عن عبدالله بن الزبير قال: كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يُهَلِّلُ بهنَّ دُبُرَ كلِّ صلاةٍ:
لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah ibn Zubayr amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitamka Tahliyl (laa ilaaha illa Allaah) kila baada ya Swalaah:
لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون
Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa hawla walaa quwwata illaa biLLaah. Laa ilaaha illa-Allaah. Walaa na’-budu illaa Iyyaahu. Lahun-Ni’-matu walahul-fadhwlu walahuth-thanaaul-hasan. Laa ilaaha illa-Allaah Mukhliswiyna Lahud-diyna walaw karihal-kaafiruwn
”Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye ni Qadiyr (Muweza) wa kila kitu. Hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allaah. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, wala hatumwabudu ila Yeye, ni Zake neema, na ni Wake ubora, na ni Zake Sifa nzuri zote, Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kumtakasia Dini Yake, ijapokuwa wanachukia makafiri.” [Muslim (1/415) [594]
Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni
عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرَةَ، أَنَّهُ قَالَ لأَبِيهِ يَا أَبَةِ إِنِّي أَسْمَعُكَ تَدْعُو كُلَّ غَدَاةٍ: ((اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ)) تُعِيدُهَا ثَلاَثًا حِينَ تُصْبِحُ وَثَلاَثًا حِينَ تُمْسِي. فَقَالَ إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدْعُو بِهِنَّ فَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَسْتَنَّ بِسُنَّتِهِ
Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah (رضي الله عنه) ambaye amesema kuwa alimwambia baba yake: “Ee baba yangu, mimi nakusikia ukiomba hivi kila asubuhi:
اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ
Allaahumma ‘aafiniy fiy badaniy, Allaahumma ‘aafiniy fiy sam-’iy, Allaahumma ‘aafiniy fiy baswariy, laa ilaaha illaa Anta. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minalkufri walfaqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ‘adhaabil qabri laa ilaaha illaa Anta. (mara 3)
Ee Allaah, nipe ‘aafiyah (afya, siha, usalama, amani) ya mwili wangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah ya masikio yangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah macho yangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najikinga Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mwabudiwa wa hakiila Wewe)) Unaomba mara tatu asubuhi na jioni. Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitamka maneno hayo katika kuomba du’aa basi nami napenda kufuata Sunnah yake.” [Abuu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [22], Ibn As-Sunniy [69], Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad na isnadi yake ameipa daraja ya Hasan Al-‘Allaamah Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaaar (Uk. 26). Pia Swahiyh Abiy Daawuwd (5090).]
Du’aa Unaporudi Safarini
عنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضى الله عنهما أَنَّرَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَفَلَمِنْ غَزْوٍ أَوْ حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ شَرَفٍمِنَ الأَرْضِ ثَلاَثَ تَكْبِيرَاتٍ، ثُمَّ يَقُولُ: ((لاَ إِلَهَإِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُالْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَعَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُوَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ))البخاري
Imepokelewa kutoka kwa Ibn ’Umar (رضي الله عنهما) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa pindi anaporudi vitani au kutoka Hajj au ’Umrah alikuwa katika kila akipanda mlima akileta Takbiyrah (Allaahu Akbar) mara tatu kisha akisema:
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamd, wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Aaibuwna taaibuwna, ’aabiduwna, saajiduwna, li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa-Allaahu Wa’dahu, wa Naswara ’Abdahu, wa Hazzamal-ahzaaba Wahdahu
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ufalme ni Wake, na Himdi ni Zake, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Tunanarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, tunasujudu, tunamhimidi Rabb wetu. Amesadikisha Allaah ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi peke Yake [Al-Bukhaariy katika Kitaab Al-Hajj, Kitaab Al-’Umrah, Kitaab Al-Maghaazi, Kitaab Al-Jihaad Was-Sayr (7/163) [1797], Muslim Kitaab Al-Hajj (2/980) [1344].
Maneno Manne Ayapendayo Allaah: Subhaana Allaah,
Wal-HamduliLLaah Wa Laa Ilaaha Ilaa-Allaah…..
عَنْ سَمُرَةَ بْنِ جُنْدَبٍ، قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلىالله عليه وسلم: ((أَحًبُّ الْكَلامِ إِلَى اللَّهِ أَرْبَعٌ:سُبْحَانَ اللَّهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ، وَلا إِلَهَ إِلا اللَّهُ، وَاللَّهُأَكْبَرُ، لا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ))
Imepokelewa kutoka kwa Samurah Bin Jundab kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:((Bora ya maneno kwa Allaah ni manne:
سُبْحَانَ اللهِ، والْحَمْدُ للهِ، وَلاَ إِلَهَ إَلاَّ اللهُ واللهُ أَكْبَرُ
Subhaana-Allaah, walhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa.
… si vibaya kuanza kwa lolote katika haya)) [Muslim (3/1685)]
Kutamka Laa Ilaaha Illa-Allaah Wakati Wa Mafazaiko
عَنْ زَيْنَبَ بِنْتِ جَحْشٍ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليهوسلم دَخَلَ عَلَيْهَا فَزِعًا يَقُولُ: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ،وَيْلٌ لِلْعَرَبِ مِنْ شَرٍّ قَدِ اقْتَرَبَ، فُتِحَ الْيَوْمَ مِنْرَدْمِ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مِثْلُ هَذَا)) وَحَلَّقَ بِإِصْبَعِهِوَبِالَّتِي تَلِيهَا، فَقَالَتْ زَيْنَبُ فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِأَنَهْلِكُ وَفِينَا الصَّالِحُونَ؟ قَالَ: ((نَعَمْ، إِذَا كَثُرَالْخَبَثُ))
Imepokelewa kutoka kwa Zaynba Bint Jahsh (رضي الله عنها) kwamba Nabiy alingia chumbani kwake akiwa katika hali ya kufazaika akasema:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ
((Laa ilaaha illa Allaah [hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah]
Ole kwa Waarabu kutokana na shari iliyokaribia. Leo limefunguka shimo katika boma la kizuzi cha Ya-ajuwj na Ma-ajuwj kama hivi!)) Akafanya kiduara kwa kufunga kidole chake cha gumba na cha shahada. Zaynab akasema: Kisha nikasema: Ee Rasuli wa Allaah, hivi tutaangamia na hali tumo watu wema?”. Akasema: ((Ndio pindi maovu yakizidi)) [Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/181) [3346], Muslim (4/2208) [2880] na Riwaayah nyengine: “Aliamka usingizini akasema….
Mema Yanayobakia Daima
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((خُذُوا جُنَّتَكُمْ)) قُلْنَا يَا رَسُولَ اللهِ : مِنْ عَدُوٍّ قَدْ حَضَرَ ؟ ، قَالَ: ((لاَ، جُنَّتَكُمْ مِنَ النَّارِ، قُولُوا : سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، فَإِنَّهَا يَأْتِينَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مُنْجِيَاتٍ، وَمُقَدَّمَاتٍ ، وَهُنَّ الْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Jikingeni!)) Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah; Je adui ameshatufikia? Akasema: ((Hapana bali kinga yenu kutokana na moto. Semeni:
سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ
Subhaana-Allaah, wal-HamduliLLaah, wa laa ilaaha illa-Allaah, wa Allaahu Akbar
Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa
Kwani yatakuja zitakuja hizo (Adhkaar) Siku ya Qiyaamah kama ni kinga na kitangulizi, nazo ni Mema yanayobakia daima)) [An-Nasaaiy fiy Sunan Al-Kubraa (10684), Atw-Twabaraniy fiy Al-Mu’jim Al-Awsatw (4027), na ameisahihisha Al-Abaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’ (3214), Swahiyh At-Targhiyb (1567), na kwa Riwaayah nyenginezo amesahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’ (3264), (6/482)]
عن بِلاَلَ بْنَ يَسَارِ بْنِ زَيْدٍ، مَوْلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ سَمِعْتُ أَبِي يُحَدِّثُنِيهِ عَنْ جَدِّي أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: (( مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ ))
Imepokelewa kutoka kwa Bilaal bin Yasaar bin Zayd mkombolewa wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba nimesikia baba yangu amenihadithia kutoka kwa babu yangu kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayesema:
أَسْتَغْفِرُ اللهَ الْعَظِيمَ الَّذِي لَا إِلَهَ إلَّا هُوَ الحَيُّ القَيّوُمُ وأَتُوبُ إِلَيهِ
Astaghfiru-Allaahal-‘Adhwiyma Alladhiy laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuwmu wa atuwbu Ilayhi
Namuomba maghfira kwa Allaah Mtukufu Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, na ninarejea kutubuia Kwake...
Allaah Atamghufuria kama ana makosa hata kama ya kukimbia vitani)) [Abu Daawuwd (2/85) [1517], At-Tirmidhiy (5/569) [3577], Al-Haakim na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahaby (1/511) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله). Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]
Du’aa ya Swafaa na Marwah na Unaporudi Safarini
Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alisoma hivi mara tatu alipopanda jabali la Swafaa na baina yake akiomba du’aa, kisha akafanya alipokuwa Marwah kama alivyofanya alipokuwa Swafaa:
لا إِلهَ إلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu, wa hazzamal ahzaaba Wahdah
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Muslim (2/888) [1218]
Pia:
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَفَلَ مِنْ غَزْوٍ أَوْ حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ شَرَفٍ مِنَ الأَرْضِ ثَلاَثَ تَكْبِيرَاتٍ، ثُمَّ يَقُولُ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporudi vitani au Hajj au ‘Umrah kila alipopanda mnyanyuko wa ardhi alileta Takbiyrah (Allaahu Akbar) mara tatu kisha akisema:
لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ
Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Aayibuwna, taaibuwna, ‘aabiduwnaa, saajiduwna, li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa Allaahu Wa’dahu, wa-Naswara ’Abdahu wa-Hazzama Al-Ahzaaba Wahdahu
Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Tunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, tunasujudu na Rabb wetu tunamsifu. Amesadikisha ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Al-Bukhaariy na wengineo]
Du’aa Ya Kuogopa Ukandamizaji Na Dhulma Ya Mtawala
عن عبدِ اللَّهِ بنِ مسعودٍ إذا كانَ على أحدِكم إمامٌ يخافُ تَغطرُسَهُ أو ظلمَهُ فليقلِ
Athar ya ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Ikiwa kuna aliye na madaraka nawe ambaye unaogopa ukandamizaji wake na dhulma yake, basi aseme:
أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ
Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim, kun liy jaaran min (fulani bin fulani) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum aw yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta
Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemkhofu]) na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe.
[Al-Bukhaariy Al-Adab Al-Mufrad[707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [545, 546].
Du’aa ya Kumwogopa Mtawala na Kukhofu
عنِ ابنِ عبَّاسٍ قالَ إذا أتيتَ سلطانًا مَهيبًاتخافُ أن يسطوَ بِكَ فقلِ
Athar ya Ibn ’Abbaas (Radhwiya Allaahu ’anhumaa) ambaye amesema: Utakapokwenda kwa mtawala anayetisha ambaye utakhofia kuwa atakushambulia, basi sema:
الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ
Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kunliy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3]
Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu (Mshindi) kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu Ambaye Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja (fulani - mtaje mtu unayemhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu. Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka sifa Zako na Umeheshimika ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako.
[Al-Bukhaariy - Adabul-Mufrad [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad[546], Swahiyh At-Targhiyb (2238)].
Adhkaar za Asubuhi na Jioni.
عَنْ عَبْدِ اللهِ بِنْ مَسْعُود رضي الله عنه، قَالَ: كَانَ نَبِيُّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم إِذَا أَمْسَى قَالَ: ((أَمْسَيْنَا وَأَمْسَى الْمُلْكُ لِلَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ)) قَالَ: أُرَاهُ قَالَ فِيهِنَّ: (( لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ رَبِّ أَسْأَلُكَ خَيْرَ مَا فِي هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَخَيْرَ مَا بَعْدَهَا وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا فِي هَذِهِ اللَّيْلَةِ وَشَرِّ مَا بَعْدَهَا رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْكَسَلِ وَسُوءِ الْكِبَرِ رَبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ عَذَابٍ فِي النَّارِ وَعَذَابٍ فِي الْقَبْرِ)) وَإِذَا أَصْبَحَ قَالَ ذَلِكَ أَيْضًا: ((أَصْبَحْنَا وَأَصْبَحَ الْمُلْكُ لِلَّهِ ))
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas’uwd (رضي الله عنه)kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa pindi anapofika jioni akisema:
أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لاإلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ،
Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah wal-HamduliLLaahi. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu
Tumeingia wakati wa jioni na umekuwa Ufalme ni wa Allaah, na Himdi ni Zake Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali yakuwa Peke Yake, Hana mshirika (Msimuliaji akasema): Nadhani alisema pia:
لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍقدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِوَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ مافي هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّأَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّأَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ وَعَـذابٍ فيالقَـبْر
Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhihil-laylati wakhayra maa ba’dahaa, wa a’uwdhu bika minsharri maa fiy haadhihil-laylati washarri maa ba’dahaa, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri
Ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye juu ya kila kitu ni Qadiyr (Muweza). Rabb wangu, nakuomba khayr zilizomo katika usiku wa leo, na khayr za baada yake, na ninajikinga Kwako kutokana na shari zilizomo katika usiku wa leo na shari za baada yake. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ubaya. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi
Na alipoamka asubuhi pia alisema (kama hivyo kwa kutaja kuamka asubuhi):
أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله
Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaah
Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah…
[Muslim (4/2088) [2723]
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2FNnSVF
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni