Swali: Kuhusu kuwaita mayahudi “waisraaiyl” na manaswara “wakristo” inahusiana na Tamyi´ kwa msingi kwamba watu wasiwachukie?
Jibu: Hapana, hizi ni istilahi baina yao. Wanaitwa ´wakristo` kwa sababu baadhi yao wanamwabudu al-Masiyh na ´Ahl-ul-Kitaab` kwa sababu wanajinasibisha katika Tawraat na Injiyl. Kilicho muhimu ni kwamba muumini asijinasibishe kwa mayahudi, manaswara wala kwa wale ambao wana kitu katika Bid´ah kama mfano wa Jahmiyyah na Mu´tazilah. Lengo ajiepushe na shari na watu wake. Badala yake anatakiwa kujinasibisha na Ahl-us-Sunnah, Maswahabah na wale waliofuata mwenendo wao imara ambao ni as-Salaf as-Swaalih.
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2twAjwb
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni