Translate

Jumanne, 27 Novemba 2018

Tafswiyr-ul-Anaam bi Sharh Nawaaqidh-il-Islaam - Sehemu ya 3

                                         Tafswiyr-ul-Anaam bi Sharh Nawaaqidh-il-Islaam 

                              Mwandishi: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy 



                                                   Tarjama: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush



Tunaendeleaa..............................



11. Haitoshelezi kwa mtu kumuabudu Allaah peke yake.


Lau mtu atasema kuwa Allaah ndiye muabudiwa na kwamba yeye anampwekesha na kumuabudu Allaah haina maana ya kwamba anakuwa muumini papo hapo. Hii sio Tawhiyd. Haitoshelezi kumuabudu Allaah peke yake. 

Bali ni lazima ukanushe ´ibaadah anayofanyiwa kila asiyekuwa Allaah. Kwa msemo mwingine ni kwamba ni lazima ulete ukanushaji na uthibitishaji. "Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" ndani yake mna ukanushaji na uthibitishaji. 



Ni lazima yapatikane mawili haya. "Hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" maana yake ni kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah. Ikiwa mtu atasema kuwa yeye anamuabudu Allaah peke yake ina maana ya kwamba anakuwa mpwekeshaji? Hapana. Haitoshelezi kule kumuabudu Allaah peke yake. 


Ni lazima kumuabudu Allaah sambamba na hilo ukanushe ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Huku ndio kukufuru Twaaghuut. Hili halipatikani isipokuwa kwa ukanushaji na uthibitishaji wa "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah". 

Kwa hivyo dalili ya kitenguzi hichi cha tatu ni Kauli ya Allaah (Ta´ala): 


 ا َ ََّل َ ام َ ِص َٰ ََل انف َى ثْـق ُ الْو ِ ة َ و ْ ر ُ الْع ِ َك ب َ ْس َم ت ْ اس ِ َد َق فـ ِ ـه اللَّ ِ ن ب ِ م ْ ؤ ُ يـ َ ِت و اغُو الطَّ ِ ب ْ ُر ْكف َ ن ي َ َم ف 

"Basi atakayemkanusha twaaghuwt [miungu ya uongo] na akamwamini Allaah kwa hakika atakuwa ameshikilia imara kishikilio madhubuti kisichovunjika."


Kalima ya Tawhiyd "hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah" ndani yake mna Takhliyah na Tahliyah. Nini maana yake? Takhliyah maana yake ni wewe ukanushe ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. Baada ya kukanusha na kukaripia ´ibaadah za kila chenye kuabudiwa badala ya Allaah ndipo kunakuja sasa Tahliyah na kumthibitishia ´ibaadah Allaah (´Azza wa Jall). 


Kwanza kunaanza na Takhliyah kisha ndio kunakuja Tahliyah. "Hakuna mungu wa haki... " hii ndio Takhliyah ikiwa na maana ya kwamba umekanusha ´ibaadah anazofanyiwa asiyekuwa Allaah. "... isipokuwa Allaah" hii ndio Tahliyah ikiwa na maana ya kwamba umemthibitishia ´ibaadah Allaah.


"Hakuna mungu wa haki... " huku ndio kukufuru Twaaghuut. "... isipokuwa Allaah" huku ndio kumuamuni Allaah.



12. Nne: Mwenye kuamini kuna uongofu au hukumu bora zaidi kuliko ya Mtume.


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: 

Mwenye kuamini kuwa kuna uongofu usiokuwa wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambao ni mkamilifu zaidi kuliko uongofu wake au kuna hukumu ya myingine asiyekuwa yeye ilio bora zaidi kuliko hukumu yake. Ni kama mfano wale wenye kufadhilisha hukumu za Twawaaghiyt juu ya hukumu yake. Huyo ni kafiri.



                                                                      MAELEZO 


Kitenguzi cha nne kinachotengua Uislamu ni kwamba yule mwenye kuamini kuwa kuna uongofu mkamilifu zaidi usiokuwa wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuna hukumu bora zaidi isiyokuwa hukumu yake amekufuru kwa maafikiano. Kwa mfano wale wenye kufadhilisha hukumu za Twawaaghiyt juu ya hukumu ya Allaah na Mtume Wake.


Mwenye kuitakidi kuwa kuna uongofu ulio mkamilifu zaidi kuliko wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au kuna hukumu ilio bora zaidi kuliko hukumu yake basi hakushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Hivyo kushuhudia kwake ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah kunabatilika. 


