Translate

Jumamosi, 23 Februari 2019

Umauti ni Ukumbusho

KIFO NI MAWAIDHA, UTANI MSIBANI NI UJINGA.

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh

Anapo kufa mmoja wetu ni wajibu wetu kutafakari, leo ni mwenzetu kesho ni mimi au wewe, zidisha mema, acha mabaya ili ukutane na Mola wako ukiwa salama.

Utani hauna nafasi msibani tena ni haramu na ujinga ulio pindukia, kwa nini usitafakari yale anayo kwenda kukutana nayo mwenzako huko kaburini nawe ukaanza maandalizi?.

Amesema Allah mtukufu.

الَّذي خَلَقَ المَوتَ وَالحَياةَ لِيَبلُوَكُم أَيُّكُم أَحسَنُ عَمَلًا ۚ وَهُوَ العَزيزُ الغَفورُ

Ambaye ameumba mauti na uhai ili kukujaribuni ni nani miongoni mwenu mwenye vitendo vizuri zaidi. Na Yeye ni Mwenye nguvu na Mwenye msamaha (Almulku 2)

Mazingatio ya waja wema walio tangulia (Salafi) juu ya kifo.

قال عمر رضي الله عنه كفى بالموت واعظا.

Amesema Umar Allah amridhie,  Yanatosha mauti kuwa ni mawaidha.

قال التيمي - رحمه الله تعالى - : شيئان قطعا لذة الدنيا : ذكر الموت , وذكر الوقوف بين يدي الله.
Amesema Attaimiy Allah amrehemu,  Vitu viwili ni vyenye kukata ladha ya dunia,  Kukumbuka kifo na kukumbuka kusimama mbele ya Allah.

وكان عمر بن عبدالعزيز يجمع العلماء فيتذكرون الموت والقيامة والآخرة، فيبكون حتى كأن بين أيديهم جنازةَ‎!!.

Alikuwa Umar bnu Abdul Azizi anawakusanya wanachuoni na wana kumbushana kifo na Kiama na maisha ya akhera, basi wanalia mpaka inakuwa kama mbele yao kuna jeneza (Msiba).

Kuna namna nyingi na mbaya za utani msibani kwa baadhi ya makabila nami nitataja baadhi tu.

(a) Kuonesha furaha mbele ya wafiwa kwa kucheza ngoma,  au kuimba nyimbo na kujichekesha.

(b)  Kumsimanga maiti, Wewe fulani ulikuwa hivi na hivi, kama ulevi au uzinzi na leo hakuna tena.

(b) Kuigiza tabia za maiti katika uhai wake kama kigugumizi, au ulemavu, au mpepesuko wa ulevi wa pombe kama alikuwa ni mlevi.

(c)  Kuwashutumu wafiwa kwamba ni wachawi, Nyinyi mumemuua ndugu yenu, mumemroga ili mumle nyama.

(d)  Kuzuia mazishi kwa kujilaza mtani kaburini katika mwanandani huku akisema nizikeni mimi na huyo aliyekufa aendelee na shughuli zake, Hatoki hapo mpaka alipwe pesa atakazo hitaji.

(d) Wakati wa mazishi ikiwa aliye kufa ni mtoto mdogo katika kupokezana kubeba maiti basi mtani akipokea maiti hukimbia nayo na kuificha ndani kwake mpaka ikombolewe kwa pesa.

(e) Kumsifia mke wa marehemu na kumkejeli maiti, Wewe huna akili, uzuri wote huu umekubali kutuachia mke wako?  na wengine huleta barua ya posa kabla ya mazishi.

Wafanyaji wa yote haya wengine ni Waislamu na wanadai kumuamini Allah na Mtume  wake.

وَيَقولونَ آمَنّا بِاللَّهِ وَبِالرَّسولِ وَأَطَعنا ثُمَّ يَتَوَلّىٰ فَريقٌ مِنهُم مِن بَعدِ ذٰلِكَ ۚ وَما أُولٰئِكَ بِالمُؤمِنينَ

Na wanasema: Tumemuamini Allah na Mtume, na tumetii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini (Annuur 47)

Jamii hurithi jambo kutoka kwa mababu na likaonekana halina tatizo tena ni dogo kwa sababu ni mila,  kumbe ni tofauti kabisa, huenda ni miongoni mwa mambo mazito yanayo mchukiza  Allah.

إِذ تَلَقَّونَهُ بِأَلسِنَتِكُم وَتَقولونَ بِأَفواهِكُم ما لَيسَ لَكُم بِهِ عِلمٌ وَتَحسَبونَهُ هَيِّنًا وَهُوَ عِندَ اللَّهِ عَظيمٌ

Mulipo yapokea kwa ndimi zenu na mukasema kwa vinywa vyenu musiyo yajua, na mulifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Allah ni kubwa (Annuur 15).

Yote haya hufanyika misibani, watu wanaangalia na kucheka bila kukemea kwa vile ni mambo ya utani.Kuna watu huko nyuma walifanya utani ona Allah alicho waambia.

وَلَئِن سَأَلتَهُم لَيَقولُنَّ إِنَّما كُنّا نَخوضُ وَنَلعَبُ ۚ قُل أَبِاللَّهِ وَآياتِهِ وَرَسولِهِ كُنتُم تَستَهزِئونَ

Na ukiwauliza, wanasema: Sisi tulikuwa tukipiga porojo na kucheza tu. Sema: Mulikuwa mukimfanyia maskhara Allah na Ishara zake na Mtume wake? (Attawbah 65)

Hiki ndicho walicho ambiwa baada ya kujitetea, sasa wewe endelea na utani wako misibani.

لا تَعتَذِروا قَد كَفَرتُم بَعدَ إيمانِكُم ۚ إِن نَعفُ عَن طائِفَةٍ مِنكُم نُعَذِّب طائِفَةً بِأَنَّهُم كانوا مُجرِمينَ

Musitoe udhuru; mumekwisha kufuru baada ya kuamini kwenu! Tukilisamehe kundi moja kati yenu, tutaliadhibu kundi jingine kwa kuwa wao ni wakosefu (Attawbah 66).

عن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ, عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ : إِنَّ الْعَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالْكَلِمَةِ مِنْ رِضْوَانِ اللَّهِ لَا يُلْقِي لَهَا بَالًا يَرْفَعُهُ اللَّهُ بِهَا دَرَجَاتٍ ، وَإِنَّ الْعَبْدَ لَيَتَكَلَّمُ بِالْكَلِمَةِ مِنْ سَخَطِ اللَّهِ لَا يُلْقِي لَهَا بَالًا يَهْوِي بِهَا فِي جَهَنَّمَ( رواه البخاري 6487) .

Kutoka kwa Abuu Hurairah Allah amridhie, Kutoka kwa Mtume swala llaahu alayhi wasallama amesema, Hakika mja huzungumza neno  katika yanayo mridhisha Allah pasi na kuzingatia basi humnyanyua Allah daraja kwa neno hilo,  Na hakika mja hutamka neno lenye kumchukiza Allah pasi na kuzingatia likamtupa neno hilo Jahanamu (Bukhari 6487).

Ninakuomba Allah mtukufu ajaalie kila mwenye kusoma ujumbe huu na alikuwa ni miongoni mwa wafanyao mambo hayo basi mara moja aachane nayo huku akitaraji kupata radhi za Mola wake.



https://ift.tt/2BL4YKI i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...