Translate

Jumatatu, 25 Februari 2019

Maana ya Aya ya 103 katika Surat Al-An’aam yanayosema “Macho Hayamzunguki”

Maana ya Aya ya 103 katika Surat Al-An’aam yanayosema  “Macho Hayamzunguki”


Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

“Na maana “Bila kuzunguka wala kayfiyah (kuzunguka vipi”, wao hawamzunguki Allaah (‘Azza wa Jalla), na kwamba wao wanamuona (Allaah) Subhaanahu bila ya kumzunguka. Na Allaah Mtukufu haiwezekani Yeye  kuzungukwa.

Anasema Subhaanahu:
وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾
na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha ujuzi Wake. [Twaahaa: 110]


Na Anasema Jalla Wa ‘Alaa:

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ  
Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote. [Al-An’aam: 103]

“Macho hayamzunguki”
Maana yake (katika Aayah hiyo) ni kuwa, “Hayamzunguki Yeye (macho ya mtu)”, na wala maana yake si “Hayamuoni.” Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Hakusema, “Hayamuoni Yeye macho.” bali Kasema, “Macho hayamzunguki.” Kudiriki ni kitu na kuona ni kitu kingine.

Hayo (macho) yanamuona Subhaanahu bila kumzunguka (pande zote kwa uoni), na kwa hili kuna radd (majibu) kwa yule mwenye kustadili (kutolea dalili) kwa Aayah hii kupinga kuonekana Allaah Qiyaamah. Akidai (mpotevu huyo) kuwa haiwezekani kuonekana Allaah, kwa sababu Allaah Kasema, “Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote;” [Al-An’aam: 103]

Tunawajibu (wenye itikadi hizo potofu), kuwa nyinyi hamfahamu maana ya “Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote”, bali maana yake ni “Hayamzunguki Yeye macho” na si maana yake “Hayamuoni Yeye”, na Hakusema Allaah, “Hayamuoni Yeye macho.”


[At-Ta’liyqaat Al-Mukhtaswarah ‘Alaa Al-‘Aqiydati Atw-Twahaawiyyah, mj. 1, uk. 78]




https://ift.tt/2VlDin7 i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...