Kwa wale wasiomfahamu, mende hawa ni wadudu wenye miguu sita, upande wa kushoto miguu mitatu, na upande wa kulia miguu mitatu.
Mende wana taya za kutafunia, miili iliyokuwa bapa, na kichwa kidogo. Wengi wao wana rangi nyekundu, kahawia mpaka nyeusi. Macho ya mende ni kama macho ya inzi, yaani ana jicho ndani ya jicho. Maana yake ni kuwa, ndani ya jicho lake moja kuna macho madogo madogo mengi.
Pia, mende wana antena mbili na mwili wao umegawanyika katika vipande vitatu yaani sehemu ya kichwa, kifua (kati kati) na sehemu ya nyuma. Kadhalika, katika kila kipande kuna jozi za miguu.
Mende ni kundi la wadudu linalofahamika kwa Jina la ‘blattodea,’ kundi ambalo pia wapo mchwa. Wataalaamu wa elimu ya viumbe wanasema kuwa, kuna aina 4,600 za mende lakini wanaopatikana katika mazingira binadamu ni aina 30. Aina nne kati ya hao 30 ni mende waharibifu. Katika bara la Amerika Kaskazini kuna aina 50 na kule Australia kuna aina 450.
Aina nyingi za mende wanapatikana sehemu za joto. Kwa ujumla, aina nyingi za mende wanapenda kuishi kijamii. Hakika, viumbe hawa, mende, wameonekana katika mazingira wanayopatikana binadamu kwa karne nyingi. Watu wengi wanawatazama mende kama wadudu wachafu lakini si kuwa wanakula uchafu kila wakati.
Ukubwa wao wengi ni kama kucha ya dole gumba ila kuna aina moja ya mende inapatikana Australia inaitwa ‘giant burrowing cockroach’ ana urefu wa sentimita tisa.
Chakula
Katika chakula, mende ni ‘omnivuorous’ wanakula kila kitu ikiwemo matunda, nafaka, karatasi, ngozi, nywele, mimea iliyokufa, mbao zilizooza, mkate nk. Inatajwa katika matumbo yao kuna bacteria fulani ambao husaidia kusaga vyakula.
Uzazi
Katika uzazi, mende wanataga kati ya mayai 300-400 kulingana na aina. Mende huchukua masaa matano kwa kutaga. Kadhalika kuna hatua anapitia mende kabla ya kuwa mende kamili kama vile yai, nyimphi kisha mende kamili.
Kutoka kuwa yai hadi mende, inachukua miezi mitatu hadi minne. Muonekano wa mayai yao ni kama gundi fulani, yananata na madogo.
Mambo 10 usiyoyajua kuhusu mende
- Mende ni wadudu wavumilivu sana wanaoweza kuishi kwenye hali zote; kwenye joto sana na hata baridi sana, yaani hata kule ncha ya Kaskazini kwenye theluji pia wanapatikana.
- Allah Aliyetukuka amejaalia katika miili ya mende kuwa wana uwezo wa kutengeneza kitu fulani kinaitwa ‘anti freeze’ ambayo inawakinga wasigande hata kwenye baridi kali.
- Mende huwa wanatambuana baina ya kundi moja na jingine kwa harufu zao, yaani mende wa kundi fulani anaweza akatambua hili si kundi lake kwa harufu.
- Kila kundi la mende lina harufu yake.
- Maisha ya mende wengi ni usiku.
- Mwanga ukiwaelekea, mende huwa wanakimbia, ingawa kuna aina moja ya mende inapatikana Asia, yeye anapenda mwanga.
- Mende wanapokutana (kujamiiana) kipekee sana. Huwa mmoja anaangalia huku mwingine kule, yaani hawatazamani.
- Jike la mende huwa ndio hasa linavutiwa na dume baada ya dume kufanya mchezo fulani wa madaha.
- Dume hufanya hivyo baada ya kupata harufu ya jike ya anapojiona kuwa yupo tayari.
- Ipo aina moja ya mende jike huwa linajamiiana mara moja tu katika maisha yake yote.
from TIF https://ift.tt/2Rm7pt6
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni