Translate

Jumanne, 27 Novemba 2018

Tafswiyr-ul-Anaam bi Sharh Nawaaqidh-il-Islaam - Sehemu ya 5

                                        Tafswiyr-ul-Anaam bi Sharh Nawaaqidh-il-Islaam 

                              
                               Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy 


                                                   Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush



Tunaendeleaa..............................



17. Tisa: Anayeitakidi kuwa kuna yeyote ana haki ya kutoka katika Shari´ah ya Muhammad(Swallaah Allaahu Aleyhi wa Sallaam).


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mwenye kuitakidi kuwa kuna watu wana haki kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) - kama ambavyo Khidhr alivyopata kutoka katika Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam) - ni kafiri.


                                                                        MAELEZO 


Mwenye kuitakidi kuwa kuna yeyote anaweza kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama jinsi Khidhr alivyopata kutoka katika Shari´ah ya Muusa, ni kafiri. Dalili ya hilo ni maneno Yake (Ta´ala):


 ْ ِغ َغيـ َ ت ْ ب َ ن يـ َ م َ و َ ِرين اسِ ا ْْلَ َ ن ِ م ةِ َ ر ِِف اْْلخِ َ و ُ ه َ و ُ ْه ن ِ م َ ل َ ب ْ ق ُ َن يـ ل َ ا فـ ً ين ِ د َالمِ ْ اْإلِس َ ر

"Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake; naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika."03:85


Anayeitakidi kuwa kuna ambaye anaweza kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama jinsi Khidhr alivyopata kutoka katika Shari´ah ya Muusa ni kafiri.


Hilo ni kwa sababu Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) imeenea kwa viumbe wote wawili; majini na wanaadamu, waarabu na wasiokuwa waarabu. Jengine ni kwamba Shari´ah ya Mtume wetu Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndio ya mwisho kabisa na yenye kufuta Shari´ah nyinginezo zote.

Allaah (Ta´ala) amesema:


 ا ً ير ِ َذ َني ن الَمِ َ ْلع ِ ُكوَن ل َ ي ِ ل ِ ه ِ د ْ ب َ َٰ ع َى ل َ َن ع ا َ ق ْ ُر ََّزَل الْف ي نـ ِ َك الَّذ َ ار َ ب َ تـ


"Amebarikika Yule Ambaye Ameteremsha Pambanuzi kwa mja Wake ili awe muonyaji kwa walimwengu." 25:01


ًَل ُ س َ لنَّا ِس ر ِ ا َك ل َ ْلن َ ْس أَر َ ً و ۖ ا َشِهيد ِ ـه اللَّ ِ ب َٰ َى َكف َ و

"Na Tumekutuma kwa watu uwe Mtume na inatosheleza Allaah kuwa ni Mwenye kushuhudia yote."39


 ا ً يع ََجِ ْ ُكم ْ لَي ِ إ ِ ـه وُل اللَّ ُ س َ ر ِِِنِّ إ ُ ا النَّاس َ ه ُّ ا أَيـ َ ي ْ ُل ق


"Sema: “Hakika mimi ni Mtume wa Allaah kwenu nyinyi nyote"." 07:158


Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

 "Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, hakuna yeyote katika Ummah huu atayesikia kuhusu mimi - sawa we ni myahudi au mnaswara - halafu asiniamini isipokuwa ataingia Motoni."Muslim (153)

"Nimepewa vitano ambavyo hakupewa Mtume yoyote kabla yangu." Moja wapo akataja: "Nabii alikuwa anatumwa kwa watu wake maalum na mimi nimetumwa kwa watu wote."al-Bukhaariy (335) na (438) na Muslim (521)


Mwenye kuitakidi kuwa inajuzu kwa yeyote kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamuabudu Allaah kwa Shari´ah nyingine ni kafiri. Kwa sababu Shari´ah ya Muhammad ni yenye kuenea; kwa majini na wanaadamu, waarabu na wasiokuwa waarabu. Jengine ni kwa sababu Shari´ah yake imefuta Shari´ah nyinginezo zote.


Vilevile ni kwa sababu baada ya kutumwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Shari´ah yake ni yenye kumgusa kila aliyepo [katika ulimwengu huu] mpaka siku ya Qiyaamah. Hili ni tofauti na Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam). Shari´ah yake haikuwa ni yenye kuenea kwa watu wote. Shari´ah yake  ilikuwa inawahusu tu wana wa Israa´iyl. Kwa ajili hii ndio maana Khidhr alipata kutoka katika Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam).


Jengine ni kwa sababu maoni ambayo ni sahihi ni kwamba Khidhr ni Nabii anayeteremshiwa Wahyi. Ndio maana Muusa akaja kujifunza kwake, kama jinsi Allaah alivyotuelezea hilo katika Suurah al-Kahf na katika Hadiyth Swahiyh iliyopokelewa na al-Bukhaariy  (74), (78) na (2267) na Muslim (2380).Kwa hiyo Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam) haimlazimu Khidhr na yeye sio katika wana wa Israa´iyl. Yeye ni mwenye kutoka katika Shari´ah ya Muusa.



18. Sababu ya Khidhr kutofuata Shari´ah ya Muusa.


Anayedai kuwa inajuzu kutoka katika Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama ilivyojuzu kwa Khidhr kutoka katika Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam) ni kafiri. Kwa sababu mbili zifuatazo ;


Ya kwanza: Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa walimwengu wote na wakati Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam) ni kwa watu maalum. Kwa hiyo Shari´ah ya Muusa (´alayhis-Salaam) haimlazimu Khidhr. Ama sisi Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kutulazimu.


Ya pili: Maoni sahihi ni kwamba Khidhr ni Nabii anayeteremshiwa Wahyi. Yeye anafuata Shari´ah yake kama ambavyo Muusa pia na yeye anafuata Shari´ah yake.


Mwenye kuamini kuwa ana haki yeye au mwingine ya kutofuata Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuabudu Allaah kwa mfumo mwingine isiyokuwa Shari´ah aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kafiri kwa maafikiano ya waislamu.


Kwa sababu Shari´ah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni yenye kuenea kwa viumbe viwili; majini na watu. Jengine ni kwa sababu hakushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah.


Yule mwenye kusema kuwa Shari´ah ya Muhammad au utume Wake ni kwa watu maalum peke yao au akasema kuwa kuna Mtume mwingine baada yake basi atakuwa hakushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah na hivyo anakuwa kafiri.


Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:


"Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, hakuna yeyote katika Ummah huu atayesikia kuhusu mimi - sawa we ni myahudi au mnaswara - halafu asiniamini isipokuwa ataingia Motoni." 



19. Kumi: Kuipuuza dini ya Allaah kwa kutojifunza nayo wala kuitendea kazi.



Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kuipuuza dini ya Allaah (Ta´ala), hajifunzi nayo na wala haitendei kazi. 

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):


 ا َ ْه نـ َ َ َض ع ْر ُُثَّ أَع ِ ه ِّ بِ َ ِت ر ا َ آي ِ ب َ ِّر َّن ذُكِ ِ َم ُ َم أَظْل ْ ن َ م َ و ۖ وَن ُ م ِ ق َ نت ُ َني م ِ ِرم ْ ُج الْم َ ن ِ نَّا م ِ إ


"Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayaat za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu."32:22


                                                                  MAELEZO 


Kuipuuza dini ya Allaah kwa njia ya kwamba mtu akawa hajifunzi nayo na wala hamuabudu Allaah. Hiki ni kitenguzi miongoni mwa mambo yanayotengua Uislamu. Mwenye kukengeuka dini ya Allaah (´Azza wa Jall) hajifunzi nayo wala hamuabudu Allaah ni kafiri. Katika hali hii atakuwa ni mwenye kumuabudu shaytwaan.


Haya ndio yale baadhi ya watu wanaita kuwa ni "mpagani". Mtu asiyejifunza dini, hamuabudu Allaah na wala haitendei kazi. Huyu ni mwenye kumuabudu shaytwaan kwa sababu yeye ndiye ambaye amemuamrisha hilo. Kwa hiyo huyu anakuwa ni mwenye kumuabudu shaytwaan. Hakuna yeyote duniani isipokuwa kuna anayemuabudu.


Muabudu mzimu ana anachokiabudu. Mayahudi wana wanachokiabudu. Manaswara wana wanachokiabudu. Muislamu wanamuabudu Allaah. Asiyekuwa muislamu anamuabudu shaytwaan. Asiyemuabudu Allaah anamuabudu shaytwaan.


Huyu anayedai kuwa hajifunzi dini na hamuabudu Allaah anamtii shaytwaan na ni mja wa shaytwaan. Yeye ndiye ambaye amemuamrisha kufanya hilo na hivyo anakuwa ni mja wake. Mwenye kuipa mgongo dini ya Allaah akawa hajifunzi dini ya Allaah na wala hamuabudu Allaah kabisa; si kwa kumuomba  du´aa, swalah, kupenda, maneno, kuamini pamoja na kuamini kuwa Allaah ndiye Muumbaji, Mruzukaji, Mwenye kuyaendesha mambo na kwamba Yeye ndiye muabudiwa wa haki, hajifunzi dini na wala hamuabudu Allaah ni kafiri.


Ni kafiri kwa kukengeuka kwake. Kwa hiyo kile kitendo chenyewe cha kukengeuka ni ukafiri. Miongoni mwa dalili ya hilo ni maneno ya Allaah (Ta´ala):


: ا َ ْه نـ َ َ َض ع ْر ُُثَّ أَع ِ ه ِّ بِ َ ِت ر ا َ آي ِ ب َ ِّر َّن ذُكِ ِ َم ُ َم أَظْل ْ ن َ م َ و ۖ وَن ُ م ِ ق َ نت ُ َني م ِ ِرم ْ ُج الْم َ ن ِ نَّا م ِ إ


"Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayaat za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu." 32:22


 أَ ْ ن َ م َ و ُ اه َ د َ َ ْت ي َّدم َ ا ق َ م َ ي َسِ ن َ ا و َ ْه نـ َ َ َض ع ْر أَع َ ف ِ ه ِّ بِ َ ِت ر ا َ آي ِ ب َ ِّر َّن ذُكِ ِ َم ُ َم ظْل


"Na Nani dhalimu zaidi kuliko yule aliyekumbushwa Aayaat za Mola wake, akazipuuza na akayasahu yale iliyotanguliza mikono yake." 18:57


 وا ُ ر ِ َ َّما أُنذ وا ع ُ َر َكف َ ين ِ الَّذ َ ُض و وَن ِر ْ ع ُ م


"Na wale waliokufuru kwa yale wanayoonywa kwayo ni wenye kupuuza."46:03


Makafiri wanakengeuka bi maa wanapuuza juu ya na kumuamini Allaah na Mtume Wake na kuitendea kazi dini hii. Amesema (Subhaanah):

 ِّ بِ َ ِت ر ا َ آي ِ ب َ ِّر َّن ذُكِ ِ َم ُ َم أَظْل ْ ن َ م َ و ا َ ْه نـ َ َ َض ع ْر ُُثَّ أَع وَن ه ۖ ِ ُ م ِ ق َ نت ُ َني م ِ ِرم ْ ُج الْم َ ن ِ نَّا م ِ إ

"Na nani dhalimu zaidi kuliko yule anayekumbushwa Aayaat za Mola wake, kisha akakengeuka nazo? Hakika Sisi Tutawalipiza wahalifu."


Kwa hivyo yule mwenye kuipuuza dini ya Allaah kwa njia ya kwamba akawa hajifunzi nayo na wala hamuabudu Allaah ni kafiri. Mtu kama huyu baadhi ya watu wanamwita kuwa ni mkanaMungu. Lakini uhalisia ni kwamba anamuabudu shaytwaan. Hakuna asiyeabudu kitu. Hakuna kiumbe chochote isipokuwa kuna kinachoabudu. Asiyemuabudu Allaah anamuabudu shaytwaan.




                                                               20. Hitimisho



Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:


Hakuna tofauti katika mambo yote haya yanayotengua Uislamu kati ya mwenye kufanya mzaha ya mwenye kukusudia na mwenye kuogopa. Isipokuwa tu yule aliyetenzwa nguvu. Yote haya ni katika [mambo] makubwa ambayo yanakuwa ni yenye khatari na mara nyingi hutokea. Hivyo basi, inatakikana kwa muislamu kutahadhari nayo na ayaogope juu ya nafsi yake. Tunajikinga kwa Allaah kwa yanayopelekea katika khasiria Zake na adhabu Yake kali. Swalah na salaam zimwendee kiumbe Chake bora Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake. 


                                                                 MAELEZO 


Mwandishi ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy  (Rahimahu Allaah) anasema kuwa hakuna tofauti katika mambo haya yanayovunja Uislamu kati ya anayefanya mzaha, mwenye kukusudia kweli na mwenye kuogopa. Isipokuwa tu mtenzwa nguvu. Vitenguzi hivi ndiyo vya khatari sana na vinavyotokea kwa wingi kwa watu. Inampasa mtu atahadhari navyo kwa sababu watu wengi hutumbukia ndani yake. Jengine ni kwa sababu khatari yake ni kubwa. Tunajilinda kwa Allaah kwa yanayopelekea katika khasiria Zake na adhabu Yake kali.


Mwandishi ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy (Rahimahu Allaah) amesema kuwa hakuna tofauti kati ya anayefanya mzaha, mwenye kukusudia kweli na mwenye kuogopa. Isipokuwa tu mtenzwa nguvu. Kwa hivyo hapa kuna hali mbali mbali:


1- Mtu amefanya moja katika vitenguzi vya Uislamu hali ya kuwa anafanya mzaha. Kama mtu anayefanyia mzaha swalah au dini kwa njia ya maskhara. Huyu anakufuru.


2- Mwingine amefanya moja katika vitenguzi vya Uislamu hali ya kuwa ni mwenye kumaanisha kweli. Kama mfano wa anayefanya mzaha na dini hali ya kuwa ni mwenye kumaanisha kweli. Huyu anakufuru.

3- Mwenye kufanya moja katika vitenguzi vya Uislamu kwa kuchelea juu ya nafsi yake, mali yake au mtoto wake. Huyu anakufuru hata kama atakuwa ni mwenye kuogopa. Kama mfano wa mwenye kuutukana Uislamu mbele ya mtu ili mali yake iweze kubaki na isichukuliwe. Kwa sababu anachelea ikiwa hatotukana Uislamu mali yake itachukuliwa. Lau atachelea mali yake, nafsi yake au mtoto wake anakufuru.

4- Mwenye kukirihishwa hali ya kuwa moyo wake umetua kwenye ukafiri anakufuru. Kwa mfano mtu ambaye amewekwa upanga shingoni mwake na kuambiwa ima ukufuru la sivyo tunakuua. Mtu ambaye yuko katika hali kama hii akitamka neno la kufuru na wakati huo huo moyo wake umetua katika imani hakufuru. Ama endapo atawekwa upanga shingoni mwake na akatamka neno la kufuru hali ya kuwa ni mwenye kuazimia ukafiri na wakati huo huo moyo wake ni wenye kutua katika ukafiri anakufuru.


Kwa hivyo mwenye kufanya moja katika mambo haya yanayotengua Uislamu hali ya kuwa ni mwenye kufanya mzaha, anamaanisha kweli au ni mwenye kuogopa anakufuru. Isipokuwa yule mwenye kutenzwa nguvu. Akikufuru pamoja na kuwa anachukia hilo na kwa sharti moyo wake uwe umetua juu ya imani [hakufuru]. Kwa kufupisha ni kwamba hapa tuna hali tano:


Ya kwanza: Kuhusu yule mwenye kufanya kufuru au moja katika yanayotengua Uislamu ilihali ni mwenye kufanya mzaha anakufuru.


Ya pili: Kuhusu anayefanya kufuru au moja katika yanayotengua Uislamu hali ya kuwa ni mwenye kumaanisha kweli anakufuru.


Ya tatu: Mwenye kufanya kufuru kwa kuogopa anakufuru.


Ya nne: Mwenye kufanya kufuru kwa kutenzwa nguvu na wakati huo huo moyo wake umetua juu ya ukafiri - kwa maana ya kwamba alipokirihishwa ndipo akaazimia ukafiri - anakufuru.


Ya tano: Mwenye kufanya kufuru kwa kutenzwa nguvu na wakati huo huo moyo wake umetua katika imani hakufuru.


Kwa hiyo hizi ni hali tano. Hali nne ambapo mtu anakufuru na moja hakufuru. Dalili yenye kuonesha kuwa anayechelea juu ya nafsi yake, familia yake au mali yake ikamfanya yeye kutamka maneno ya kufuru hata na yeye pia anakuwa kafiri ni maneno Yake (Ta´ala):

نِ َ اْإلَِي ِ ن ب ٌّ ِ ئ َ طْم ُ م ُ ه ُ َْلب قـ َ و َ ْكِره أُ ْ ن َ ََِّل م إ ِ ه ِ ان َ َي ِ إ ِ ْد ع َ ن بـ ِ م ِ ـه اللَّ ِ ب َ َر ن َكف َ م

"Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake [atapata adhabu] isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya iymaan."


Hapa tunapata kuona kuwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amevua hali moja peke yake; naye ni yule mwenye kutenzwa nguvu kwa sharti kwa sharti ya kwamba moyo wake uwe umetua katika imani:

 انِ َ اْإلَِي ِ ن ب ٌّ ِ ئ َ طْم ُ م ُ ه ُ َْلب قـ َ و َ ْكِره أُ ْ ن َ ََِّل م إ

"... isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya iymaan."


Baada ya hapo Allaah (Subhaanah) akasema:


 ِ ب َ َح َشر ن َّمن َٰكِ لَـ َ و انِ َ اْإلَِي ِ ن ب ٌّ ِ ئ َ طْم ُ م ُ ه ُ َْلب قـ َ و َ ْكِره أُ ْ ن َ ََِّل م إ ِ ه ِ ان َ َي ِ إ ِ ْد ع َ ن بـ ِ م ِ ـه اللَّ ِ ب َ َر ن َكف َ ٌٌ م َض َغ ْ ِهم ْ َي ل َ َع ا فـ ً َ ْدر ِر ص ْ الْ ُكف ٌ يم َظِ ٌب ع َذا َ ع ْ ُم ََّل َ و ِ ـه اللَّ َ ِّن ِ م ةِ َ ر َى اْْلخِ ل َ ا ع َ ي ْ دنـ َ ال ُّ اة َ ي َ وا ا ْْل ُّ ب َ َح ت ْ اس ُ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ


"Atakayemkufuru Allaah baada ya kuamini kwake [atapata adhabu] isipokuwa yule aliyetenzwa nguvu na huku moyo wake umetua juu ya iymaan. Lakini aliyekifungulia ukafiri kifua chake, basi hao juu yao ni ghadhabu kutoka kwa Allaah na watapata adhabu kuu. Hivyo kwa sababu wao wamependelea uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah."16:106-107


Mwenye kukufuru kwa sababu ya mali yake, familia yake au mali yake amependelea dunia juu ya Aakhirah, ameitanguliza dunia mbele kabla ya Aakhirah, ameitanguliza dunia mbele juu ya dini


: ةِ َ ر َى اْْلخِ ل َ ا ع َ ي ْ دنـ َ ال ُّ اة َ ي َ وا ا ْْل ُّ ب َ َح ت ْ اس ُ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ


"Hivyo kwa sababu wao wamependelea uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah."


Akifanya ukafiri kwa kuchelea familia yake, mali yake au juu ya nafsi yake anakufuru. Hapewi udhuru kwa kuchelea kwake. Allaah (Ta´ala) amesema:


ةِ َ ر َى اْْلخِ ل َ ا ع َ ي ْ دنـ َ ال ُّ اة َ ي َ وا ا ْْل ُّ ب َ َح ت ْ اس ُ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ

"Hivyo kwa sababu wao wamependelea uhai wa dunia kuliko wa Aakhirah."


Hali kadhalika akifanya ukafiri kwa kufanya mzaha, kwa kukusudia kweli au kwa kutenzwa nguvu lakini moyo wake ukawa ni wenye kutua katika ukafiri. Hakuna anayevuliwa isipokuwa yule aliyelazimishwa na wakati huo huo moyo wake umetua katika imani.


Makusudio ya "kutenzwa nguvu" haina maana ya vitisho. Maana yake ni mtu akakirihishwa na kulazimishwa kwa njia ya kwamba akatiwa upanga juu ya shingo yake au akatishwa na mtu ambaye ni muuaji na anajua kuwa kweli huyu ni mwenye kutimiza ahadi yake papo hapo endapo sintokufuru. Huyu ndiye mtenzwa nguvu tunayekusudia. Ikiwa atatamka au kufanya kitendo cha ukafiri na huku moyo wake umetua katika imani haitomdhuru kitu. Ama mtu kuogopa peke yake juu ya nafsi yake, familia yake au mali yake halimjuzishii kukufuru.


Tunamuomba Allaah (´Azza wa Jall) usalama na afya na atufishe juu ya Uislamu. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na kufuru, shirki, unafiki, majanga na tabia ovu. Tunamuomba Allaah atuthibitishe katika dini Yake na atukinge na mitihani yenye kupotosha, atufishe katika Uislamu hali ya kuwa si wenye kugeuza wala kubadilisha. Hakika Yeye ndiye msimamizi na muweza wa hilo.


Swalah na salaam zimwendee mja na Mtume Wake Mtume wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na Taabi´uun.




                                                                  MWISHO


from fisabilillaah.com https://ift.tt/2r6gN8A
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...