[12] Inatakiwa kuamini ufufuliwaji na Njia. Nembo ya waumini siku hiyo itakuwa:
”Salimisha, salimisha.”
Imekuja katika Hadiyth kwamba Njia itakuwa yenye makali zaidi kuliko upanga na nyembamba zaidi kuliko unywele[1].
[13] Kuamini Mizani. Amesema (Ta´ala):
وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ
“Tutaweka mizani ya uadilifu siku ya Qiyaamah, basi hakuna nafsi itakayodhulumiwa chochote japo ikiwa uzito wa mbegu ya haradali Tutaileta. Inatosheleza Kwetu kuwa wenye kuhesabu.”[2]
´Abdullaah bin Mas´uud amesema:
”Siku ya Qiyaamah watu wataletwa kwenye Mizani na hapo watabishana ubishi mkubwa kabisa.”
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kwa kutoa mchana na usiku. Kwenye mkono Wake mwingine kuna mizani ambayo hushusha na hupandisha.”[3]
[14] Inatakiwa kuamini Hodhi na Uombezi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mimi nina Hodhi inayoanzia Ayla kwenda mpaka Adeni na vikombe vyake ni sawa na idadi ya nyota mbinguni.”[4]
Bi maana ni kubwa sana.
Anas bin Maalik amesema:
”Mwenye kukadhibisha Hodhi basi hatokunywa humo.”
[15] Mtu anatakiwa kuamini pia mahojiano. Allaah (Ta´ala) atamuhoji mja kwa yale yote aliyoyafanya, madogo na makubwa.
[1] Muslim (195).
[2] 21:47
[3] al-Bukhaariy (4684), Muslim (993), Ahmad (2/242) na at-Tirmidhiy (3045) ambaye amesema:
“Hdiyth hii ni nuri na Swahiyh na akaifasiri Aayah:
وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ
“Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah umefumbwa.” Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali mikono Yake imefumbuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)
Hadiyth imepolewa na maimamu. Tunaiamini kwa udhahiri wake pasi na kuifasiri wala kuifanyia namna. Hivyo ndivo walivosema maimamu akiwemo Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, Ibn ´Uyaynah na Ibn-ul-Mubaarak; zinatakiwa kupitishwa na kuziamini pasi na kuzifanyia namna.”
[4]al-Bukhaariy (6591) na Muslim (2298).
from Firqatu Nnajia https://ift.tt/2GLDMiY
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni