲۸ ) وقال في "تمام المنة" )۲۹٦(( : )صحيح لغيره((.

Maana ya hadithi: (kutoka kwa Qurratan bin Iyaasi Al- Muzaniyyi Amesema: “Tulikatazwa kupanga swafu baina ya nguzo katika zama za Mtume (salallahu Alayhi Wasallam) na kulifanya kua mbali nalo jambo hilo na kuwekwa mbali nalo (na kuondolewa kila atakae Sali sehemu hiyo.)

 ) ۲ )


عن عبد الحميد بن محمود قال : )) صلينا خلف أمير من األمراء، فاضطرنا الناس، فصلينا بين الساريتين، فلما صلينا، قال أنس بن مالك) كنا نتقي هذا على عهد رسول هللا صلى هللا عليه وسلم((. أخرجه الترميذي )۲۲۹ ) وابو داود ) ۳ ) و النسائي )۸۲۱ )والحاكم ) \ ( وعبد الرزاق ) ۲۶۸ )وابن إبي شيبة ) \ ( وأحمد ) ۳\۱۳۱ )وابن خزيمة ) ( وابن حبان)۲۲۱۵)والبيهقي)۳\۱۰۶ )والمزي في ))تهذيب الكمال(( ) \ق ( وابن القاسم في )) المدونة(( ) \ ( وصححه ابن حجر في "الفتح" ) \ ( وحسنه السيوطي في "جمع الجوامع ) ( قلت : بل هو صحيح ، وصححه األلباني في "صحيح الترميذي" ) ( و "وصحيح النسائي" )


( Maana ya Hadithi: (kutoka kwa Abdul Hamid bin Mahmoud Amesema: “Tulisali nyuma ya Amir (kiongozi). Wakatulazimisha watu tukasali baina ya nguzo, basi tulipomaliza kusali, akasema Anas bin Maalik: “Sisi tulikua tukijiepusha na jambo hili la kusali baina ya nguzo katika zama za Mtume (Salallahu Alayhi Wasallam)”


) ( قال ابن مسعود : )) التصطفوا بين السواري وال تأتموا بقوم يمترون و يلغون((. أخرجه عبد الرزاق ) ( و ) ( وابن أبي شيبة ) \ ( وسعيد بن منصور في )) سننه(( والطبراني في ))الكبير(( ) ( و ابن القاسم في ))المدونة(( ) ( والبيهقي ) \ (. وقال الهيثمي في ))
المجمع(( ) \ (: )) إسناده حسن


((. Amesema Ibnu Mas-ud: (Radhiyallahu Anhu): ()Msipange swafu baina ya nguzo na wala na wala musiwafuate watu waliyokua na mashaka au kujadiliana katika mambo ya kibatili na wakawa wanafanya laghau (mambo ya kipuuzi (. )) )


(. عن قرة بن إياس قال: رآني عمر وأنا أصلي بين اسطوانتين، فأخذ بقفائي ، فأدناني إلى سترة فقال: ))صل إليها((.


Kutoka kwa Qurratan bin Iyaasi amesema: ((Ameniona Omar bin khatwab nikisali baina ya nguzo basi akanishika kichogo changu na kunisogeza karibu na stara na akasema kuniambia: “swali ilhali umeielekea stara”)). Nimesema hapa (Abuu Muhammad Hasnuu): “Kusali hali ya kuelekea stara ni jambo la wajibu na ndo maana Omar bin Khatwab alipomuona Qurratan amesali hali ya kua hajaielekea stara, akamueka sehemu ambayo atakuwa ameielekea stara na jambo la kusali mtu baina ya nguzo za msikiti linamfanya mtu huyo asali hali ya kua asielekee stara isipokua atakapoweka mbele yake kitu kwa hiyo ewe mwenye kusali lifahamu hili ili ufanye ibada kwa elimu na uwe mbali na kufanya makosa kwenye Ibada.” )


(. عن إبراهيم التيمي أنه قال: ))ال تصلوا بين األساطين((. رواه ابن أبي شيبة) \ ( بسند صحيح. وله طريق أخرى عنده أيضا. وفي سندها شريك - وهو النخعي- سيء الحفظ : )... عن إبراهيم أنه كره الصالة بين األساطين وقال: ))أتموا الصفوف((. قال أهل الحديث ))وما قبله يشهد له، ويدل على أن شريكا حفظه


((. Kutoka kwa Ibrahim Attaymiyy hakika yeye Amesema: “Msisali baina ya nguzo za msikiti”. Amesimulia hadithi hii Ibnu Abiy shaybah (3/380) kwa sanad  sahihi na hadithi hii ina njia nyengine kwake yeye vile vile, na katika sanad yake kuna msimulizi anaeitwa Shariku nae ni Annakhaiyyi ni Sayyiul- Hifdhi (hifahi yake mbaya sio nzuri) : “kutoka kwa Ibrahimu hakika yeye amechukia kusali baina ya nguzo za msikitini na akasema: ((Timizeni swafu)).”Wamesema watu wa hadithi: “Na ile hadithi iliyotangulia inatoa ushahidi na kujulisha kuwa Shariku amehifadhi na haikua mbaya hifadhi yake katika hadithi hii.” Kauli yake Ibrahimu:((timizeni swafu)): Hii inaonesha kwa watu wakipanga swafu na baina yao ikawa ipo nguzo inaonesha na kujulisha kua swafu hiyo haijatimia bali kuna nafasi nayo ni hiyo nafasi ya nguzo, na kutimiza kwa swafu ni kunyooka kwake na isiwe imekatika au kuwepo kizuizi kama hizo nguzo na mfano wake (vitu vyengine).

*Neno”sanad” maana yake ni mategemezi na ni wasimulizi wa hadithi ( Ruwatul- Hadithi)



KUPANGILIA MILANGO KWA WANAZUONI WA HADITHI JUU YA MAS-ALA HAYA WAKIASHIRIA HUKUMU YAKE YA KUA HAIFAI KUPANGA SWAFU BAINA YA NGUZO. 


Katika kipengele hichi nitataja baadhi ya Abuwabu (milango) kutoka katika baadhi ya vitabu vya hadithi ikiashiria hukumu ya mas-ala hayo kwa tarjama (tafsiri) zilizokusudiwa na wanazuoni wa vitabu hivyo.


Na hapa naanza kunukuu kwa kusema:

 أ(- بوب اإلمام البخاري في ))صحيحه(( على حديث ابن عمر بقوله: )) باب الصالة بين السواري في غير جماعة((.


a) Ameweka mlango Imamu Bukhari katika kitabu chake ) Sahihil- Bukhari) juu ya kutolea maelezo hadithi ya Ibnu Omar kwa kauli yake: “mlango wa kusali baina ya nguzo sala isiyokua ya jamaa.” 

قال الحافظ ابن حجر في )) الفتح(( ) \ ( شارحا: ))إنما قيدها بغير الجماعة ألن ذلك يقطع الصفوف، وتسوية الصفوف في الجماعة مطلوب((، وقال الرافعي في )) شرح المسند((: "احتج البخاري بهذا الحديث على أنه ال بأس با لصالة بين الساريتين إذا لم يكن في الجماعة".

Amesema Hafidh Ibnu Hajari : katika (Alfat-hu 1/578) Hali ya kusherehesha kauli ya Imam Bukhari kwa kusema : ((Hakika Imamu Bukhari amefunga kifungo cha kuwa mtu ataweza kusali baina ya nguzo sala isiyokua ya jamaa, kwa sababu endapo sala itasaliwa jamaa na watu wakapanga swafu baina ya nguzo jambo hilo linakata swafu, na kuziweka swafu sawa na kua zimenyooka na kuungana mwanzo wake hadi mwisho wake ni jambo litakiwalo katika sala ya jamaa.))

 وقال نحو ما قال ابن حجر اإلمام العيني في )عمدة القاري


(. Na amesema mfano wa maneno aliyosema Ibnu Hajari, Imamu Iyniyy katika kitabu “Umdatul  Qaariy” (4/284). ) 

ب( – وبوب الترميذي في ))سننه(( على حديث أنس. بقوله: ))باب ما جاء في كراهية الصف بين السواري

b) Na ameweka mlango Imamu Tirmidhiyyu katika sunaniy yake juu ya kuitolea maelezo hadithi ya Anasi kwa kauli yake: “Mlango wa yale yaliyokuja kuhusiana na chukizo la kupanga swafu baina ya nguzo”.


 )ج( – وبمثله بوب البيهقي على الحديثين في )) سننه(( . وقال بعده : ) وهذا – وهللا أعلم – ألن االسطوانة تحول بينهم وبين وصل الصف


c) Na kwa mfano wa maneno hayo ya Imamu Tirmidhiyyu ndio akayawekea mlango Imamu Bayhaqiyyu katika sananiy yake juu ya kuzitolea maelezo hadithi mbili na baadaye akasema: “Na haya na Allaah ndiye Mjuzi. Kwa hakika nguzo za misikitini huzuia baina yao (wanaosali) na baina ya kuiunga swafu”.


د( – وبوب ابن خزيمة في ))صحيحه(( على حديث قرة بقوله : )) باب طرد المصطفين بين السواري عنها


d) Na ameweka mlango Ibnu Khuzaymah katika sahihi yake juu ya kuitolea maelezo hadithi ya Qurratan kwa kauli yake : "Mlango wa kuwekwa mbali na kufukuzwa kwa wale wanaopanga swafu baina ya nguzo"


 ) ( – وبوب اإلمام ابن حبان في ))صحيحه(( على حديث قرة بقوله : ))ذكر الزجر عن الصالة بين السواري جماعة((. وبوب على حديث أنس بقوله)) ذكر خبر ثان يصرح بهذا الزجر المطلق))

e) Na ameweka mlango Imam Hibbaani katika sahihi yake juu ya kuitolea maelezo hadithi ya Qurratan kwa kauli yake: (Kutaja gombezo (katazo) la kuswali baina ya nguzo sala ya jamaa)

Na Akaweka mlango juu ya kuitolea maelezo hadithi ya Anasi kwa kauli yake: (kutaja khabari ya pili (hadithi ya pili) inayoweka wazi gombezo (katazo) moja kwa moja.

((و( – وبوب الشيخ الساعاتي في )) منحة المعبود(( ) \ ( بقوله : ) )باب كراهة الصف بين السواري))


f) Na Ameweka mlango shekhe Saatiy katika kitabu (Minhatul- Maabudu) (1/137) kwa kauli yake: (Mlango unaozungumzia chukizo la kupanga swafu baina ya nguzo)


)ز( – وبوب بعض األئمة على الحديث تبويبا مطلقا بقوله: )) باب الصف بين السواري (( أو )باب الصالة بين السواري ( كا إلمام النسائي وابن ماجه وغيرهما.فأطلقوا القول دون استنباط الحكم بالتبويب، مكتفين بظاهر النص وداللة منطوقه و مفهومه.

g) Na wameweka mlango baadhi ya Maimamu wa hadithi pasi na kufungamanisha na hukumu yoyote ile, kwa kauli zao : (Mlango wa kupanga swafu baina ya nguzo) au (Mlango wa kusali baina ya nguzo) waliyoweka milango hiyo kwa namna hiyo ni kama vile Imamu Nasaaiyyu na Ibnu Majah na wengineo. Na wao wametaja kauli pasi na kuifanyia Istimbatwi (kutohowa hukumu) ya hukumu katika milango hiyo hali ya kutosheka na dhahiri (uwazi) ya hadithi na dalili ule upande wa kutamkwa kwake na kufahamika kwake.





KAULI ZA MAULAMAA JUU YA KUKATAZA KWAO KUPANGWA SWAFU BAINA YA NGUZO ZA MSIKITINI.



Maulamaa (Wanazuoni au Wanachuoni) wameelezea kua haifai kupanga swafu baina ya nguzo za msikiti ila kwa dharura miongoni mwa Maulamaa hao ni hawa wafuatao pamoja na kauili zao: -


قال ابن قدامة في ))المغني(( ) \ ( : ))اليكره لإلمام أن يقف بين السواري، ويكره للمأمومين ألنها تقطع صفوفهم، وكره ابن مسعود (1)والنخعي


1. Amesema Ibnu Qudaamah katika kitabu ((Al- Mughniy, 2/220)): “Hapachukizwi kwa Imamu kusimama baina ya nguzo na panachukizwa kwa Maamuma kwa sababu jambo hilo la kupanga swafu baina ya nguzo linakata swafu zao na amelichukia hilo Ibnu Mas-udi na Annakhaiyyu.”

) ( – وقال الشوكاني معلقا على حديثي النهي عن أنس و قرة في كتابه ))نيل األوطار(( ) \ ) ))والحديثان المذكوران في الباب يدالن على كراهة الصالة بين السواري، وظاهرهما أن ذلك محرم.
(2)


2. Na amesema Shaukani : Hali ya kutolea maelezo hadithi mbili zilizoelezea katazo la kusali baina ya nguzo hadithi hizo kutoka kwa Anasi na Qurratan (Radhiyallahu Anhuma) katika kitabu chake ((Nailil- Autwaari,2/236)): Na hadithi zilizotajwa katika mlango zinajulisha juu ya chukizo la kusali baina ya nguzo na uwazi wa hadithi hizo zinaonyesha kua ni haramu (yaani ni haramu kusali baina ya nguzo).


ف ال ابن مفلع كما في)) الفروع(( ) \ (: ))ويكره للمأموم الوقوف بين السواري، قال أحمد: ألنها تقطع الصف .
(3)


3. Amesema Ibnu Muflihu katika kitabu : ((Al- Furui, 2/39)): “Na panachukizwa kwa Maamuma kusimama baina ya nguzo, amesema Imamu Ahmad: Hakika jambo hilo linakata swafu”.


) ( – قال المحب الطبري كما في )) الفتح(( ) \ (: ))كره قوم الصف بين السواري للنهي الوارد في ذلك، ومحل الكراهة عند عدم الصف((.


4. Amesema Al-Muhib Attwabariy : kama yalivyokuja katika kitabu (Al-fat-hu, 1/477) “Wamechukia watu kupanga swafu baina ya nguzo kwa ajili ya katazo lililokuja katika jambo hili na pahala pa kupatikana chukizo hilo ni pale panapokosekana dhiki katika msikiti.”


وقال الترميذي في ))سننه(( ) \ ( : ))وقد كره قوم من أهل العلم أن يصف بين السواري وبه يقول أحمد وإسحاق((.


5. Na amesema Imamu Tirmidhiyyu katika sunaniy yake (1/444) : “Na hakika wamechukia watu katika watu wa elimu kupanga swafu baina ya nguzo na kauli hiyo ya kuchukia ndio anasema Imamu Ahmad na Is-haqa”


) ( وقال السندي في )) حاشيته(( على ) سنن النسائي( ) \ ( شارحا قول أنس: " كنا نتقي هذا....." بقوله : )) أي القيام بين السواري لقطع السواري الصف((.


6. Na amesema Sindiyyu katika maelezo yake juu ya kitabu (sunaniyy Nasaai 2/94) hali ya kusherehesha kauli ya Anasi inayosema: ‘Tulikua sisi tukijiepusha na jambo hili” kwa kauli yake: (Yaani kusimama baina ya nguzo kwa kule ukataji wa nguzo kukata swafu.”


– وقال األلباني في ))الصحيحة(( ) الحديث رقم ( : "وهذا الحديث نص صريح في ترك الصف بين السواري وأن الواجب أن يتقدم أو يتأخر إال عند اإلضطرار كما وقع لهم".


7. Na amesema Albaniy katika kitabu chake (ASSWAHIHAT, NAMBA YA HADITHI 335): “Na hii hadithi ni maelezo yaliyowazi katika kuelezea kuacha kupanga swafu baina ya nguzo na lililowajibu ni kutanguliza swafu ikawa mbele na nguzo ikawa nyuma au kuchelewa swafu ikawa nyuma na nguzo ikawa mbele, isipokuwa pakilazimika kupangwa swafu baina ya nguzo kwa dharura kama lilivyotokea hilo. Kwao wao (hao Maswabaha na Matabiina)”


قال ابن باز لما سئل عن الصف بين السواري فقال رحمه هللا تعال:))خالف السنة((.


8. Amesema Ibnu Baazi : (Rahimahullahu) zama alipoulizwa kuhusu kupanga swafu baina ya nguzo akajibu: “Ni kinyume na sunna jambo hilo (la kupanga swafu baina ya nguzo”).


وقال الشيخ مقبل لما سئل : ما حكم الصالة بين السواري و ما حكم من يقول بجوازها للضرورة؟ فأجاب رحمه هللا تعالى: " هي مكروهة في صالة الجماعة، يقول أنس : إنهم كانوا يكرهون ذلك، لكن إذا ازدحم المسجد فال بأس إن شاء هللا. وأما الرجل يصلي منفردا فال بأس أن يصلي بين السواري، وقد كان الصحابة يبتدرون السواري ليصلوا إليها سواء أصلى إليها أو بين السواري للمنفرد وال ما نع من هذا"


9. Na amesema Shekhe Maqbil zama alipoulizwa: “Ni ipi hukumu ya kusali baina ya nguzo na ipi hukumu ya yule mwenye kusema kua inajuzu kwa dharura? Akajibu kwa kauli yake hii: “Jambo hilo (la kusali baina ya nguzo) linachukizwa katika sala ya  jamaa, Anasema Anasi (Mmoja kati ya Maswabaha wa Mtume) Swallallahu Alayhi Wasallam( ) :” Hakika walikuwa (Maswahaba wa Mtume). Wanachukia jambo hilo, lakini msikiti utakapo kua umejaa na msongamano umekua mkubwa hakuna ubaya wa kusali baina ya nguzo Inshaallahu. Na Amma mtu atakapokuwa anasali pekee yake basi hakuna ubaya wa kusali baina ya nguzo na hakika walikua masahaba wakikimbilia nguzo na kusali hali ya kuzielekea nguzo (kuzifanya stara zao) sawa sawa ikiwa amesali ameielekea nguzo au amesali baina ya nguzo kwa mwenye kusali peke yake na wala hakuna kizuizi katika hili.”


قالت اللجنة الدائمة في))فتاوى اللجنة الدائمة((. )) \ (( : ) يكره الوقوف بين السواري إذا قطعن الصفوف إال في حاالة ضيق المسجد و كثرة المصلين(.


10. Imesema LUJNATI DAAIMAH: “Panachukizwa kusimama baina ya nguzo zitakapo kuwa swafu zinakatwa kwa kufanya hivyo, isipokua katika hali ya kuwa msikiti una nafasi ndogo na wenye kusali ni wengi (hapo itafaa kusali baina ya nguzo kwa dharura hiyo.) ”

*TANBIIHI: Fatawa ya Shekhe Ibnu Baazi na Shekhe Muqbili, marejeo yake ni sauti zilizokuwemo kwenye kaseti zilzizorikodiwa sauti hizo.





                WAKATI UNAORUHUSIWA NA SHERIA KUSALI BAINA YA NGUZO.



Kama ilivyokwisha tangulia katika kauli za Wanachuoni kuhusu kupanga swafu baina ya nguzo kua ni jambo lisilofaa isipokua kwa dharura walizozitaja nazo ni hizi zifuatazo ambazo zikitokea dharura hizo basi wakati huo pata ruhusika kusali baina ya nguzo nazo ni kama zifuatavyo: -


a) Dharura ya kwanza : Ni pale itakapo kuwa msikiti umezidiwa na idadi ya wale wenye kusali kwa maana nyengine msikiti umekua ni mdogo na wenye kusali ni wengi hapo itafaa kusali baina ya nguzo na dharura hii mara nyingi hujitokeza siku ya Ijumaa watu wanaposali sala ya ijumaa au panapotokea msikitini, kuwepo semina miongoni mwa semina za kielimu na mikusanyiko mengineyo ambayo hupelekea kua watu ni wengi na msikiti kuwa ni mdogo kwa dharura kama hii wakati huo kusali baina ya nguzo kutakua hakuna ubaya na haya tumekwisha yaona katika kauli za Wanachuoni hapo nyuma kabla ya kuelezea kipengele hichi na hapa naongezea baadhi ya kauli za wengine nazo ni hizi zifuatazo.


1.قال الشيخ ابن عثيمين : " الصف بين السواري جائز إذا ضاق المسجد، حكاه بعض العلماء

 . * إجماعا. وأما عند السعة ففيه خالف.  والصحيح: أنه منهي عنه ألنه يئدي إلى انقطاع الصف

في "مجموع الفتاوى والمقاالت"*

1) Amesema Shekhe Ibnu Uthaymin : “Kupanga swafu baina ya nguzo inafaa utakapokua msikiti una dhiki ya sehemu au dhiki ya nafasi wameyasimulia hayo baadhi ya Wanachuoni hali ya kua ni Ijmaa (makubaliano juu ya mas-ala hayo). Amma wakati msikiti utakapo kuwa na nafasi ya kutosha basi kuhusu hili ndani yake kuna ikhtilafu, na kauli iliyosahihi ni kuwa ni jambo (yaani kuhusu kupanga swafu baina ya nguzo) lililokatazwa kwa sababu hupelekea kukatika kwa swafu.”


– وقال ابن حبيب: " ليس النهي عن تقطيع الصفوف إذا ضاق المسجد، وإنما نهي عنه إذا كان المسجد واسعا". وانظر ))عمدة القاري


 2) Na Amesema Ibnu Habibi : (Hakika katazo katika kuzikata swafu itakapo kuwa msikiti umedhikika kinafasi (yaani itafaa kuunga swafu ikiwa msikiti umezidiwa na watu kwa hiyo itafaa kupanga swafu baina ya nguzo) na hakika lililokatazwa ni kupanga swafu baina ya nguzo itakapokua msikiti una nafasi ya kutosha.




b) Dharura ya pili : au hali ya pili ambayo kuruhusika kusaliwa baina ya nguzo ni pale mtu atakapokuwa amesali pekee yake bila ya kupanga swafu na wenzake kama vile Imamu au mwenye kusali sala yake peke yake, huyu ameruhusika kusali baina ya nguzo na wakati huo katazo halitamkamata na pia hali hii tumekwisha kuona kauli za baadhi ya Wanachuoni juu ya hali hii kabla ya kuingia kipengele hichi hapo nyuma kidogo ila na hapa napenda kuengezea kauli za baadhi ya wengine nazo ni hizi zifuatazo: -


– قال البهوتي كما في "كشف القناع" ) \ ( : ))وال يكره اإلمام أن يقف بين السواري ألنه ليس ثم صف يقطع


 1. Amesema Buhuutiy kama yalivyokuja maelezo yake katika kitabu (kashfulQinaai1/494) :“Na wala hapachukizwi kwa Imamu kusimama baina ya nguzo kwa sababu hakuna swafu inayokatwa”


– وفال بعضهم : " وتجوز صالة اإلمام و المنفرد بين السواري، ودليل ذلك حديث ابن عمر "أنه سأل بالال أين صلى النبي صلى هللا عليه وسلم في الكعبة فقال: بين العمودين المقدمين". ))متفق عليه


2. Na wamesema baadhi yao katika wanachuoni : “Na inafaa sala ya Imamu na mwenye kusali peke yake baina ya nguzo, na dalili ya hayo ni hadithi ya Ibnu Omar: “Hakika yeye alimuuliza Bilali wapi alisali Mtume (Salallahu Alayhi Wasallam) alipoingia ndani ya Al-qaaba, akasema Bilali: alisali baina ya nguzo mbili za mbele”.


وأكد ذلك اإلمام الشوكاني بقوله في))نيل األوطار(( ) \ ( : "وقد ثبت أن النبي صلى هللا عليه وسلم صلى في الكعبة بين ساريتين".


 Na ameyatilia nguvu hayo yaliyopita hapo juu Imamu Shaukaniy kwa kauli yake iliyomo katika kitabu chake (Nailil-Autwaariy,3/236) : “Na hakika imedhibiti hakika Mtume (Salallahu Alayhi Wasallam) Amesali ndani ya Al-qaba baina ya nguzo”.





HOJA ZA WALE WANAOSEMA KUA INAFAA KUSALI AU KUPANGA SWAFU BAINA YA NGUZO BILA YA DHARURA YOYOTE PAMOJA NA JAWABU ZA UFAFANUZI JUU YA HOJA HIZO. 



Wapo baadhi ya watu wanasema kua inafaa kupanga swafu baina ya nguzo pasi na dharura yoyote ile na hujengea hoja juu ya madai yao hayo na miongoni mwa hoja wanazozijenga ni hizi zifuatazo:


1. Hoja ya kwanza husema : “ Kuwa sehemu zote zilizomo ndani ya msikiti zinafaa kusali na hazina tatizo lolote”. Jawabu juu ya hoja hii ni kweli kabisa kuwa sehemu zote zilizomo ndani ya msikiti zinafaa kusali isipokua sehemu za chooni lakini kusali ni kitu chengine na kupanga swafu baina ya nguzo ni kitu chengine.

>>Tunapozungumzia sehemu ya msikiti kufaa kusali hakuna atakaepinga akasema haifai ila itategemea ni namna gani ya kusali sehemu hiyo, ikiwa baina ya nguzo na sala ikawa ya jamaa itakua haifai ila kwa dharura, na ikiwa ni mtu pekee yake anasali baina ya nguzo itafaa itakapokuwa mbele yake ameweka stara lakini itakapokuwa hajaweka stara mbele yake na wala hakuna stara yoyote  iliyomruhusu kisheria hapo itakua pia haifai kusali katika hali hii. Kwa hiyo maneno yao haya wanayosema : “ kuwa sehemu zote zilizomo ndani ya msikiti zinafaa kusali na hazina tatizo lolote.” Ndugu zangu haya maneno Si hoja na wala hayana msingi wa elimu na ni maneno ya kupigwa na ukuta na watu waache maneno hayo na washikamane na yale yaliyosahihi.



2. Hoja ya pili ; husema : “Kwani kuna ubaya gani wa kupanga swafu baina ya nguzo.?” Maneno yao hayo huyasema kutetea madai yao ya kufaa kupanga swafu baina ya nguzo na huku wakisema hakuna ubaya wowote juu ya kupanga swafu baina ya nguzo.

>>Sisi tunawajibu kua ubaya upo tena mkubwa juu ya jambo la kupanga swafu baina ya nguzo, nao ni kua mnapopanga swafu baina ya nguzo bila ya dharura yoyote ile huwa mnaikata swafu na mtu mwenye kuikata swafu kwa makusudi na yeye atakatwa na ALLAAH na akikatwa na ALLAAH atakuwa mtu huyo katika waliokula khasara DUNIANI na AKHERA na dalili ya hayo ni maneno ya Mtume wetu (Salallahu Alayhi Wasallam) pale aliposema:

))ومن قطع صفا قطعه هللا((. رواه أبو دواد ) ( ، والنسائي ) ( ، والمنذري في ))الترغيب والترهيب(( ) ( والسيوطي في )) الجامع الصغير(( ) ( وصححه النووي في ))المجموع(( ) \ ( وأحمد شاكر في ))مسند أحمد(( ) \ ( واأللباني في ))صحيح أبي داود) ( و ))السلسلة الصحيحة))


()Na yoyote mwenye kukata swafu, Allah atamkata mtu huyo((. Kwa mujibu wa maneno haya ya Mtume (Salallahu Alayhi Wasallam) yanayoonesha wazi kuwa ubaya upo tena mkubwa, kwa hiyo ni vyema watu kurudi katika mafunzo sahihi na wakaacha mazoea waliyozoeshwa kwani dini yetu ina mafunzo yake na mazoea hayana nafasi katika dini, na kauli kama hizo wanazosema watu : “Kwani kuna ubaya gani?.” Ni kauli zinazoonesha kua watu wanafuata mazoea na siyo dini kwa hiyo zinduka ewe Muislamu.



3. Hoja ya tatu ambayo wanaitegemea ni kauli ya Omar bin Khatwab (Radhiyallahu Anhu) pale aliposema:

))المصلون أحق با لسواري من المتحدثين إليها((. رواه البخاري في )) صحيحه(( معلقا ووصله ابن أبي شيبة والحميدي من طريق همدان عن عمربه.

"Wenye kusali wana haki Zaidi ya nguzo kuliko wanaozungumza".

Hii kauli ya Omar bin Khatwab ni sahihi na ameiweka Imamu Bukhariy katika sahihi yake na hii kauli ya Omar bin Khatwab panakusudiwa ni kusali kuzielekea nguzo na siyo kusali baina ya nguzo na ndo maana Imamu Bukhariy kabla ya kuiweka kauli hii juu yake ameweka mlango unaosema: ( األسطوانة إلى الصالة باب (maana yake ni: (Mlango wa sala kuielekea nguzo) kisha baada ya kuuweka mlango huo Imam Bukhariy, hadithi ya mwanzo aliyoiweka katika mlango huo ni hii kauli ya Omar bin Khatwab, kwa hiyo siyo dalili wala siyo hoja ya kumjuzishia mtu yoyote katika kupanga swafu baina ya nguzo na kwa ajili hii amesema Ibnu Hajar katika kitabu chake (AL- FAT-HU,3/220, 1/577):


)) وأراد عمر بذالك أن تكون صالته إلى سترة((

“Na amekusudia Omar kwa kauli yake hiyo ni kuwa sala yake mtu anayosali hali ya kuielekea stara”.

Kwa hiyo madai ya wale wanaotegemea kauli hii ya Omar bin khatwab yatakua yamebatilika na yatakua yamekosa mashiko madai hayo.



4. Hoja yao ya nne ambayo wanaitegemea ni kauli ya Ibnu Siriyna inayosema:

))ال أعلم با لصالة بين السواري بأسا((. رواه ابن أبي شية ) \ ( بسند صحيح، وله طريق أخرى في ))مصنف عبد الرزق

“Sijui kuhusu kusali (sala) baina ya nguzo kua kuna ubaya wowote ule”


Hii kauli si hoja ya kuruhusika kwa watu kupanga swafu baina ya nguzo bali hii kauli ipo katika upande wa kuelezea kusali baina ya nguzo na haya tayari tumekwisha kuyaelezea kua inafaa kusali baina ya nguzo kwa mtu pekee yake au kwa Imam hali ya kua mbele yake kuna stara lakini siyo kupanga swafu baina ya nguzo.


5. Hoja yao ya tano ni riwaya ya Hassan inayosema :


 ))عن الحسن أنه كان ال يرى بأسا با لصف بين السواري(( رواه ابن ابي شيبه ) \ ( من طريق ابن علية عن يونس به ، وضعف أهل الحديث هذا األثر لحال ابن علية وهو إبرهيم ابن علية.


“Kutoka kwa Hassan, hakika yeye alikua haoni ubaya kupanga swafu baina ya nguzo”. Hii athari au hii kauli ni dhaifu na wameidhoofisha Ahlul- hadithi KWA HALI YA Ibnu Ulayya ya kutokubaliwa hadithi zake kutoka kwa Hassani: Kwa hiyo hii siyo hoja kwani ni kauli dhaifu na zipo kauli nyengine ambazo wanategemea wale wanaoona kua inafaa kupanga swafu baina ya nguzo lakini kauli hizo ni dhaifu hazisimami kua ni hoja kutokana na udhaifu wake. Kwa hiyo sunna katika kupanga swafu ni kuhakikisha swafu inanyooka mwanzo wake hadi mwisho wake na kuepukwa nguzo kwa maana watu wasipange swafu sehemu zilizokuwepo nguzo ispokua kwa dharura tu.

اتبعوا وال تبتدعوا فقد كفيتم 

Fuateni (yaliyofundishwa na uislamu kwa misingi sahihi) na walaa msizue( kwa kufanya bidaa na yale yaliyozoeleka kwa wazee bila ya mashiko yoyote yale).

Basi hakika mumetoshelezeshwa kwa mafunzo sahihi kutoka kwa Mtume (Salallahu Alayhi Wasallam).



                                                                      HITIMISHO 



Mwisho wa kitabu changu hichi napenda kuhitimisha kwa maneno haya yafuatayo:


إياكم والصف بين السواري ألنه حرام ال يجوز للمأمومين أن يصفوا بين السواري من غير ضرورة للجماعة، با ألدلة واردة وأ قوال أهل العلم في هذه المسألة، ونسأل هللا العظيم أن يوفقنا التمسك بدينه على الطريقة الصحيحة التي علمها نبيها صلى هللا عليه وعلى آله وصحبه وسلم.


“Tahadharini (enyi waislamu) na kupanga swafu baina ya nguzo kwa sababu jambo hilo ni haramu na halifai kwa Maamuma kupanga swafu baina ya nguzo pasi na dharura ya kuwa jamaa ni kubwa na msikiti ni mdogo kwa dalili zilizokuja na kauli za Wanachuoni katika mas-ala haya. Na tunamuomba Allahu Mtukufu atuwafikishe kushikamana na dini yake juu ya ile njia iliyo sahihi ambayo ameifundisha Mtume wake “Sallallahu Alayhi Wasallam” mpaka siku ya malipo “Aaaamin”. 



Mafunzo sahihi ya uislamu juu ya jambo zima la kupanga swafu baina ya nguzo ni jambo lililokua halifai kwani jambo hilo linapelekea kukata swafu na Mtume (Salallahu Alayhi Wasallamu) ametoa makemeo makali kwa yule anaekata swafu ni pale aliposema:

 ومنقطع صفا قطعه اهلل"


" “Na yeyote atakaeikata swafu basi Allahu na yeye mtu huyo atamkata” kwa hiyo tahadhari na kuikata swafu ima kwa kutoitimiza swafu hiyo au watu kupanga swafu baina ya nguzo hiyo au watu kupanga swafu baina ya nguzo ikawa swafu katikati kuna nguzo pahala pakuingia mtu ikakuwepo nguzo, hii ni kuikata swafu na ni jambo baya sana.


Wengi katika wanaosali hawajui kua kupanga swafu baina ya nguzo ni jambo lisilofaa na hii ni kwa sababu ya kutokuisoma dini yao, na endapo atatokea mtu atawafahamisha basi hua ni wakali sana na kutokubali mafahamisho ya mtu huyo kwani wao wameshazoea kupanga swafu baina ya nguzo,!!


Na hivi ndivyo zilivyo hali za wengi katika waislam wa zama hizi wanafanya ibada kwa mazoea na siyo kwa elimu, jambo ambalo ni msiba mkubwa katika ummah wa kiislamu. Kwa hiyo ni vyema waislamu wa zama hizi tukabadilika na kua katika pahala pa kufanya ibada kwa elimu na siyo kufanya ibada kwa mazoea na kwa jambo hili la kupanga swafu baina ya nguzo huenda kitabu hichi kikatoa nuru ya elimu kuhusu mas-ala haya na ikawa sababu ya kua sisi ni wenye kupanga swafu vizuri na kuziunganisha swafu hizo na kujiepusha na kupanga swafu baina ya nguzo ili tukaingia na kuyapata yale aliyoyasema mtume ( Mtume Swalallahu Alayhi Wasallam) kuhusu mwenye kuunganisha swafu, nayo ni pale Aliposema:

 "ومنوصل صفا وصله اهلل"

"Na yeyote atakaeunganisha swafu basi Allahu na yeye mtu huyo atamuunganisha”. Tunamuomba Allahu Atupe tawfiiq ya kujiepusha na kupanga swafu baina ya nguzo ili iwe sababu ya yeye Allah kutuunganisha na kutupa yaliyo mazuri Aaamin

KIMEANDIKWA NA KUTAYARISHWA NA:-

 ABUU MUHAMMAD HASNUU AMOUR KOMBO AZZINJIBARIY ATTANZANIY 

+ 255 776-819 880/ + 255 742-602 641/+ 255 779 819 880.




*Hakijabadilishwa Kitu Chochote Kuwa Muadilifu Usibadili Chochote*

from fisabilillaah.com https://ift.tt/2Q6fuFq
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...