Translate

Ijumaa, 22 Februari 2019

  1. Kitanzi kwenye koo ya ndugu Kabanga

Baada ya kuona maana ya Salaf kilugha na kisheria na kuona kwamba madhehebu ya Salaf na neno ´Salaf` limethibiti katika Qur-aan, Sunnah na katika maneno ya maulamaa wa zamani na wa sasa na kwamba inafaa kabisa kujiita Salafy na hakuna ubaya wowote kufanya hivo, tofauti na anavyoona bwana Kabanga na watu wa Bid´ah wengine kwamba kufanya hivo haifai, kwamba ni kujiweka kipote na ni kujisifu na kwamba Allaah ametwita waislamu, tumejibu shubuha hiyo ambayo mara nyingi inatumiwa na watu wa Bid´ah kama vile Shaykh ´Abdul-Hamiyd Kishki wa Misri (Allaah amrehemu), Kishki wa Tanzania mimbari ya Vetenari na wengineo. Katika makala hiyo iliotangulia nambari tatu na tumebainikiwa kwamba inafaa tena mtu afanye hivo kwa kinywa kipana na kwa kifua mbele japokuwa atachukia bwana Kabanga na wengineo. Lengo lao – na Allaah ndiye anajua zaidi – ni kama kwamba anataka kuizima nuru ya Da´wah Salafiyyah ambayo imeanza kuchomoza katika nchi ya Burundi. Lakini tunamwambia:

وَاللَّـهُ مُتِمُّ نُورِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ

“Allaah ataitimiza nuru Yake japo makafiri watachukia.” (61:08)

Sasa leo ndugu msomaji tutaendelea na makala nambari nne ambayo lengo ni kuorodhesha baadhi ya shubuha zilizokuwa katika Khutbah yake na kuzijibu. Kwa kweli Khutbha yake ina makosa mengi (ndugu yetu mmoja – Allaah amlipe na amuhifadhi – amesema kwa harakaharaka yeye kaona makosa makubwa kumi) na mimi sintoweza kunukuu moja baada ya nyingine kwa sababu makala itarefuka sana. Bali nitanukuu tu baadhi ya zile shubuha kubwakubwa khasa ambazo zinahusiana na mada yetu ya usalafy na masalafy.

KIPENGE CHA NNE: Majibu juu ya baadhi ya shubuha ili kuichafua Da´wah Salafiyyah na Salafiyyuun

SHUBUHA YA KWANZA: Kabanga amesema:

”Muhammad ni Mtume wa Allaah na wale waliokuwa pamoja naye ni waaminifu. Hao waislamu, hao waaminifu walikuwa sana ni wakakamavu kwa makafiri wakioneana huruma wao kwa wao.” Halafu akaendelea kusema kwa kuuliza: ”Je, katika wakati wetu huu tunaoneana huruma waislamu? Je, tuko washupavu kwa makafiri?” Halafu yeye mwenyewe akajijibu kwa kusema: ”Laa wa alfu laa (hapana mara elfumoja). Leo waislamu tumekuwa washupavu kwa waislamu wenzetu na tumekuwa tunawahurumia makafiri. Pesa ya waislamu wote tunawapa makafiri na waislamu pesa yao hatuwapi.”

Majibu yetu: Bwana Kabanga maneno yako umeyasema kijumla na hujayaweka wazi. Tulikuwa tunakuomba utuwekee wazi ni waislamu gani hao ambao ni washupavu kwa waislamu wenzao na ni wenye kuwahurumia makafiri. Lakini lililo karibu zaidi ni kwamba majembe haya yanawaendea masalafy kwani Khutbah yako ni vita ulivyovielekeza kwa masalafy. Kama dhana yangu umesibu, basi tunasema:

كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِن يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا

“Ni maneno makubwa yanayotoka midomoni mwao – hawasemi isipokuwa uongo tu.” (18:05)

Hakuna watu walio na huruma kwa waislamu wenzao kama walivyo masalafiy na khaswa wale maulamaa wao. Na ndio maana utakuta katika vitabu kama vile “Thalaathat-ul-Usuwl”, “Qawaa´id-ul-Arba´ah” vya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab anaanza kwa kusema:

“Tambua ee msomaji – Allaah akurehemu; Tambue ee msomaji – Allaah akuhifadhi; Tambue ee msomaji Allaah akuelekeze katika kumtii” n.k. ambapo anamfunza yule mwanafunzi na wakati huohuo anamuombea du´aa. Kadhalika vitabu vilivyoandikwa na wanachuoni wa kisalafy kama mfano wa “Ithbaatu Swifat-il-´Uluww” cha Imaam Ibn Qudaamah al-Maqdisiy utawaona wanaanza vtabu vyao kwa kuandika Hadiyth isemayo:

“Wenye huruma hurehemewa na Yule Mwingi wa huruma. Wahurumieni wale walioko ardhini atakuhurumieni Yule aliye juu ya mbingu.”

Vilevile Hadiyth hiyo imepokelewa na Imam Ahmad (2/160), Abu Daawuud (4941), at-Tirmidhiy (1904), al-Haakim (4/159) na ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 20. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (4941).

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema alipokuwa anaeleza sifa za Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah:

Pamoja na misingi hii wanaamrisha mema na wanakataza maovu kwa yale ambayo Shari´ah imeyawajibisha. Wanaonelea kufanya Hajj, kupigana Jihaad, Swalah ya Ijumaa na sikukuu pamoja na watawala, ni mamoja wakiwa wema au waovu. Wanahifadhi Swalah ya Jamaa´ah na wanaona kuwapa naswaha Ummah ni katika sehemu ya Dini. Na wanaamini maana ya kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”

Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakutanisha baina ya vidole vyake viwili.

Na kauli yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mfano wa waumini, katika kupendana kwao, na kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao, ni kama mfano wa mwili mmoja. Wakati kiungo cha mwili kinapatwa na maumivu, mwili mzima unapatwa na homa na maumivu.”[1]

Vipi basi pamoja na haya yote bwana Kabanga atawazulia uongo masalafy kwamba ni wakali juu ya waislamu wenzao na ni wenye kuwahurumia makafiri?

Lakini ieleweke kwamba ikiwa bwana Kabanga anamaanisha kwamba ni wakali kwa watu wa Bid´ah waliozusha katika dini ya Allaah yale yasiyokuwemo, basi jawabu ni kweli kwamba masalafy ni wakali kwelikweli kwa watu wa Bid´ah ambao wanaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mfano wa watu wa Bid´ah ambao masalafy ni wakali kwao ni kama vile makhawaarij, masufi, matabligh na watu wa Bid´ah wengineo. Kuna dalili nyingi sana kutoka katika Qur-aan, Sunnah na maneno ya maulamaa wakubwa zinazoonyesha kwamba watu wa Bid´ah wanatakiwa kuchukiwa na kutengwa khaswa ikiwa mtu tayari amekwishawanasihi. Tutosheke na dalili zifuatazo:

1- Qur-aan

وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

“Unapowaona wale wanaoziingilia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka, usikae pamoja na watu madhalimu.” (06:68)

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na siku ya Mwisho.” (24:02)

Unaona hapa anavosema Allaah juu ya waislamu watenda madhambi waliozini? Amesema wazi kwamba wasifanyiwe huruma. Au Aayah hii ndio mara ya kwanza kuisoma bwana Kabanga?

2- Sunnah

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema alipokuwa anawazungumzia makhawaarij:

“Popote mtapokutana nao (yaani makhaawarij) waueni. Lau nitakutana nao, nitawaua kama walivyouawa kina ´Aad.”[2]

Kuna ukali zaidi katika matendo zaidi ya kuua? Huyu ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema hivi ambaye amesifiwa na Allaah kwamba ni mpole na mwenye huruma mno kwa waumini. Lakini huyuhuyu ndiye kasema juu ya makhawaarij kwamba ni mbwa wa Motoni na kwamba ni viumbe waovu kabisa[3]. Kwa hiyo mpaka hapa msomaji atapata kubainikiwa kwamba maneno ya bwana Kabanga aliposema kwamba waislamu  wa leo – akikusudia masalaf y – ni wakali na washupavu kwa waislamu wenzao ni maneno ya uongo kabisa kama jua la mchana wa saa sita. Hivyo usidanganyike na maneno yake. Muislamu mwerevu na mwenye busara ni yule anayeweka kila kitu mahali pake;  mahali pa upole anafanya upole na mahali pa ukali anafanya ukali. Hiyo ndio maana sahihi ya hekima.

Itaendelea….

Imeandaliwa na: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush

Tarehe: 17 Jumada al-Aakhir 1440 sawa na 22/02/2019

[1] al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah.

[2] al-Bukhaariy (6995), Muslim (1064), an-Nasaa´iy (2578), Abu Daawuud (4764), Ibn Maajah (169) na Ahmad (03/68).

[3] Ibn Maajah (176). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”al-Mishkaah” (3554).



from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2SQk5ND
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...