Swali: Ni ipi tofauti kati ya mchawi na kuhani? Nikienda kwa mmoja wao ambapo akaniamrisha kufanya kitu fulani na nikakifanya lakini hata hivyo nisimsadikishe nakuwa ni mwenye kuingia katika Hadiyth isemayo:
“Atakayemwendea kuhani au mpigaramli akamsadikisha basi ni mwenye kukufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”?
Je, anapata dhambi kwa kitendo chake hichi?
Jibu: Mchawi anaweza kuwa kuhani kama ambavo kuhani anaweza kuwa mchawi. Kwa msemo mwingine sifa mbili hizi mbaya zinaweza kukusanyika kwa mtu mmoja ambapo mtu akawa mchawi na wakati huohuo akawa kuhani. Lakini tofauti kati ya hayo mawili endapo tutamweka mchawi nafasi yake na kuhani nafasi yake ni kwamba kuhani anakuwa na mashaytwaan ambao wanamweleza kuhusu khabari za mbinguni kuhusu mambo yaliyoko katika mustakabali. Kuhani yeye anaelezea mambo yaliyoko katika mustakabali.
Mchawi na kuhani wanaweza kuelezea jambo lililopitika. Kwa mfano anaweza kukuelezea ni wapi kitu chako kipo ukikipoteza. Ukipotewa na kitu fulani anakweleza mahali kilipo. Huyu ni mpiga ramli na mchawi. Lakini watu hawa hawaelezei mambo katika mustakabali. Kwa sababu hawana mashaytwaan wanaowaeleza kuhusu yanayotokea mbinguni. Kwa ajili hii tunasema kuhusiana na watu hawa watatu; mchawi, mpiga ramli na kuhani kwamba sifa zote hizi zinaweza kupatikana kwa mtu mmoja kama ambavo zinaweza kutokuwepo baadhi yake. Lakini hata hivyo kuhani ni yule anayeelezea mambo katika mustakabali. Haelezei jambo liliopo hivi sasa, bali jambo katika mustakabali.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2XtbFKz
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni