Translate

Jumapili, 24 Februari 2019

Je, Wanandoa waliosilimu watafunga ndoa upya?

*Swali*

Swali, kwaupande wa wenzetu wakristo Kwa imani yao wao walikuwa wanaishi pamoja wakiwa wamefunga Ndoa kanisani ila Baada ya Miaka miwili Wakapata Dawa ikawaingia wakaamua kuslimu na kuwa Waislam Je inabidi Wafunge Ndoa Upya Au wanaendelea na Ndoa ile ile walio funga Kanisan?

*Jibu*

✅Ama kuhusu swali hili ni kuwa mtu aliyesilimu na mkewe, Uislamu unaikubali ndoa yao waliyofunga kanisani au kimila ikiwa ndio inayotambuliwa kiada wakati huo walipooana.

➡Hivyo, wanandoa hao hawana haja kufunga ndoa tena ila tu ikiwa wao wenyewe wanaona kufanya hivyo watakuwa na utulivu zaidi.

➡Na Ikiwa watakuwa na Watoto basi bila shaka watoto waliowazaa kwa ndoa hiyo kabla kusilimu watakuwa wanatambulika kama watoto halali.

➡Tofauti inaweza kuwepo ikiwa watoto hawatosalimu kama wazazi wao, na ikiwa ni hivyo, watoto hawatoweza kuwarithi wazazi wao wala kinyume chake.

Na Allaah Anajua zaidi

Imeandaliwa na *Imaam Masjid Tawbah*



https://ift.tt/2U3Mufy i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...