Translate

Ijumaa, 30 Novemba 2018

Allaah anaonekana usingizini?

Swali: Je, Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anaonekana usingizini?

Jibu: Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba mapote yote yanathibitisha haya na kwamba Allaah anaonekana usingizini isipokuwa tu Jahmiyyah. Kutokana na kupinga kwao vikali wamepinga kwamba Allaah haonekani usingizini. Lakini hili halipelekei katika kufananisha. Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) ametaja kwamba muumini anamuona Mola wake kwa mujibu wa matendo yake. Matendo yake yakiwa mema basi anamuona Mola wake katika muonekano mzuri. Matendo yake yakiwa mabaya basi anamuona Mola wake kwa mujibu wa matendo yake. Kwa ajili hii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimemuona Mola wangu kwa sura nzuri.”

Hili halipelekei kufananisha juu ya kwamba Allaah anakuwa katika sura aliyomuona mtu. Lakini hata hivyo inakuwa ni kuona kweli. Kwa hivyo mtu anamuona Allaah kutokanaa na vile matendo yake yalivyo.



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2E4OnEn
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...