MAANA YA SWALAH
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Maana Ya Swalaah Kilugha
Ni du'aa kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):
خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ إِنَّ صَلَاتَكَ سَكَنٌ لَّهُمْ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ﴿١٠٣﴾
Chukua (ee Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika mali zao Swadaqah, uwatakase na ziwazidishie kwazo na waombee du’aa (na maghfirah). Hakika du’aa yako ni utulivu kwao. Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. [At-Tawbah: 103]
Hadiyth ifuatayo inathibitisha pia maana hiyo:
عن أبي هريرة -رضي الله عنه- قال: قال رسول الله -صلى الله عليه وسلم: ((إذا دعي أحدكم فليجب فإن كان صائمًا فليصلِّ و إن كان مفطرًا فليطعم)) أخرجه مسلم
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Akialikwa mmoja wenu aitike (mwaliko), ikiwa amefunga aombe du'aa (kwa waliomualika), akiwa hakufunga basi ale (chakula))) [Muslim]
Yaani Awaombee du'aa ya maghfirah, baraka na kheri)
Swalaah kutoka kwa Allaah ni Himdi na kutoka kwa Malaika ni du'aa kama Anavyosema:
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
56. Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa mamkizi ya amani na kwa tasliymaa [Al-Ahzaab: 56]
Abu 'Alyah amesema: Swalaah ya Allaah ni kumsifu mja kwa Malaika Wake na Swalaah ya Malaika ni du'aa.
Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Wanawaswalia" maana wanawabarikia"
Vile vile Swalaah kutoka kwa Allaah ni maghfirah au Baraka. Swalaah kwa maana ya maghfirah nikutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala):
أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ ﴿١٥٧﴾
Hao zitakuwa juu yao Barakah kutoka kwa Rabb wao na rahmah, na hao ndio wenye kuongoka. [Al-Baqarah: 157]
Na kama ilivyosimuliwa kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa alisema:
اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى آل أَبِي أَوْفَى
‘Allahumma Swalli ‘alaa Aali Abi Awfiy’ Akimaanisha ‘Ee Allaah wasamehe jamaa wa Abu Awfiy’.
Hivyo hapa Swalaah ina maana ya maghfirah.
Maana Swalaah Kishariy'ah
Ni kumuabudu Allaah kwa kauli na vitendo maalumu vinavyoanza na Takbiyrah (Allaahu Akbar) na kumalizika na Tasliym (kutoa salaam).
Na imeitwa Swalaah kwa sababu inahusiana na du'aa katika kumuabudu Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) tunaposimama, tunaporukuu, tunaposujudu na tunapokaa, hivyo Swalaah nzima ni du'aa.
Na Allaah anajua zaidi
https://ift.tt/2GYkOoy i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni