Mapokezi yote utayosikia ambayo hayakufikiwa na akili yako, kwa mfano maneno ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Nyoyo za waja ziko baina ya Vidole viwili katika Vidole vya Allaah (´Azza wa Jall).”
“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka katika mbingu ya dunia.”
“Anashuka siku ya ´Arafah.”
“Hakutoachwa kutupwa ndani ya Moto [watu na mawe] mpaka (Jalla Thanaa´uh) aweke unyayo Wake juu yake.”
Maneno ya Allaah (Ta´ala) kumwambia mja:
“Ukija Kwangu kwa kutembea, basi Mimi nitakuchepukia.”
“Hakika Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hushuka siku ya ´Arafah.”
“Hakika Allaah alimuumba Aadam kwa sura Yake.”
“Nilimuona Mola Wangu katika sura nzuri.”,
na mfano wa Hadiyth kama hizi, ni lazima kwako kujisalimisha, kuthibitisha na kutojiingiza katika namna yake na kuridhika na kutosheka na hilo. Usifasiri kitu katika hayo kwa matamanio yako. Hakika kuamini haya ni jambo la wajibu. Yeyote atayefasiri kitu katika haya kwa matamanio yake au akarudisha kitu katika haya, basi huyo ni Jahmiy.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2IGMFwm
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni