Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Tunaendelea.....................
15. Saba: Mwenye kufanya, kujifunza, kufunza au kuridhia uchawi.
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Uchawi. Unajumuisha Swarf na ´Atwf. Atakayeufanya au akawa radhi nao anakufuru.
Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):
ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن ُوََل إ ق َ يـ ََّّتَٰ َ ح د َ أَح ْ ن ِ م انِ َ ِّم ِ ل َ ع ُ ا يـ َ م َ و
"Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi].”02:102
MAELEZO
Maana ya uchawi kilugha ni ibara ya kitu kimechojificha na ikakosekana sababu yake.
Maana ya uchawi Kishari´ah ni ibara ya kuzingua na vifundo na madawa. Unaathiri kwenye mioyo na miili. Unapiga na kuua. Unafarikanisha baina ya mtu na mkewe.
Uchawi umeitwa uchawi kwa sababu mchawi anaathiri kwa kujificha. Mchawi anafanya uzinguzi na vifundo ambavyo vinaathiri kwa kujificha kwenye mioyo na miili.
Uchawi unaweza kuathiri kwa maradhi, kwa kuua na kwa kufarikanisha baina ya wanandoa. Mchawi ambaye ana uhusiano na mashaytwaan ni lazima atumbukie katika shirki. Ni aina moja wapo ya shirki.
Kwa sababu mchawi ambaye ana mafungamano na mashaytwaan ni lazima baina yao wawe na kubadilishana huduma; ni lazima kuwepo mikataba. Jini anafunga mkataba na mchawi na hivyo mtu ambaye ni mchawi anakuwa ni mwenye kukufuru kutokana na yale yanayopelekea katika mkataba huu.
Mtu huyu hujikurubisha kwake kwa kufanya mambo ya ushirikina ambayo anamtaka kufanya. Kwa mfano jini linaweza kumuomba amchinjie, auweke msahafu kwenye najisi, aukojolee au ajikurubishe kwake kwa kufanya mambo mengine ambayo ni ya shirki.
Kwa hiyo pale ambapo mchawi huyo atafanya shirki ndipo jini atamhudumikia kwa kile anachokitaka; akimuamrisha amkate mtu amkata, amuue mtu amuua, amletee maelezo fulani na mengineyo.
Kwa hiyo uchawi ni shirki. Atakayefanya uchawi, kujifunza nao, kuufunza au akawa radhi nao amekufuru. Mwenye kuridhia ni kama mtendaji. Yule mwenye kuridhia shirki ni mshirikina.
Dalili ni manneo ya Allaah (Ta´ala) kuhusu kisa cha Malaika wawili ambao waliteremshwa ardhini na kuwapa watu mtihani:
ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن ُوََل إ ق َ يـ ََّّتَٰ َ ح د َ أَح ْ ن ِ م انِ َ ِّم ِ ل َ ع ُ ا يـ َ م َ و
"Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]".”
Anapowajia mtu na kuwaomba wamfunze uchawi humnasihi na kumkataza kwa makemeo makali na huku wanamwambia:
ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن إ
“Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi].”
Aking´ang´ania ndipo wanamfunza.
Vilevile maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):
َ ر ْ ِّح السِ َ وَن النَّاس ُ ِّم ِ ل َ ع ُ وا يـ ُ َر َني َكف اطِ َ َّن ال َّشي َٰكِ لَـ َ ُن و ا َ م ْ َي ل ُ س َ َر َكف ا َ م َ و
"Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu uchawi." 02:102
Wamekufuru kwa kile kitendo chao cha kuwafunza watu uchawi. Uchawi ni kufuru na kuritadi. Yule mwenye kufanya uchawi na kuuridhia ni kafiri.
Vilevile kunaingia Swarf na ´Atwf.
Swarf maana yake ni kumkimbiza mtu mke wake au mke na mume wake. Hilo linatendeka kwa njia ya kwamba mtu akija kwa mke wake anamuona kwa umbile baya na matokeo yake anamkimbia na anakuwa hataki kumjongelea. Au kinyume chake yeye akawa anamchukia mume wake kwa njia ya kwamba anapomuona mume wake basi humuona kwa umbile baya asiloweza stahamili hata kumwangalia.
Hivyo kunatokea mtengano baina yao. Hii ndio Swarf. Mchawi amefanya wanakuwa ni wenye kukimbiana pamoja na kuwa uhakika wa mambo hakuna kitu kwa wote wawili.
Kilichopo ni kwamba mchawi amewafanyia uchawi kwa njia ya kwamba amemfanya mwanamke amuone mume wake katika umbile baya kwa kiasi cha kushindwa hata kumwangalia.
Hali kadhalika amfanye mume katika umbile baya kwa njia ya kwamba mke wake akimtazama hastahamili kumwangalia. Hiyo inakuwa ni sababu ya kupatikana kufarikiana.
´Atwf ni kinyume cha Swarf. Mchawi anampendekeza mwanamke kwa mume kwa njia ya kwamba anamfanyia uchawi mwanaume na anakuwa ni mwenye kumili kwa mwanamke. Anampendekeza mbele ya macho yake ijapokuwa atakuwa ni mbaya na mwenye umbile baya. Pamoja na hivyo mbele ya macho yake hakuna mzuri amuonae kama yeye.
Vilevile mchawi akimfanyia uchawi mwanamke kwa hali ya kwamba pale anapomtazama mume wake hakuna mzuri amuonae kama yeye ijapokuwa atakuwa mbaya na mwenye maumbile mabaya. Hii ndio inaitwa ´Atwf. Amempendekeza kwake. Hii ni aina moja wapo ya uchawi.
Miongoni mwa uchawi kunaingia vilevile at-Tiwalah.
At-Tiwalah Ni kitu au dawa inayofanywa na mchawi kisha wanampa mume au mke ambacho wanadai kuwa inampendekeza mwanamke kwa mumewe na mwanaume kwa mkewe. Yule mwenye kufanya au akawa radhi na uchawi anakuwa kafiri kwa dalili ya Qur-aan.
Amesema (Ta´ala):
ْنيِ َ َك ل َ َى الْم ل َ ا أُنِزَل ع َ م َ و َ ر ْ ِّح السِ َ وَن النَّاس ُ ِّم ِ ل َ ع ُ وا يـ ُ َر َني َكف اطِ َ َّن ال َّشي َٰكِ لَـ َ ُن و ا َ م ْ َي ل ُ س َ َر َكف ا َ م َ َت و و ُ ار َ م َ َت و و ُ ار َ ه َ ِل اب َ ب ِ ۖ ب ََّّتَٰ َ ح د َ أَح ْ ن ِ م انِ َ ِّم ِ ل َ ع ُ ا يـ َ م َ و ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن ُوََل إ ق َ يـ
"Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili [katika mji wa] Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]".”
Mwenye kufanya uchawi, akajifunza nao, akaufunza au akawa radhi nao - ikiwa ni pamoja vilevile na Swarf na ´Atwf - anakuwa kafiri kwa kuwa amemshirikisha Allaah (´Azza wa Jall).
Dalili ni Aayah zifuatazo:
ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن ُوََل إ ق َ يـ ََّّتَٰ َ ح د َ أَح ْ ن ِ م انِ َ ِّم ِ ل َ ع ُ ا يـ َ م َ و
"Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi]"
.” ُ ق ِّ ِر َ ف ُ ا يـ َ ا م َ م ُ ْه نـ ِ وَن م ُ لَّم َ ع َ تـ َ ي َ فـ ِ ه ْجِ َو ز َ و ِ ء ْ ر َ َْ َني الْم بـ ِ ه ِ وَن ب
"Basi wakajifunza kutoka kwa hao [Malaika] wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe."
َى ل َ ا أُنِزَل ع َ م َ و َ ر ْ ِّح السِ َ وَن النَّاس ُ ِّم ِ ل َ ع ُ وا يـ ُ َر َني َكف اطِ َ َّن ال َّشي َٰكِ لَـ َ ُن و ا َ م ْ َي ل ُ س َ َر َكف ا َ م َ َت و و ُ ار َ م َ َت و و ُ ار َ ه َ ِل اب َ ب ِ ب ْنيِ َ َك ل َ ۖ الْم ََّّتَٰ َ ح د َ أَح ْ ن ِ م انِ َ ِّم ِ ل َ ع ُ ا يـ َ م َ و ْ ُر ْكف َ ََال ت ٌ ف ة َ ن ْ تـ ِ ف ُ ََِّّنَا َْنْن ُوََل إ ق َ يـ
"Na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili [katika mji wa] Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Na [hao Malaika wawili] hawamfundishi yeyote mpaka wamueleze: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru [kwa kufanya uchawi].” 02:102
Lakini pamoja na hivyo mchawi hawezi kumdhuru yeyote isipokuwa pale ambapo Allaah (´Azza wa Jall) atakadiria dhara hilo kwa mtu huyo. Hapo ndipo madhara yatapatikana.
Amesema (Ta´ala):
ِ ـه اللَّ ْذنِ ِ إ ِ ََِّل ب إ د َ أَح ْ ن ِ م ِ ه ِ ب َ ين ِّ َضاِر ِ ُم ب ا ه َ م َ و
"Na wao si wenye kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah." 02:102
16. Nane: Kuwasaidia washirikina dhidi ya waislamu.
Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Kuwasaidia washirikina [makafiri] dhidi ya waislamu.
Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):
ْ م ُ ْه نـ ِ م ُ نَّه ِ إ َ ف ْ ن ُكم ِّ ِ ُم م ََّّل َ َو تـ َ ن يـ َ م َ ۖ َني و مِ ِ ال الظَّ َ م ْ َو ي الْق ِ ْد ه َ ََل يـ َ ـه َّن اللَّ ِ إ
"Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu." 05:51
MAELEZO
Muislamu akawasaidia makafiri dhidi ya waislamu. Kwa mfano kama kuna vita baina ya waislamu na makafiri halafu akawasaidia na kuwasapoti makafiri hawa katika kuwapiga vita waislamu. Ni mamoja akawasaidia kwa mali, silaha au kwa kuwapa maoni. Akiwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ili waweze kupata njama anakuwa kafiri.
Kwa sababu amewafadhilisha makafiri juu ya waislamu. Ufadhilishaji huu unalazimisha kuwa anauchukia Uislamu, Allaah na Mtume Wake. Yule mwenye kumchukia Allaah (´Azza wa Jall), Mtume Wake au kitu katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anakuwa kafiri.
Amesema (Ta´ala):
ْ ُم اََّل َ ْم َط أَع َ ب ْ أَح َ ف ُ ـه َل اللَّ َ ا أَنز َ وا م ُ َكِره ْ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ
"Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale Aliyoyateremsha Allaah, basi Akayaporomosha matendo yao."47:09
Asiyempenda Allaah na Mtume Wake ni kafiri.
Msingi wa mapenzi ni lazima upatikane. Lakini kuhusu ukamilifu, kwa msemo mwingine kile kitendo cha mtu kutanguliza mapenzi ya kumpenda Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya mke, watoto na mali, huu ndio ukamilifu tunaokusudia.
Mwenye kutanguliza kitu katika mali, mke au kitu kingine juu ya mapenzi ya kumpenda Allaah na Mtume Wake anakuwa ni mtenda dhambi aliye na imani pungufu. Lakini asipompenda Allaah na Mtume Wake anakuwa kafiri. Anayewasaidia makafiri dhidi ya waislamu hampendi Allaah na Mtume Wake. Kinyume chake ni mwenye kuwachukia na kuchukia yale Aliyoteremsha.
Hivyo anaingia katika maneno Yake (Ta´ala):
ْ ُم اََّل َ ْم َط أَع َ ب ْ أَح َ ف ُ ـه َل اللَّ َ ا أَنز َ وا م ُ َكِره ْ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ
"Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale Aliyoyateremsha Allaah, basi Akayaporomosha matendo yao."47:09
Dalili nyingine maalum yenye kuonesha kuwa kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni ukafiri ni Aayah hii Tukufu katika Suurah al-Maaidah:
َ اء َ ي ِ ل ْ َٰى أَو َ ار َ النَّص َ و َ ود ُ ه َ ُذوا الْيـ تَّخِ َ ََل تـ ُوا ن َ آم َ ين ِ ا الَّذ َ ه ُّ ا أَيـ َ ۖ ي بـ ض َ ْ ع َ بـ ُ اء َ ي ِ ل ْ أَو ْ م ُ ع ۖ ْ ُضه ْ م ُ ْه نـ ِ م ُ نَّه ِ إ َ ف ْ ن ُكم ِّ ِ ُم م ََّّل َ َو تـ َ ن يـ َ م َ و
"Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni marafiki - wao kwa wao ni marafiki. Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu."05:51
Tawallin ni kuwapenda washirikina. Kitendo hichi ni ukafiri na kuritadi. Kuwasaidia kwake makafiri dhidi ya wailsamu kunatokamana na mapenzi haya. Kwa hiyo yule mwenye kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni dalili tosha ya kwamba anawapenda makafiri kitendo ambacho ni kuritadi.
Tofauti kati ya Tawallin na Muwaalaah
Kufanya Tawallin na makafiri ni kuritadi. Kuhusu kufanya Muwaalaah na wao, kwa msemo mwingine kuwapenda, kutangamana nao na kuwa na urafiki nao ni dhambi kubwa. Msingi wa Tawallin ni kuwa na mapenzi ndani ya moyo. Mapenzi haya ndio yanazalisha kuwasapoti na kuwasaidia.
Kile kitendo chake cha kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu, sawa iwe kwa mali, silaha au maoni ni dalili tosha ya yeye kuwa na Tawallin kwa makafiri na kwamba anawapenda, jambo ambalo ni kuritadi kutokana na dalili ya Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:
َ اء َ ي ِ ل ْ َٰى أَو َ ار َ النَّص َ و َ ود ُ ه َ ُذوا الْيـ تَّخِ َ ََل تـ ُوا ن َ آم َ ين ِ ا الَّذ َ ه ُّ ا أَيـ َ ي
"Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni marafiki."
Bi maana usifanye nao Tawallin. َ
َ ار َ النَّص َ و َ ود ُ ه َ ُذوا الْيـ تَّخِ َ ََل تـ ُوا ن َ آم َ ين ِ ا الَّذ َ ه ُّ ا أَيـ َ ي َ اء َ ي ِ ل ْ ۖ ض َٰى أَو ْ ع َ بـ ُ اء َ ي ِ ل ْ أَو ْ م ُ ْ ُضه ع َ بـ
"Enyi mlioamini! Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni marafiki - wao kwa wao ni marafiki" 05:51
Makafiri ni wapenzi wao kwa wao.
ُم ََّّل َ َو تـ َ ن يـ َ م َ و
"Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao...
" Bi maana makafiri.
ْ م ُ ْه نـ ِ م ُ نَّه ِ إ َ ف ْ ن ُكم ِّ ِ م
"... katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao."
Bi maana muislamu ambaye atafanya Tawallin na makafiri basi yeye ni katika wao. Ni kafiri kama wao.
نَّ ِ إ َ ف ْ ن ُكم ِّ ِ ُم م ََّّل َ َو تـ َ ن يـ َ م َ و ْ م ُ ْه نـ ِ م ُ ۖ َني ه مِ ِ ال الظَّ َ م ْ َو ي الْق ِ ْد ه َ ََل يـ َ ـه َّن اللَّ ِ إ
"Na yeyote katika nyinyi atakayefanya urafiki nao; basi hakika yeye ni miongoni mwao. Hakika Allaah Haongoi watu madhalimu."
Kwa hivyo kuwasapoti na kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu ni kuritadi. Kwa sababu huku ni kufanya Tawallin na makafiri. Kufanya Tawallin na makafiri ni kuritadi kutoka katika Uislamu kwa dalili ya Qur-aan.
Tutaendelea.....Usikose Sehemu ya 5 In Shaa Allaah............
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2AqLZDV
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni