Translate

Alhamisi, 28 Februari 2019

010-Lu-ulu-un-Manthuwrun: Mja Atafufuliwa Kwa Kitendo Alichofariki Nacho

 

 

 

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 10

Mja Atafufuliwa Kwa Kitendo Alichofariki Nacho

 

www.alhidaaya.com

 

 

 

 

عَنْ جَابِرٍ (رضي الله عنه) قَال: قَالَ النَّبِيَّ (صلى الله عليه و آله وسلم): ((يُبْعَثُ كُلُّ عَبْدٍ عَلَى مَا مَاتَ عَلَيْهِ)) رواه مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir (رضي الله عنه) ambaye amesema: Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Kila mja atafufuliwa katika hali aliyofia)) [Muslim]

 

 

 

Mafunzo Na Mwongozo

 

 

1. Hima ya kutenda mema na kubakia katika istiqaamah (kuthibitika katika Dini) ili kitendo cha mwisho kabla ya kufariki kiwe ni kitendo chema, na kiwe ni kiliwazo siku ya kufufuliwa. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾

Ambao Malaika huwafisha katika hali nzuri (Malaika) watasema: “Salaamun ‘Alaykum!” Amani iwe juu yenu ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.”  [An-Nahl (16: 32).]

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

 

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾

Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda.  [An-Nahl 16: 97].

 

Na pia rejea: Al-Hijr (15: 99), Al-‘Imraan (3: 102).

 

 

2. Umuhimu wa kupata husnul-khaatimah (mwisho mwema) kabla ya kuaga dunia na sio kuwa katika maasi, khasa pale mtu anapofikia katika umri mkubwa, kwa sababu kuna hatari ya mtu kugeuka kutoka katika twaa’ah (utiifu) na taqwa na kuingia katika maasi kama ilivyothibiti katika Hadiyth:

 

 

عَنْ أَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم -وَهُوَ الصَّادِقُ الْمَصْدُوقُ: ((إِنَّ أَحَدَكُمْ يُجْمَعُ خَلْقُهُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا نُطْفَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَ ذَلِكَ، ثُمَّ يُرْسَلُ إلَيْهِ الْمَلَكُ فَيَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، وَيُؤْمَرُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ: بِكَتْبِ رِزْقِهِ، وَأَجَلِهِ، وَعَمَلِهِ، وَشَقِيٍّ أَمْ سَعِيدٍ؛ فَوَاَللَّهِ الَّذِي لَا إلَهَ غَيْرُهُ إنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُهَا. وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا إلَّا ذِرَاعٌ فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الْكِتَابُ فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الْجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا)) رواه البخاري ومسلم

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdillaah bin Mas-‘uwd  (رضي الله عنه)  ambaye amesema: “Ametusimulia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  ambaye ni mkweli mwenye kuaminiwa: “Hakika kila mmoja wenu hukusanywa umbo lake katika tumbo la mama yake siku arubaini akiwa ni mkusanyiko wa mbegu (za uzazi za mama na baba), kisha arubaini zifuatazo huwa ni donge la damu, kisha arubaini zijazo huwa pande la nyama, kisha Allaah Humtuma Malaika kwake na kumpulizia roho (yake).  Na (Malaika huyo) anaamrishwa maneno manne; Kuandika rizki yake, ajali yake (umri atakaoishi duniani), amali zake, mtu muovu au mwema. Wa-Allaahi naapa kwa Yule Ambaye hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Yeye, hakika mmoja wenu huenda afanye ‘amali za watu wa Jannah hadi ikawa baina yake na Jannah ni dhiraa na kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa motoni akaingia motoni. Na mmoja wenu hufanya ‘amali za watu wa motoni hadi ikawa baina yake na moto ni dhiraa na hapo kile kilichoandikwa kikathibiti akafanya ‘amali ya watu wa Jannah akaingia Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na katika riwaayah inayomalizikia: ((…’amali zinahesabika za mwisho)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

3. Kutahadhari kubakia katika taqwa na twaa’ah (utiifu) wa Allaah (سبحانه وتعالى) na Rasuli Wake (صلى الله عليه وآله وسلم) na kwa sababu Allaah (سبحانه وتعالى) Anawajua vyema waja Wake na yaliyomo moyoni Naye ni Mweza wa kugeuza nyoyo zao pindi wanapomuasi. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّـهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ ۖ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ﴿٢٤﴾

Enyi walioamini! Muitikieni Allaah na Rasuli Anapokuiteni kwenye yale yenye kukuhuisheni na jueni kwamba Allaah Anaingilia kati baina ya mtu na moyo wake; na kwamba Kwake mtakusanywa. [Al-Anfaal (8: 24)].

 

 

4. Umuhimu wa kuomba du’aa ya kuthibitika katika Dini mpaka kufariki. Nayo ni du’aa ambayo alikuwa akiiomba sana Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

اللَّهُمَّ يَا مُقَلِّبَ الْقُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِك

((Allaahuuma Yaa Muqallibal-Quluub Thabbit Qalbiy 'Alaa Diynik – Ee Allaah, ee Mgeuza nyoyo, Thibitisha  moyo wangu katika Dini Yako)) [At-Tirmidhiy na amesema: Hadiyth Hasan]

 

Na pia kuomba Du’aa ya Nabiy Yuwsuf (عليه السلام)

 

 (اللَّهُمَّ)  فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ ﴿١٠١﴾

(Ee Allaah) Muanzilishi wa mbingu na ardhi. Wewe ni Mlinzi, Msaidizi wangu duniani na Aakhirah. Nifishe hali ya kuwa Muislamu na Unikutanishe na Swalihina.” [Yuwsuf (12: 101)]

 

 

 

5. Hatari ya kutenda maasi yakaja kuwa ndio kitendo cha mwisho cha Muislamu, kwani mauti yanamfikia mtu bila ya taarifa, mfano kupatwa na ajali ukiwa katika kuendesha gari na huku unasikiliza muziki.   

 

 

 

6. Kilicho muhimu ni ‘amali za mwisho, basi atakayefanya ‘amali zake kuwa ni bora katika uhai wake wa mwisho atapata bishara njema na kheri Siku ya Qiyaamah, na atakayefanya maovu katika uhai wake wa mwisho atakutana na shari huko Aakhirah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ ۖ فَأَلْقَوُا السَّلَمَ مَا كُنَّا نَعْمَلُ مِن سُوءٍ ۚ بَلَىٰ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٢٨﴾

Ambao Malaika huwafisha wakiwa wamejidhulumu nafsi zao, watasalimu amri (watasema): “Hatukuwa tukitenda uovu wowote.” (Wataambiwa): “Hapana! Hakika Allaah ni Mjuzi kwa yale mliyokuwa mkitenda.”

 

فَادْخُلُوا أَبْوَابَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا ۖ فَلَبِئْسَ مَثْوَى الْمُتَكَبِّرِينَ﴿٢٩﴾

 “Basi ingieni milango ya Jahannam ni wenye kudumu humo.” Ni uovu ulioje makazi ya wanaotakabari.

 

 

وَقِيلَ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا مَاذَا أَنزَلَ رَبُّكُمْ ۚ قَالُوا خَيْرًا ۗ لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا فِي هَـٰذِهِ الدُّنْيَا حَسَنَةٌ ۚ وَلَدَارُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ ۚ وَلَنِعْمَ دَارُ الْمُتَّقِينَ﴿٣٠﴾

Na wanapoambiwa wale waliokuwa na taqwa: “Nini Ameteremsha Rabb wenu?” Husema: “Kheri.” Kwa wale waliofanya ihsaan katika dunia hii watapata hasanah (mazuri). Na bila shaka nyumba ya Aakhirah ni bora zaidi. Na uzuri ulioje nyumba ya wenye taqwa.

 

 

جَنَّاتُ عَدْنٍ يَدْخُلُونَهَا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ لَهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ ۚ كَذَٰلِكَ يَجْزِي اللَّـهُ الْمُتَّقِينَ﴿٣١﴾

Jannaat za kudumu milele wataziingia humo, zipitazo chini yake mito. Watapata humo wayatakayo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyowalipa wenye taqwa.

 

 

الَّذِينَ تَتَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ طَيِّبِينَ ۙ يَقُولُونَ سَلَامٌ عَلَيْكُمُ ادْخُلُوا الْجَنَّةَ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ﴿٣٢﴾

Wale ambao Malaika huwafisha katika hali njema watasema: “Salaamun ‘Alaykum, (amani iwe juu yenu) ingieni Jannah kwa yale mliyokuwa mkitenda.” [An-Nahl (16: 28-32)]

 

 

Na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Anasema:

 

إِنَّ الْعَبْدَ لَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ النَّارِ، وَإِنَّهُ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَإِنَّهُ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، وَإِنَّمَا الأَعْمَالُ بِالْخَوَاتِيمِ ‏"‏‏.‏

((Hakika mja hutenda ‘amali za watu motoni lakini uhakika akaja kuwa ni mtu wa Jannah, na akaja kutenda ‘amali za watu wa Jannah lakini uhakika akaja kuwa mtu wa motoni. Hakika ‘amali zinahesabika za mwishoni)) [Al-Bukhaariy]

 

 

 

7. Kutochoka wala kulegea katika kufanya mema na kuacha kutenda maovu  kwa sababu hakuna anayejua wakati gani atatembelewa na Malakul-Mawt (Malaika wa kutoa roho). Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ وَاخْشَوْا يَوْمًا لَّا يَجْزِي وَالِدٌ عَن وَلَدِهِ وَلَا مَوْلُودٌ هُوَ جَازٍ عَن وَالِدِهِ شَيْئًا ۚ إِنَّ وَعْدَ اللَّـهِ حَقٌّ ۖ فَلَا تَغُرَّنَّكُمُ الْحَيَاةُ الدُّنْيَا وَلَا يَغُرَّنَّكُم بِاللَّـهِ الْغَرُورُ ﴿٣٣﴾

Enyi watu! Mcheni Rabb wenu, na iogopeni Siku ambayo mzazi hatomfaa mwanawe na wala mwana hatomfaa mzazi wake chochote. Hakika ahadi ya Allaah ni haki; basi usikughururini uhai wa dunia, na wala (shaytwaan) mwenye kughuri asikughururini kuhusu Allaah.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَيُنَزِّلُ الْغَيْثَ وَيَعْلَمُ مَا فِي الْأَرْحَامِ ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾

Hakika Allaah Ana elimu ya Saa (Qiyaamah), na Anateremsha mvua na Anajua yale yaliyomo katika tumbo la uzazi na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan 31: 33-34)]

 

 

 



from Alhidaaya.com https://ift.tt/2T5z46h
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...