*Swali*
Mume wangu amenikimbia yuko Mkoa mwingine na sipati huduma yeyote
jee si dhambi kwenda kwa mganga ili apate kurudi? kama dhambi munanishauri nifanye nini na nasikia mtu akidai Talaka pepo ya Mola haisikii hata harufu? Mtihani mkubwa kwangu umekuwa naomba msaada wenu.
*Majibu*
✅Tambua na tahadhari kwamba kwenda kumkabili mganga ni kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Majina Yake na Sifa Zake tukufu kwani unamkabili mganga kwa kuamini kwamba yeye atakuwa na uwezo wa kumrudisha mume wako na hali yeye ni kiumbe kama wewe dhaifu kabisa.
⏩Waganga hawana ila kutumia uchawi na kulaghai watu kwa kutaka mapato au chumo kutoka kwa watu wanaomwendea.
➡Mtu Mwenye kumwendea mganga ikiwa kwa ajili ya kumtegemea amtatulie matatizo yake au amtabirie jambo, hutoka nje ya Uislamu kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)⤵
((من أتى كاهناً فصدقه بما يقول فقد كفر بما أنزل على محمد صلى الله عليه وسلم)) رواه أبو داود
((Atakayemwendea mchawi na kuamini aliyoambiwa, basi amekufuru yale aliyoteremshiwa Muhammad [Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam]))
↪Imepokelewa na Imaam Abu Daawud
✅Hivyo pia ni kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na ni dhambi ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hamsamehe mja⤵
((إِنَّ اللّهَ لاَ يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَن يَشَاء وَمَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدِ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا))
((Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na Husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa))
↪Surat An-Nisaa Aya ya 48.
➡Hatari nyingine ni kwamba mwenye kumshirkisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hataingia Peponi⤵
((إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللّهُ عَلَيهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَار))
((Kwani anayemshirikisha Allaah hakika Allaah Atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na waliodhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru))
↪Surat Al-Maaidah Aya ya 72
✅Zingatia na fuata yafuatayo na InshaAllaah mumeo ikiwa ana kheri na wewe atarudi kwako, na ikiwa hakuna kheri, basi muombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akupe mwenye kheri zaidi yake.
1⃣Unatakiwa ujiulize mwenyewe kwanini mumeo amekukimbia? Bila ya shaka kuna sababu fulani.
➡Ikiwa ulikuwa na udhaifu fulani kwake, basi jambo la kwanza ni kujirekebisha huo udhaifu au tabia ambayo huenda ikawa ni sababu ya kukukimbia.
2⃣Unatakiwa uwatafute watu katika jamaa zako au jamaa zake wakusaidie kuwasiliana naye na waseme naye wapate kujua tatizo lenu ili mpate kusuluhishwa.
➡Ikiwa ni makosa kutoka kwako nawe unamtaka mumeo arudi, basi ujirekebishe na ukiri makosa yako na uombe radhi kwake na kumuahidi kwamba hutorudia tena na uko tayari kumridhisha. Salamu hizi hakikisha zinamfikia kwanza.
✅Kisha tambua kwamba Muislamu anapokutwa na mitihani ya aina yoyote anapaswa kuwa na subira na kumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa kuamini Qadhwaa na Qadar.
✅Kumbuka kwamba kupewa mitihani kuna maana ya kupandishwa daraja la mja anaposubiri.
✅Zidisha Taqwa na kumkabili Mola wako Aliyekuumba na Mwenye uwezo wa kukuondolea kila mitihani, shida, dhiki na matatizo.
(( وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا))
((Na anayemcha Mwenyezi Mungu Humtengezea njia ya kutokea))
↪Surat At-Twalaaq Aya ya 2
(( وَمَن يَتَّقِ اللَّهَ يَجْعَل لَّهُ مِنْ أَمْرِهِ يُسْرًا ))
((Na anayemcha Allaah, Humfanyia mambo yake kuwa mepesi))
↪Surat At-Twalaaq Aya ya 4.
⏩Amka usiku katika thuluthi ya mwisho ya usiku uswali Tahajjud na umuombe Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala).
✅Jishughulishe na kumkumbuka Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kila mara asubuhi na jioni, kwa kusoma Qur-aan, kusikiliza mawaidha, kutafuta elimu ya dini yako, yote haya yatakupa faida ya dunia na Akhera na yatakuridhisha nafsi yako, na pia yatakupunguzia mawazo.
➡Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)⤵
((الَّذِينَ آمَنُواْ وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللّهِ أَلاَ بِذِكْرِ اللّهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ))
((Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Allaah Hakika kwa kumkumbuka Allaah ndio nyoyo hutua!))
↪Surat Ar-Ra'ad Aya ya 28.
✅Kuwa na tawakkul (kumtegemea Allah) na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa mambo yako yote Naye Atakufungulia kila njia za kheri⤵
(( وَمَن يَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّهِ فَهُوَ حَسْبُهُ إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا))
((Na anayemtegemea Allaah Yeye Humtosha. Hakika Allaah Anatimiza amri yake. Allaah Kajaalia kila kitu na kipimo chake))
↪Surat At-Twalaaq Aya ya 3
✅Baada ya kufafanua yote hayo, tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akufanyie wepesi mtihani wako na Akufungulie lililo na kheri nawe.
Na Allaah Anajua zaidi
Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*
https://ift.tt/2Vi2FGb i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni