Translate

Jumamosi, 23 Februari 2019

Ukweli Unapelekea Jannah, Uongo Unapelekea Motoni

(Mkusanyiko Wa Hadiyth Mbali Mbali Na Mafunzo Yake)

Hadiyth Ya 4

Ukweli Unapelekea Jannah, Uongo Unapelekea Motoni




عَنْ عَبْدُ الله إبنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ (صلى الله عليه و آله وسلم قَالَ: ((إِنَّ الصِّدْقَ يَهْدِي إِلَى الْبِرِّ وَإِنَّ الْبِرَّ يَهْدِي إِلَى الْجَنَّةِ ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَصْدُقُ حَتَّى يَكُونَ صِدِّيقًا ، وَإِنَّ الْكَذِبَ يَهْدِي إِلَى الْفُجُورِ وَإِنَّ الْفُجُورَ يَهْدِي إِلَى النَّارِ ، وَإِنَّ الرَّجُلَ لَيَكْذِبُ حَتَّى يُكْتَبَ عِنْدَ اللَّهِ كَذَّابًا)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه)  kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakika ukweli unaongoza katika wema, na hakika wema unaongoza katika Jannah, na mtu ataendelea kusema ukweli mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni mkweli. Na hakika uongo unaongoza katika uovu, na hakika uovu unapeleka motoni, na mtu ataendelea kusema uongo mpaka aandikiwe mbele ya Allaah kuwa ni muongo)).[Al-Bukhaariy na Muslim]


Mafunzo Na Mwongozo:


1. Muislamu atangamane na wakweli ili naye apate tabia ya ukweli, nayo ni amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ وَكُونُوا مَعَ الصَّادِقِينَ﴿١١٩﴾
Enyi walioamini! Mcheni Allaah na kuweni pamoja na wakweli. [At-Tawbah 9: 119].


2. Umuhimu wa kuwa na sifa ya ‘ukweli’ na iwe sifa kuu ya Muumin.

Rejea: Al-Hujuraat (49: 150).


3. Kuhimizwa na pendekezo katika kusema ukweli, kwani ni sababu ya kutenda mema. Na tahadharisho la uongo kwani ni sababu ya kutenda maovu.


4. Hatari ya kufuata nyayo za shaytwaan za kuanza kusema uongo hadi unampeleka mtu motoni.


5. Mkweli atajulikana kwa kupewa sifa ya ‘mkweli’, na muongo atajulikana kwa kupewa sifa ya ‘muongo’.



6. Ukweli utamfaa mtu mwenyewe Aakhirah na matokeo na thawabu zake   ni kupata Jannah. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

قَالَ اللَّـهُ هَـٰذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ ۚ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ ۚ ذَٰلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ ﴿١١٩﴾
Allaah Atasema: “Hii ndiyo Siku itakayowafaa Asw-Swaadiqiyna ukweli wao; watapata Jannaat zipitazo chini yake mito; ni wenye kudumu humo abadi.  Allaah Ameridhika nao, nao wameridhika Naye. Huko ni kufuzu adhimu.”  [Al-Maaidah 5: 119]


na matokeo na malipo ya muongo ni adhabu kutoka kwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea: Al-Ahzaab (33: 24).


7. Ukweli uwe kwa niyyah, kauli na ‘amali njema ili alipwe mtu malipo mema.



8. Allaah (سبحانه وتعالى) Amewasifu wakweli na Atawapa malipo mema kabisa.

Rejea: Al-Ahzaab (33: 35), Al-Hadiyd (57: 18).



9. Kusema uongo ni katika maovu ya ulimi, na ulimi usipochungwa unamuangamiza mtu.  

Rejea Hadiyth namba (37), (86), (87), (93), (94), (126).



10. Ikiwa huna hakika na jambo fulani ni bora kujiepusha kulisema ili ubakie salama na kusema uongo kwani ukweli ni utulivu na uongo ni mashaka. Hadiyth ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): 
 
عن أبي محمد الحسن بنِ عليِّ بن أبي طالب رضي الله عنهما قَالَ: حَفظْتُ مِنْ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لا يَرِيبُكَ؛ فإنَّ الصِّدقَ طُمَأنِينَةٌ، وَالكَذِبَ رِيبَةٌ)). رواه الترمذي، وَقالَ: ((حديث صحيح))
Abuu Muhammad, Al-Hasan bin ‘Alliy bin Abiy Twaalib  (رضي الله عنهما)    amesema: Nimehifadhi kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  maneno haya: “Acha linalokutia shaka ufuate lisilokutia shaka; hakika ukweli ni utulivu na uongo ni mashaka.” [At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth  hii ni Hasan]


from Uislamu Wangu https://ift.tt/2SjSejz
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...