HUKUMU YA SWALAH
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh
Hukumu Ya Swalaah
Swalaah ni fardhi kwa kila Muislamu mwenye akili timamu, aliyebaleghe kutokana na dalili kutoka katika Qur-aan:
وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾
Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah; na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 5]
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا ﴿١٠٣﴾
hakika Swalaah kwa Waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalumu [An-Nisaa: 103]
Kwa Maana ya Kwamba ikifika wakati wake wa Swalah basi Muumini anatakiwa kuacha Shughuli zake na kuitekeleza Kwanza Ibada ya Swalah.
Na sio kwamba Mtu imefika wakati wa Swalah yeye anajiwekea ratiba yake kuwa ngoja kwanza Nisubiri wakati upite kidogo ndio Uswali la Hasha, inatakiwa ikifika tu wakati wake basi inatakiwa itekelezwe kwanza Ibada hii ikiwa hauna Udhuru wa Kisheriah.
Ama katika Sunnah ni kauli yake Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mu'aadh Bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kupeleka risala Yemen kwa kumwambia: ((…na wafundishe kwamba Allaah Amewafaridhisha Swalaah tano kila siku…)) [Al-Bukhaariy Na Muslim]
Vile vile,
عبدالله بن عمر قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم (( بُنِـيَ الإِسْلاَمُ علـى خَمْسٍ: شَهادَةِ أنْ لا إِلٰهَ إلا الله وأنَّ مُـحَمَّداً رَسُولُ الله وإِقامِ الصَّلاَةِ وإِيتاءِ الزَّكاةِ وَحَجِّ البَـيْتِ وَصَوْمِ رَمَضَانَ(( البخاري
Kutoka kwa 'Abdullaah ibn 'Umar ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Uislamu umejengeka kwa matano; Kushuhudia (na kukiri kwa moyo) kwamba hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allaah na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah na kuswali (Swalaah tano), kutoa Zakaah, kuhiji katika Nyumba (Makkah) na kufunga (mwezi wa) Ramadhwaan)) [Al-Bukhaariy]
Kuna Aayah na Hadiyth nyingi zinazothibitisha kuwajibika kwa Swalaah. Ama mwanamke mwenye hedhi na aliye katika nifaas hawawajibiki kuswali kutokana na kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
أليس إذا حاضت المرأة لم تصل ولم تصم ؟ -متفق
((Kwani sio kweli kwamba mwanamke anapokuwa katika hedhi haswali wala hafungi?)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Allaah anajua zaidi
https://ift.tt/2tz4KSh i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni