Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Tunaendeleaa.........
07. Pili: Mwenye kuweka baina yake na Allaah mkati na kati
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Mwenye kuweka baina yake na baina ya Allaah wakati na kati akawa anawaomba, kuwataka uombezi na kuwategemea anakufuru kwa maafikiano.
MAELEZO
Anayeweka baina yake na Allaah wakati na kati, kwa mfano akamuomba maiti au aliyemo ndani ya kaburi kama kusema: "Ee fulani! Niombee kwa Allaah." Pamoja na kwamba aina hii inaingia katika ile aina ya kwanza lakini hata hivyo ni maalum kuliko hiyo ya kwanza. Shirki ni kumfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah kwa njia ya jumla. Kwa mfano mtu akamuomba asiyekuwa Allaah, akachinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah au akamuwekea nadhiri asiyekuwa Allaah.
Kuhusiana na kitenguzi cha pili hichi ni mtu akaweka baina yake yeye na Allaah wakati na kati kwa madai ya kwamba wanamfikishia haja zake kwa Allaah. Kwa mfano mtu akamwambia aliyemo ndani ya kaburi: "Ee fulani! Niombee kwa Allaah", "Ee Mtume wa Allaah! Niombee". Bi maana amemfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mkati na kati baina yake yeye na Allaah. Hii ni shirki. Kwa sababu amemuomba asiyekuwa Allaah. Mwenye kumuomba asiyekuwa Allaah ameshirikisha. Huyo anaguswa na maandiko yenye kusema:
: َُّك َ ُضر ََل ي َ ُ َك و َع نف َ ا ََل ي َ م ِ ـه اللَّ ونِ ُ ن د ِ م ُ َْدع ََل ت َ ۖ َني و مِ ِ ال الظَّ َ ِّن ِ ذًا م ِ َك إ نَّ ِ إ َ َت ف ْل َ َع ِن فـ إ َ ف
“Na wala usiombe badala ya Allaah asiyekunufaisha na wala asiyekudhuru. Na ukifanya [hivyo], basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.”10:106
َني ِ َّذب َ ع ُ الْم َ ن ِ ُكوَن م َ ت َ فـ َ ر َ ا آخ ً َٰه لَـ ِ إ ِ ـه اللَّ َ ع َ م ُ َْدع ََال ت ف
"Basi usiombe [au kuabudu] pamoja na Allaah mungu mwengine ukaja
kuwa miongoni mwa watakaoadhibiwa."26:213
3 ٌ يم َظِ ع ٌ َك لَظُْلم ْ ِّر َّن الشِ ِ إ
"Hakika shirki ni dhulma kubwa mno.” 31:13
َ و ِ ه ِّ بِ َ َ ر ند عِ ُ ه ُ اب َ س ََِّّنَا حِ إ َ ف ِ ه ِ ب ُ َن لَه ا َ ه ْ ر ُ ََل بـ َ ر َ ا آخ ً َٰه لَـ ِ إ ِ ـه اللَّ َ ع َ م ُ ْدع َ ن ي َ وَن م ۖ ُ ر ِ الْ َكاف ُ ح ِ ل ْ ف ُ ََل يـ ُ نَّه ِ إ
"Na yeyote yule anayeomba [du’aa au kuabudu] pamoja na Allaah mungu mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Mola wake - hakika hawafaulu makafiri."5 23:117
Amemuita kuwa ni kafiri.
ْ ُكم كِ ْ ر ِشِ وَن ب ُ ُر ْكف َ ي ِ ة َ ام َ ي ِ الْق َ م ْ و َ يـ َ و
"Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu." 35:14
ري طْمِ ِ ن ق ِ ُكوَن م ِ ل َْ ا َي َ م ِ ه ِ ون ُ ن د ِ وَن م ُ َْدع ت َ ين ِ الَّذ َ و ْ وا لَ ُكم ُ اب َ َج ت ْ ا اس َ وا م ُ ع ََسِ ْ لَو َ و ْ ُكم َ اء َ ُع وا د ُ ع َ م ْ َس ََل ي ْ ُم وه ُ َْدع ۖ ِن ت إ ْ ُكم كِ ْ ر ِشِ وَن ب ُ ُر ْكف َ ي ِ ة َ ام َ ي ِ الْق َ م ْ و َ يـ َ و
"Na wale mnaowaomba badala Yake hawamiliki hata kijiwavu cha kokwa ya tende. Mkiwaomba hawasikii maombi yenu na hata wakisikia, basi [wasingeliweza] kukujibuni. Na Siku ya Qiyaamah watakanusha ushirikina wenu."35:13-14
Allaah ameita yale wayafanyayo kuwa ni shirki.
Kwa hivyo yule mwenye kuweka baina yake na Allaah mkati na kati ambapo akawa anamuomba badala ya Allaah, anamuomba uombezi au anamtegemea anakufuru kwa maafikiano ya waislamu. Hii ni aina ya shirki.
Kutegemea maana yake ni mtu akauegemeza moyo wake kwake na akamwachia mambo yake ili aweze kufikia mahitajio yake.
Kitenguzi cha kwanza kimeenea na hichi cha pili ni maalum. Kitenguzi cha kwanza ni kushirikisha katika ´ibaadah ya Allaah. Ni mamoja ´ibaadah hiyo iwe ni du´aa, kuchinja, nadhiri, kutii katika uhalalishaji au uharamishaji, Rukuu´ au Sujuud.
Kitenguzi cha pili ni maalum. Nacho ni mtu akaweka baina yake yeye na Allaah mkati na kati ambapo akawa anamuomba, kumtaka uombezi na kumtegemea ili kufikia mahitajio yake. Mtu akamfanya maiti kuwa baina yake yeye na Allaah na kusema: "Ee fulani! Niombee kwa Allaah", "Ee fulani! Nifikishie haja yangu kwa Allaah". Hili linamuhusu aliye hai vilevile. Kwa mfano akamtegemea kuwa atamuokoa na Moto, amnusuru na maadui zake, amfanyie wepesi katika riziki, kupata mtoto au kuingia Peponi, Mtu huyu amemtegemea katika mambo ambayo hategemewi yeyote isipokuwa Allaah.
Hivyo basi, yule mwenye kuweka baina yake yeye na Allaah mkati na kati, sawa awe hai au maiti, anakuwa mshirikina. Aliye hai anaombwa mambo ambayo anayaweza. Kwa mfano unaweza kumuomba aliye hai akutengenezee gari yako, akukope pesa au kukulimia shamba. Ama kumuomba aliye hai akusamehe dhambi zako, akuokoe na Moto, akukunjulie riziki yako, akunusuru dhidi ya adui yako au asikuzuie kuingia Peponi ni mambo ambayo hayawezi na hayamiliki. Kwa hiyo ni shirki.
Mtu akiweka baina yake na Allaah wakati na kati kwa njia ya kwamba akawa anawaomba badala ya Allaah, anawataka uombezi au anawategemea na akawaachia mambo yake ili aweze kufikia mahitajio yake anakufuru kwa maafikiano ya waislamu. Ndio maana mwandishi amesema:
"Anakufuru kwa maafikiano."
Dalili ya hili ni dalili zile zile zenye kusema kuwa kufanya shirki katika ´ibaadah ya Allaah ni kufuru yenye kumtoa mtu katika Uislamu. Dalili ambazo ndani yake mna kuharamisha shirki, kumuomba asiyekuwa Allaah katika mambo yasiyoweza yeyote isipokuwa Allaah ndio dalili zile zile za kitenguzi hichi kinachovunja Uislamu. Amesema (Ta´ala):
َُّك َ ُضر ََل ي َ ُ َك و َع نف َ ا ََل ي َ م ِ ـه اللَّ ونِ ُ ن د ِ م ُ َْدع ََل ت َ ۖ َني و مِ ِ ال الظَّ َ ِّن ِ ذًا م ِ َك إ نَّ ِ إ َ َت ف ْل َ َع ِن فـ إ َ ف
“Na wala usiombe badala ya Allaah asiyekunufaisha na wala asiyekudhuru. Na ukifanya [hivyo], basi hakika utakuwa miongoni mwa madhalimu.”10:106
Bi maana usije kuwa katika washirikina.
ا ً د َ أَح ِ ـه اللَّ َ ع َ وا م ُ َْدع ََال ت ف ِ ـه لَّ ِ ل َ د اجِ َ َس أَ َّن الْم َ و
"Na kwamba Misikiti ni [kwa ajili] ya Allaah, basi msiombe yeyote pamoja na Allaah."72:18
ا ً د َ أَح ِ ه ِ ْشِرُك ب ََل أُ َ و ِّ ِِب َ و ر ُ ْع ََِّّنَا أَد إ ْ ُل ق
"Sema: “Hakika mimi namuomba Mola wangu [Pekee] na wala simshirikishi na yeyote".”72:20
Kwa hivyo yule mwenye kuweka baina yake yeye na Allaah wakati na kati akawa ni mwenye kuwaomba, kuwataka uombezi au akawategemea kwa njia ya kwamba akawaachia mambo yake ili aweze kufikia mahitajio yake amefanya shirki kwa sababu amemfanyia ´ibaadah asiyekuwa Allaah.
08. Tatu: Asiyemkufurisha kafiri au akatilia shaka ukafiri wake.
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Asiyekuwakufurisha washirikina au akawa na shaka juu ya ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi amekufuru.
MAELEZO
Kitenguzi cha tatu miongoni mwa mambo yanayotengua Uislamu ni yule asiyemkufurisha mshirikina au akatilia shaka ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi amekufuru kwa maafikiano.
Neno "mshirikina" linahusu makafiri wote ikiwa ni pamoja na mayahudi, manaswara, wenye kuabudu makaburi, wakomunisti na wakanaMungu. Wote hawa ni washirikina. Kinachowakutanisha ni kitu kimoja: kumshirikisha Allaah (´Azza wa Jall).
Mayahudi ni washirikina kwa sababu hawamwamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo ni shirki. Manaswara ni washirikina kwa kuwa na wao hawamwamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wanamuabudu ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam). Waabudu makaburi, waabudu moto na wanafiki ni washirikina.
Hivyo basi, yule asiyekuwakufurisha washirikina ni kafiri. Kadhalika mwenye kuwa na shaka juu ya ukafiri wa makafiri. Mwenye kutilia shaka kuwa mayahudi, manaswara au wenye kuabudu makaburi ni makafiri basi na yeye ni kafiri kutokana na shaka yake hii.
Vilevile mwenye kuonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi. Kwa mfano mtu akasema kuwa anaona kuwa mayahudi wako katika dini sahihi na manaswara wako katika dini sahihi. Mfano mwingine ni kama mtu aulizwe juu ya mayahudi na manaswara ambapo akasema kuwa hawezi kusema lolote juu yao.
Akajibu kwa kusema kuwa mayahudi, manaswara na waislamu wote wako katika dini na ambaye anataka kuamini Uislamu, uyahudi au unaswara ana haki ya kufanya hivo. Hii ni shirki. Huyu kwa maafikiano anakuwa kafiri kwa sababu ameonelea kuwa madhehebu ya washirikina ni sahihi na vilevile hakuwakufurisha.
Kadhalika pale atapotilia shaka na kusema kuwa hajui kama ni makafiri au sio makafiri kwa sababu mayahudi wameteremshiwa Kitabu ambacho ni Tawrat, manaswara wameteremshiwa Injiyl na waislamu wameteremshiwa Qur-aan. Kwa hivyo mimi sijui kama ni makafiri au sio makafiri. Huyu anakufuru akitilia shaka. Ni lazima aazimie ukafiri wa mayahudi, manaswara na waabudu makaburi.
Dalili ya hili ni maneno Yake (Ta´ala):
: َٰ َى ثْـق ُ الْو ِ ة َ و ْ ر ُ الْع ِ َك ب َ ْس َم ت ْ اس ِ َد َق فـ ِ ـه اللَّ ِ ن ب ِ م ْ ؤ ُ يـ َ ِت و اغُو الطَّ ِ ب ْ ُر ْكف َ ن ي َ َم ف
"Basi atakayemkanusha twaaghuwt [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti." 02:256
Asiyekuwakufurisha washirikina au akawa na shaka juu ya ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi basi hakukufuru Twaaghuut. Imani haisihi isipokuwa kwa kupatikana mambo mawili:
La kwanza: Kukufuru Twaaghuut.
La pili: Kumuamini Allaah.
09. Maana ya "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah.
Twaaghuut ni kila ambacho mja anakivukia mipaka katika vinavyoabudiwa, kufuatwa au kutiiwa. Kila chenye kwenda kinyume na Shari´ah ni Twaaghuut. Kimeitwa kuwa ni "Twaaghuut" kutokamana na neno Twughyaan, nayo maana yake ni kuvuka mpaka.
Maana ya kukufuru Twaaghuut ni wewe kujitenga mbali na ´ibaadah anayofanyiwa asiyekuwa Allaah, ukaikanusha, kuichukia, kujenga uadui na kuwajengea uadui wenye nayo. Kukufuru Twaaghuut ni kujitenga na kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah, kukanusha kila ´ibaadah anayofanyiwa asiyekuwa Allaah, kuikanusha, kuichukia, kuwachukia wenye nayo na kuwajengea uadui. Hii ndio maana ya kukufuru Twaaghuut.
Namna ya kujiepusha Ni wewe kujiweka mbali na shirki aina zote na kila dini isiyokuwa ya Kiislamu, uikemee, uikanushe, uichukie, uinjengee uadui na uwanjengee uadui wenye nayo. Hili ndio jambo la kwanza.
Jambo la pili ni kumuamini Allaah. Utapofanya mambo mawili haya basi wewe ni mpwekeshaji. Bi maana ukakufuru Twaaghuut na kumuamini Allaah. Hii ndio maana ya "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah".
Maana yake ni kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Hii ndio kalima ya Tawhiyd. Hili ndio neno la Tawhiyd linalomkinga mwenye nalo na shirki. Ndio neno ambalo kwa ajili yalo Allaah amewatuma Mitume, akawagawanya watu baina ya waangamivu na wenye furaha, kukasimama Jihaad, kukasimama Qiyaamah na kwa ajili yake kukaumbwa Pepo na Moto.
"Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" maana yake ni kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Neno "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" ndani yake mna mambo mawili:
a) Kufuru.
b) Imani.
"Hakuna mungu wa haki... "
huku ni kuikufuru Twaaghuut.
"... isipokuwa Allaah."
huku ni kumuamini Allaah.
"Hakuna mungu wa haki... " huku ni kukanusha aina zote za ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah na ndio maana ya kukufuru Twaaghuut.
".... isipokuwa Allaah" unamthibitishia Allaah (´Azza wa Jall) aina zote za ´ibaadah. Huku ndio kumuamini Allaah.
10. Asiyewakufurisha washirikina hakukufuru Twaaghuut
Asiyekuwakufurisha washirikina ina maana ya kwamba hakukufuru Twaaghuut. Kwa msemo mwingine ni kwamba amekiri shirki. Mwenye kutilia shaka juu ya ukafiri wa mayahudi na manaswara au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi hakukufuru Twaaghuut. Hivyo basi hawi muumini.
Kwa hiyo dalili juu ya kwamba asiyewakufurisha washirikina au akatilia shaka ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi ni kalima ya Tawhiyd "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" kwa sababu hakukufuru Twaaghuut.
Vilevile Allaah (Ta´ala) amesema:
َٰ َى ثْـق ُ الْو ِ ة َ و ْ ر ُ الْع ِ َك ب َ ْس َم ت ْ اس ِ َد َق فـ ِ ـه اللَّ ِ ن ب ِ م ْ ؤ ُ يـ َ ِت و اغُو الطَّ ِ ب ْ ُر ْكف َ ن ي َ َم ف "Basi atakayemkanusha twaaghuwt [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti." 02:256
Ambaye hawakufurishi washirikina au akatilia shaka ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi hakukufuru Twaaghuut na yule asiyekufuru Twaaghuut hakumuamini Allaah. Kama ambavyo yule asiyewakufurisha washirikina au akawa na shaka juu ya ukafiri wao au akaonelea kuwa madhehebu yao ni sahihi hakuhakikisha kalima ya Tawhiyd.
Kinyume chake ameitengua kalima ya Tawhiyd. Kitendo chake hichi kimeitengua kalima ya Tawhiyd ambayo ni "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah". Kwa sababu kalima ya Tawhiyd ndani yake mna kukufuru Twaaghuut na kumuamini Allaah.
Kama tulivyotangulia kusema ya kwamba Tawhiyd na imani havipatikani isipokuwa kwa mambo mawili; kukufuru Twaaghuut na kumuamini Allaah. Kwa ajili hiyo ndio maana kalima ya Tawhiyd ambayo ni "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" ndani yake mna ukanushaji na uthibitishaji.
NA ALLAAH ANAJUA ZAIDI
Tutaendeleaa....Usikose Sehemu ya 3 In Shaa Allaah...................
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2FIVbsZ
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni