NAMNA YA KUFUNGISHA NDOA YA KIISLAMU
Assalam Aleykum warahmatullah wabarakatuh Ndugu zangu katika Imani.
💝JE UNATAKA KUJUA JINSI YA KUFUNGISHA NDOA BASI FUATILIA DARSA ZETU NDANI YA WHATSSAP 💝
💞Ndugu zangu katika Imani Hebu leo tujifunze Jinsi ya kufungisha Nikah (ndoa) katika Dini yetu hii Tukufu ya Kiislamu.
💖Ndugu zangu katika Imani kuhusu Swiyghah (au maneno) yanayotakiwa kusemwa au kutamkwa katika kufungisha ndoa(Nikah katika uislam) nitayataja hapo chini .
💞Basi Ikiwa hayo masharti yote yamekamilika(yaani masharti ya ndoa ya Kiislamu) basi utasoma khutba ya nikaha kama ifuatavyo:
💕 Kwanza kabisa baada ya pande zote kukutana yaani Ndugu wa bwana harusi na majirani zake na Ndugu wa bibi harusi na majirani zake basi mmoja wenu yaani labda ustadh au mwanamume yoyote mwenye kujua kusoma Qur'an atasoma hivi,
💖 Innal Hamda Lillaahi Nahmaduhu wa Nasta‘iynuhu wa Nastaghfiruhu wa Natuwbu ilayhi. Wa Na‘udhu Billaahi min shuruuri anfusina wa sayyi’ati a‘maalina man yahdihi Allaahu falaa mudhwilla lahu wa man yudhwlil falaa haadiya lahu wa Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhu wa Rasuuluhu💖
➡Baada ya hapo utasoma Suraatul Al-Imran Aaya ya 102;
💝Baada ya hapo utasoma Suraatil An-Nisaa Aayah ya 1
💝Kisha utasoma Suraatil Al-Ahzaab Aaya ya 70 hadi Aya ya 71.
✅Kisha utawahimiza waliohudhuria na haswa vijana kuoa kwani hiyo ni Sunnah ya Manabii na watu wema. Pia uwaonye Waislamu wasiwe ni wenye kuiendea zinaa kwani hiyo ni njia mbaya zaidi
👉Soma Qur'an 17: 32
✅Basi Baada ya kumaliza mawaidha hayo mafupi utamshika mkono bwana harusi na kumwambia:
"Zawwajtuka fulaan binti fulaan bimahriha kamat tafaktum au bimahriha kadhaa(kwa Kiswahili unaweza kumwambia Nimekuoza wewe fulani binti fulani [utaje jina la binti pamoja na la babake] kwa mahari mliyosikilizana au kwa mahari kadhaa [utaje kiwango cha mahari]). Bwana harusi naye atajibu kwa kusema:Nimekubali kumuoa fulani binti fulani kwa mahari yake…
Ndugu zangu katika Imani, Basi baada ya kumaliza hilo watasoma suraatul Fatha yaani Alhamdu kisha wataomba du'aa.
Na baada ya hapo bwana harusi atatakiwa kwenda kumuona bibi harusi na kumuombea du'aa kisha baada ya hapo watamchukua bibi harusi na kuondoka naye.
Ndugu zangu katika Imani, Naamini mpaka kufikia hapo umejua na umefaidika basi usiache kufuatilia Darsa na Mada ndani ya group WhatSapp
from fisabilillaah.com http://bit.ly/2SHyquF
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
SWALI: Assalaam alaykum Naomba maana ya majina yeyote tuwapao watoto wetu AU mnielekeze wapi naweza kupata labda katika kitabu cha fas...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni