Translate

Jumatano, 28 Novemba 2018

Sifa za Mke Mwema - Sehemu ya 3

                                                               ص فات ال زوج ة ال صال حة 

                                                                Sifa za Mke Mwema

                         Mwandishi : Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad.

                                                  Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush.



Tunaendeleaaa.................



                                             Mke mwema anatakiwa kumheshimu mume wake 



Katika sifa za mke mwema ni kwamba anamuheshimu mume wake na anajua nafasi yake na haki zake. Kumekuja Hadiyth nyingi kuhusu hili. Moja wapo ni yale aliyopokea at-Twabaraaniy katika “al-Muj´am al-Kabiyr” kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


  “Simwamrishi yeyoye kumsujudia yeyote.Lau ningelimwamrisha mtu kumsujudia yeyote, basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake.” 11/356. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (3490).


at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Muj´am al-Kabiyr” kupitia Zayd bin Arqam kwamba Mu´aadh amesema:

“Ewe Mtume wa Allaah! Watu wa kitabu wanawasujudia maaskofu na wakuu wao; je, tusikusujudie? Akasema: “Lau ningelimwamrisha mtu amsujudie yeyote basi ningelimwamrisha mwanamke kumsujudia mume wake. Mwanamke hakutimiza haki za mume wake mpaka pale ambapo atakapomuomba kufanya naye jimaa wakati yeye atakuwa ameketi juu ya tandiko dogo na akamtii.” 5/207. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika “as-Swahiyhah” (3366)


Haki za mume zinakuwa maradufu ikiwa ni mwema, mchaMungu, mtu wa Dini na anahifadhi ´ibaadah za Allaah na kumtii. at-Tirmidhiy na Ibn Maajah wamepokea kupitia kwa Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anhu) ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:


“Hakuna mwanamke ambaye anamuudhi mume wake katika maisha haya isipokuwa mke wake katika al-Huur al-´Ayn anasema: “Usimuudhi, Allaah Akuue! Ni mgeni kwako tu. Karibuni atakuacha na kuja kwetu.”at-Tirmidhiy (1174) na Ibn Maajah (2014). Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (173).


Wanachuoni wanasema kwamba katika Hadiyth hii kuna matishio makali kwa wanawake wanaowaudhi waume zao.




                                    Mke mwema anatakiwa kuwa muadilifu kwa watoto wake 



Katika sifa za mke mwema ni kwamba Allaah Akimneemesha kwa kumpa watoto anafanya uadilifu baina yao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu. Fanyeni uadilifu baina ya watoto wenu.” 3544. Imepokelewa na an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allâhu ´anhu). Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (1240).


Hadiyth hii imepokelewa na Abu Daawuud na kumekuja Hadiyth nyingi kwa maana kama hii.



                                                  Mke mwema anatakiwa kubaki nyumbani 



Katika sifa za mke mwema ni kwamba anabaki nyumbani na hawi ni mwenye kutoka na kuingia nyumbani kila wakati. Anatoka nje tu wakati wa haja. Anapotoka hawi ni mwenye kujipodoa na uso ukiwa wazi. Anatakiwa kuteremsha chini macho yake na kuhifadhi tupu yake.


Tumepitia baadhi ya maandiko kuhusu hilo. Moja katika dalili ni yale ambayo at-Twabaraaniy amepokea katika “al-Awsaat” kupitia Saalim bin ´Abdillaah bin ´Umar kutoka kwa baba yake ambaye ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: 


“Mwanamke ni ´Awrah. Wakati anapotoka nje Shetani anamtazama (anamfanya) kama mabadiliko. Anakuwa yu karibu na Allaah pindi anapokuwa ndani kabisa ya nyumba yake.”2890 och 8096. Imaam al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika ”as-Swahiyhah” (2688).



                                                   Mke mwema hatoi siri za mume wake 



Katika sifa za mke mwema ni kwamba hatoi siri za mume wake na zile za ndani kwao. Hata kama kutatokea kutengana na kutokukubaliana ni lazima kwao wote wawili kumcha Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika suala hili.


Kuhusiana na hili amepokea Imaam Ahmad katika “al-Musnad” yake kupitia Amsaa´ bint Yaziyd ambaye ameeleza kwamba alikuwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanaume na wanawake walikuwa wamekaa kwake. Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): 


“Pengine mwanaume akasema aliyofanya na mke wake. Pengine mwanamke akasema aliyofanya na mume wake.” Wakanyamaza kimya. Nikasema: “Ndio, Mtume wa Allaah. Wanawake wanafanya hivyo. Wanaume wanafanya hivyo.” Akasema: “Msifanye hivyo. Hili linafanana na Shetani ambaye anapata mwanamke wa kishetani njiani na akaanza kujamiiana naye na huku watu wanatazama.”27583. Ni Swahiyh kupitia Hadiyth zingine kwa mujibu wa Shaykh al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) katika ”Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (2022). Razana ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (2011).


Amesema:


”Wanawake wanafanya hivyo. Wanaume wanafanya hivyo.” 


Ameanza na wanawake kwanza kwa sababu hili hufanywa sana kati yao na huwa kwa mara kidogo sana kati ya wanaume. Mwanamke huongea na marafiki zake na maswahiba zake kuhusu mambo kama hayo ya binafsi. Wengi katika wao hawajali kuongea siri za mume na mambo yao binafsi.


Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: 


“Hili linafanana na Shetani ambaye anapata mwanamke wa kishetani njiani na akaanza kujamiiana naye na huku watu wanatazama.”

Bi maana mwanamke na mwanaume wenye sifa kama hii na wanafichukua siri zao ni kama Shetani wa kiume ambaye amepata Shetani wa kike njiani na akajamiiana naye na huku watu wanatazama.




                                                                            HITIMISHO




Hizi ni baadhi ya sifa za mke mwema ambazo nimezikusanya kutoka katika maandiko ya Allaah (´Azza wa Jalla) na Sunnah za Mtume Mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Nimefanya hivyo kwa kutaraji kwa Mola (Subhaanahu) Amnufaishe kwazo yule Amtakaye katika waja Wake.



Ni Yeye Peke Yake ndiye mwenye kuwafikisha.



Ninamuomba Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwa Majina Yake Mazuri na Sifa Zake Kuu Atuongoze sote katika njia iliyonyooka, yale tunayojifunza iwe ni hoja yetu na si dhidi yetu, Atubariki katika maneno yetu, matendo yetu, wakati wetu, wake zetu, watoto wetu, mali zetu na maisha yetu yote, Atutengenezee Dini yetu ambayo ndio kinga yetu, Atutengenezee maisha yetu ya duniani ambayo tunaishi na maisha yetu ya Aakhirah ambayo ndio kituo chetu cha mwisho, Afanye uhai kwetu kuongezeka iwe ni kheri ya kila kitu na mauti iwe ni raha kwetu kutokana na kila shari, Awatengeneze wanawake wa Waislamu na wasichana wao, Awaongoze katika njia iliyonyooka, warudi Kwake kwa njia nzuri na Awaepushe na fitina zote zilizodhahiri na zilizojificha na Atuongoze sote katika kila kheri Anayoipenda na Kuiridhia. Hakika Yeye (Tabaaraka wa Ta´ala) ni Mwenye kuzisikia Du´aa, Yeye ndiye wa kuwekewa matarajio, Anatutosheleza na ni Mbora wa kuyasimamia mambo.


Wito wetu wa mwisho tunamhimidi Allaah, Mola wa walimwengu.


Swalla Allaahu was-Sallam, wa Baarak wa an´aam ´alaa ´abddihiy wa Rasuulihiy Mustwafaaa Muhammad bin ´Abdillaah. SwalawaatuAllaahi wa salaam ´alayhi, wa ´alaa aalihiy, wa Swahbihii ajma´iyn..Asli ya kijitabu hichi ni muhadhara ambao nimepanga kidogo lakini hata hivyo nikaacha ubaki usulubu wake kama muhadhara.



                                                     NA   ALLAAH  ANAJUA   ZAIDI


Ukiwa na Maoni ,Ushauri ,Swali Tafadhali wasiliana nami kwa Email : https://ift.tt/2PWXnBY  au Pia Unaweza Kujiunga nasi katika Whatssap Group kwa Namba 0714-974-397 ( Imaam Masjid  Tawbah) 


Pia unaweza Kujiunga Nasi katika Harakati mbalimbali za Dini kwa sasa tupo katika Harakati za KUJENGA  MADRASA  na  UKUSANYAJI   WA  JUZUU  NA  MISAHAFU.




                                                                     WABILLAAH  TAWFIQ



from fisabilillaah.com https://ift.tt/2TOo7mq
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...