Kwa hiyo yule mwenye kuamini kuwa kuna uongofu bora zaidi kuliko wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au uko sawa sawa na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au ya kwamba kuna hukumu yenye kulingana na hukumu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufuru. 


Hali kadhalika ikiwa ataamini kuwa uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au hukumu yake ndio kamilifu zaidi, lakini hata hivyo akasema kuwa inajuzu kuwa na uongofu usiokuwa wa Mtume na kwamba inajuzu kuhukumiwa na isiyokuwa hukumu yake anakuwa kafiri. Kwa sababu atakuwa amehalalisha jambo ambalo kilazima linajulikana uharamu wake.


Haijuzu kuhukumiwa kwa kanuni hata kama utakuwa unaitakidi kuwa hukumu na Shari´ah ndio bora zaidi. Katika hali hii utakuwa umehalalisha jambo ambalo kilazima linajulikana kidini uharamu wake. Ni kama mfano wa mwenye kusema zinaa ni halali lakini hata hivyo mimi sizini au ribaa ni halali lakini sintotaamiliana na ribaa, huyu anakufuru. Kwa sababu ribaa ni haramu. Kule kuihalalisha ilihali ni jambo ambalo kilazima inajulikana kidini uharamu wake ni kufuru. 


Vilevile ikiwa atasema hukumu ya kanuni inajuzu pamoja na kuwa hukumu ya Shari´ah ni bora zaidi. Kule kuazimia hukumu ya kanuni ni kufuru na kuritadi. Kwa sababu umehalalisha jambo la haramu ambalo inajulikana kilazimi katika dini uharamu wake. Kuhukumu kwa kanuni ni haramu kwa maafikiano. Ni kama mfano wa zinaa ambayo ni haramu kwa maafikiano. Ni kama mfano vilevile wa ribaa ambayo ni haramu kwa maafikiano. 


Kwa hivyo yule mwenye kusema kuwa zinaa ni halali anakufuru. Mwenye kusema ribaa ni halali anakufuru. Mwenye kusema inajuzu kuhukumu kwa kanuni anakufuru. Haijalishi kitu hata kama atakuwa anaitakidi kuhukumu kwa Shari´ah ndio bora zaidi. 


Yule anayeamini kuwa kuna uongofu bora zaidi kuliko wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au wenye kulingana nao pamoja na kujuzisha kuchukua uongofu mwingine usiokuwa wake anakufuru. Hali kadhalika yule mwenye kuamini ya kwamba inajuzu kuhukumu kinyume na hukumu ya Allaah na Mtume Wake - sawa ikiwa ataamini kuwa hukumu ya Allaah ndio bora zaidi, iko chini zaidi au inalingana nayo - anakuwa kafiri. Si kwa jengine bali ni kwa sababu amehalalisha jambo ambalo inajulikana kilazimika katika dini uharamu wake.


Dalili ni kuwa hakushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah. Asiyeshuhudia ya kuwa Muhammad ni Mtume wa Allaah anakuwa kafiri. Kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah linahitajia kuhukumiwa na Shari´ah na kuitakidi kuwa haijuzu kuhukumiwa na isiyokuwa Shari´ah na vilevile kuamini kuwa haijuzu kufuata uongofu usiokuwa wa uongofu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).



13. Tano: Mwenye kuchukia jambo lolote la dini.  


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: 


Mwenye kuchukia kitu katika yale mambo aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kama atakifanya, anakufuru.


                                                                    
                                                                MAELEZO 


Ambaye anachukia kitu miongoni mwa yale mambo aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hata kama atakifanya, anakufuru. Kwa mfano Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekuja na Shari´ah ya swalah. Yule mwenye kuchukia swalah amekufuru. Kadhalika amekuja na Shari´ah ya zakaah na kuoa wake wengi. Mwenye kupinga hukumu hii ya Kishari´ah ambayo inahusu kuoa wake wengi anakufuru. 


Kwa ajili hii inawapaswa wanawake wafahamu kuwa haiwastahikii wao kuchukia kuoa wake wengi. Hii ni hukumu ya Allaah na Mtume Wake. Lakini hata hivyo ikiwa anachukia jambo hili na halipendi na akawa na chuki ya kimaumbile - na si kwamba anaichukia ile hukumu ya Kishari´ah - hilo halimdhuru. Au akachukia kwa vile baadhi ya wanaume hawafanyi uadilifu. 


Kwa msemo mwingine ni kwamba akawa ni mwenye kuchukia kuolelewa juu yake kwa sababu anachelea mwanaume huyu hatofanya uadilifu haina neno. 


Ama ikiwa anachukia ile hukumu ya Kishari´ah ambayo ni kuoa wake wengi huku ni kuritadi. Bi maana ikiwa anachukia chuki ambayo ni ya kubughudhi yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). 

Dalili ya hili ni maneno Yake (Ta´ala):

 أَ ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ ْ ُم اََّل َ ْم َط أَع َ ب ْ أَح َ ف ُ ـه َل اللَّ َ ا أَنز َ وا م ُ َكِره ْ م ُ نـَّه 

"Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale Aliyoyateremsha Allaah, basi Akayaporomosha matendo yao." 47:09


Mwenye kuchukia kitu chochote katika yale aliyoteremsha Allaah au yaliyoweka Allaah na Mtume Wake anakuwa kafiri. Akichukia uwekwaji wa swalah, zakaah, swawm, hajj au uoaji wa wake wengi - ni mamoja awe analichukia au kulibughudhi - anakuwa kafiri. Kwa sababu kitendo hicho kinapingana na imani. Kumpenda Allaah na Mtume Wake ni jambo la lazima. 


Asiyempenda Allaah na Mtume Wake ni kafiri. Ukamilifu wa mapenzi ni kutanguliza mapenzi ya kumpenda Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya kila kitu. Lakini ule msingi wa mapenzi ni lazima uwepo. Asiyempenda Allaah na Mtume Wake ni kafiri. 


Kwa hiyo yule mwenye kuchukia au kubughudhi kitu katika yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au katika yale yaliyokuja kutoka kwa Allaah katika Kitabu Chake au akamchukia Mtume Wake, anakuwa ni kafiri mwenye kuritadi. 


Allaah (´Azza wa Jall) amesema:


 ْ ُم اََّل َ ْم َط أَع َ ب ْ أَح َ ف ُ ـه َل اللَّ َ ا أَنز َ وا م ُ َكِره ْ م ُ أَنـَّه ِ َك ب ِ ل َٰ ذَ 

"Hivyo kwa kuwa wao wameyachukia yale Aliyoyateremsha Allaah, basi Akayaporomosha matendo yao." 47:09



14. Sita: Anayefanyia mzaha dini. 


Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema: Mwenye kufanyia mzaha kitu katika dini ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au thawabu na adhabu ya Allaah amekufuru. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):


 ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف وا ق ُ ر ِ َذ ت ْ َع ُوَن ََل تـ ِزئ ْ َه تـ ْ َس ت ْ ُم ُكنت ِ ه ِ ول ُ س َ ر َ و ِ ه ِ ات َ آي َ و ِ ـه اللَّ ِ أَب ْ ُل ق 

"Sema: "Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"." 09:65-66



                                                                   MAELEZO 


Yule ambaye anafanyia mzaha kitu miongoni mwa yale mambo aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au anayefanyia shere kitu katika dini ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), thawabu au adhabu yake amekufuru. 


Akifanyia mzaha swalah amekufuru. Akifanyia mzaha zakaah amekufuru. Akifanyia mzaha swawm amekufuru. Akiwafanyia mzaha waswalaji, kama kufanyia maskhara swalah ambayo wanaiswali waislamu, amekufuru. 


Kadhalika akifanyia mzaha ndevu kwa sababu ya kuchukia yale maamrisho yaliyoletwa na Uislamu juu ya kufuga ndevu anakufuru. Kwa sababu ni jambo limewekwa na Allaah kupitia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). 


Ama ikiwa anamfanyia mzaha mtu kwa dhati yake hakufuru. Hali kadhalika akifanyia mzaha Pepo na Moto na kwamba Pepo ni thawabu kwa waumini na Moto ni adhabu kwa makafiri na akasema mambo gani tena haya ya Pepo au Moto anakuru. 


Vilevile inahusiana na yule mwenye kufanyia mzaha thawabu za matendo mema, kwa mfano mtu mwenye kusikia au kusoma Hadiyth iliyosimuliwa na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

"Mwenye kusema "Subhaan Allaahi wa bi hamdih" kwa siku mara mia moja anafutiwa maasi yake hata kama itakuwa ni mfano wa povu la bahari." al-Bukhaariy (6405) na Muslim (2691).


Mtu akazifanyia thawabu hizi mzaha na maskhara - na si kwa sababu haonelei kuwa ni Swahiyh - anakufuru. Akifanyia mzaha kitu katika dini ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akafanyia mzaha thawabu ambazo Allaah amewaandalia wenye kutii au akafanyia mzaha thawabu ambazo Allaah ameziandaa kwa ajili ya matendo mema au kwa adhabu ambayo Allaah amewaandalia watenda maasi au amemuandalia kafiri, anakufuru. 


Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):


 ِ ول ُ س َ ر َ و ِ ه ِ ات َ آي َ و ِ ـه اللَّ ِ أَب ْ ُل ُوَن ق ِزئ ْ َه تـ ْ َس ت ْ ُم ُكنت ِ ه ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف وا ق ُ ر ِ َذ ت ْ َع ََل تـ 

"Sema: "Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"." 

Amewathibitishia ukafiri baada ya kuamini kwao. 


Aayah hii imewateremkia kundi fulani la Mujaahiduun katika vita vya Tabuk ambao walimfanyia mzaha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake wasomaji. Imepokelewa katika Hadiyth ya kwamba waliambizana kuwa hatujaona watu kama wasomaji wetu hawa; wana matumbo makubwa, ndimi zenye kusema uongo sana na ni waoga wakati wa mapambano. 


Bi maana hatujaona watu mfano wao kwa kula, kusema uongo sana na woga wakati wa kupigana vita na maadui. 


Wanamaanisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake wasomaji. ´Awf bin Maalik akawasikia walipokuwa wanazungumza ambapo akawaambia: 

"Umesema uongo. Wewe ni mnafiki. Nitamweleza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)." 


Akaja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kumweleza. Alipofika kwake akakuta Wahyi umeshamtangulia. Allaah akateremsha Aayah ifuatayo:

 ُوَن ِزئ ْ َه تـ ْ َس ت ْ ُم ُكنت ِ ه ِ ول ُ س َ ر َ و ِ ه ِ ات َ آي َ و ِ ـه اللَّ ِ أَب ْ ُل ق ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف وا ق ُ ر ِ َذ ت ْ َع ََل تـ 

"Sema: "Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"." 


Akaja mtu yule aliyezungumza maneno haya na kutaka kutoa udhuru kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku akisema: 

"Ee Mtume wa Allaah! Tulikuwa tunapiga porojo tu na kucheza." 


Bi maana hatufanya hivo kwa kukusudia. Tulizungumza vile kwa sababu tu ya kujifanyia usahali na safari. Kama jinsi baadhi yetu wanavyosema ya kwamba ni mazungumzo ya kufanya usahali sarafini. 


Anasema hivyo na huku Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazidishi mbali na kusoma Aayah ifuatayo: 

: ُوَن ِزئ ْ َه تـ ْ َس ت ْ ُم ُكنت ِ ه ِ ول ُ س َ ر َ و ِ ه ِ ات َ آي َ و ِ ـه اللَّ ِ أَب ْ ُل ق ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف وا ق ُ ر ِ َذ ت ْ َع ََل تـ 


"Sema: "Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"." 


Mtu huyo alikuwa ameshikilia kamba ya kipando cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni ile kamba inayokuwa imezunguka kwenye kiuno cha ngamia na huku miguu yake inaburuta kwenye ardhi na mawe yanapiga miguu yake na wakati huo huo huku anazidi kuomba udhuru. 

Lakini pamoja na hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hazidishi mbali na kumsomea Aayah hii:

 ُوَن ِزئ ْ َه تـ ْ َس ت ْ ُم ُكنت ِ ه ِ ول ُ س َ ر َ و ِ ه ِ ات َ آي َ و ِ ـه اللَّ ِ أَب ْ ُل ق ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف وا ق ُ ر ِ َذ ت ْ َع ََل تـ 

"Sema: "Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayaat Zake na Mtume Wake? Msitoe udhuru. Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"."


Allaah akawathibitishia ukafiri baada ya kuamini kwao pale aliposema:

 ْ ُكم ِ ان َ َي ِ إ َ ْد ع َ ُُت بـ ْ َر َْد َكف ق 

"Mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu"." 09:65-66. Kisa hiki kimepokelewa na Ibn Jariyr (Rahimahu Allaah) katika Tafsiyr yake (11/543)



Tutaendeleaa.....Usikose Sehemu ya 4 In Shaa Allaah..................


from fisabilillaah.com https://ift.tt/2QjFMDG
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...