Mambo ya Haramu yanayofanyika Saloon katika kazi ya kinyozi
8. Baadhi ya Vinyozi kuweka Wanawake wa Kuwaosha Wanaume Nywele zao na hata wengine Kuchuliwa (Massage) na Wanawake
Ingawa nasaha hizi zilikusudiwa vinyozi wa nchi za Ulaya na mazingira mfano wake, lakini si vibaya kuchanganya na mazingira ya vinyozi walioko Afrika ambao ndio wengi hufanya jambo hili.
Ifahamike kuwa hili ni jambo lisilofaa na kukubalika kishariy’ah, achilia mbali kidini, bali japo kimaadili na hayaa za kiuana Aadam ni jambo lililo kinyume na murua.
Ikiwa tu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) katoa makemeo makali mno kwa mwanamme na mwanamke kupeana mikono au kugusana, ijekuwa kuoshwa mwanamme na mwanamke asiye mahram wake!
Amesema Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam):
“Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake.” [At-Twabaraaniy katika Al-Mu’jamAl-Kabiyr na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]
Ee mja wa Allaah, jiweke mbali na makaripio hayo makali na epuka ukharibifu huo wa shariy’ah na maadili kwa tamaa za kuvuta wateja dhaifu walitawaliwa na matamanio ya nafsi. Usiwe wewe ndio kichocheo cha maasi na uchafu.
9. Baadhi ya Saluni Vinyozi huwanyoa Nywele Wanawake
Mwanamke kunyoa nywele zake kipara au kunyolewa ni jambo lililokatazwa na shariy’ah. Kadhaalika mwanamke kukata nywele zake kimitindo kama makafiri.
Kutoka kwa ‘Aliy (Radhwiya Allaahu ‘anhu) anaeleza kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza wanawake kunyoa nywele zao. [At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]
Kadhaalika, Al-Khallaal (Rahimahu Allaah) anasimulia kutoka kwa Qataadah (Rahimahu Allaah) naye kutoka kwa ‘Ikrimah (Rahimahu Allaah) ambaye amesema: “Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza wanawake kunyoa nywele zao.”
Vilevile Hadiyth iliyohadithiwa na Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kunyoa nywele si jukumu lililowekewa wanawake; kukata kidogo ndivyo inavyotakiwa.” [Abuu Daawuwd].
Na Hadiyth nyingine kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ni kuwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Wanawake (mahujaji) hawafai kunyoa (vichwa vyao); wanaweza tu kupunguza nywele zao.” [Abuu Daawuwd].
Ibn al-Mundhir amesema: “Yapo maafikiano miongoni mwa Wanachuoni kuhusu hili, kwa kuwa kunyoa nywele za kichwa cha mwanamke ni aina ya adhabu.”
Kwa hali ya dharura kama maradhi ya kichwa au wadudu wa kichwani, hapo ndipo tu mwanamke anaporuhusiwa kunyoa kipara.
Ee kinyozi wa Kiislamu, mche Mola wako na jiepushe kunyoa wanawake nywele. Kumbuka kuwa, katika kumnyoa mwanamke nywele, mbali na makatazo yaliyo hapo juu, vilevile kunahusisha kutazama maeneo ya wazi ya mwanamke yasiyoruhusiwa kishariy’ah na kadhaalika kumgusa mwanamke na kumshika. Yote hayo ni haramu ya wazi.
https://ift.tt/2ItzC17 i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni