Translate

Alhamisi, 29 Novemba 2018

066-Asbaabun-Nuzuwl: Sasa Allaah Amekukhafifishieni Na Amejua Kwamba Kati Yenu Kuna Udhaifu…

 

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

Al-Anfaal:  65-66

 

066- Sasa Allaah Amekukhafifishieni Na Amejua Kwamba Kati Yenu Kuna Udhaifu…

 

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

  

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ حَرِّضِ الْمُؤْمِنِينَ عَلَى الْقِتَالِ ۚ إِن يَكُن مِّنكُمْ عِشْرُونَ صَابِرُونَ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ يَغْلِبُوا أَلْفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ﴿٦٥﴾

65. Ee Nabiy! Shajiisha Waumini kupigana vita. Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) ishirini wanaosubiri, basi watawashinda (makafiri) mia mbili. Na wakiweko miongoni mwenu mia watawashinda elfu katika wale waliokufuru kwa kuwa wao ni watu wasiofahamu. 

 

الْآنَ خَفَّفَ اللَّـهُ عَنكُمْ وَعَلِمَ أَنَّ فِيكُمْ ضَعْفًا ۚ فَإِن يَكُن مِّنكُم مِّائَةٌ صَابِرَةٌ يَغْلِبُوا مِائَتَيْنِ ۚ وَإِن يَكُن مِّنكُمْ أَلْفٌ يَغْلِبُوا أَلْفَيْنِ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ﴿٦٦﴾

66. Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kati yenu kuna udhaifu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) mia wenye kusubiri, watawashinda (makafiri) mia mbili; na wakiweko miongoni mwenu (Waumini) elfu, wawatashinda (makafiri) elfu mbili kwa idhini ya Allaah. Na Allaah Yu pamoja na wenye kusubiri.

 

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنه) kwamba pindi ilipoteremka: “Wakiweko miongoni mwenu (Waumini) ishirini wanaosubiri, basi watawashinda (makafiri) mia mbili.” [Al-Anfaal: 65] ikawa jambo gumu kwa Waislamu kwamba mtu mmoja hapaswi kukimbia (vita) mbele ya (makafiri) kumi. Basi ikaja takhfifu pindi (Allaah) Aliposema: “Sasa Allaah Amekukhafifishieni na Amejua kwamba kati yenu kuna udhaifu. Hivyo basi wakiweko miongoni mwenu (Waumini) mia wenye kusubiri, watawashinda (makafiri) mia mbili.” Basi Allaah Alipowafanyia takhfifu kwa kuwapunguzia idadi (ya maadui ambao kila mmoja wao atapambana nao), ikapungua subira yao kadiri ya walivyofanyiwa takhfifu (ya idadi ya maadui watakaopigana nao). [Al-Bukhaariy na wengineo].

 

 

 

 

 

 

 

 

 



from Alhidaaya.com https://ift.tt/2rbA8p3
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...