Translate

Jumatatu, 11 Februari 2019

Inafaa kuunga nywele kwa uzi / nyuzi

SWALI

Ni ipi hukumu ya mwanamke kuunganisha nywele zake na uzi?

JIBU

✅Naam ama katika mapambo ya kike yaliyokatazwa ni kuunga nywele zake kwa nywele nyingine, zikiwa ni za kweli (zake au za mwengine) au za bandia kama vile wigi au vipande vya kuongeza.

Al-Hadithi

Imepokewa na ‘Aaishah, dadake Asmaa’, Ibn ‘Umar, Ibn Mas‘uud na Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhum) kuwa:

“Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwenye kuunga nywele na mwenye kuungwa”
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy.

Al-Hadithi

Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alilitilia mkazo sana katika kupiga vita aina hii ya hadaa kufikia hadi kukataza yule zimtokaye nywele zake kwa sababu ya maradhi kuziunga kwa nywele nyingine hata akiwa ni biharusi anayepelekwa kwa mumewe.
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy, an-Nasaa’iy na Ibn Maajah.

✅Huku kuungwa kwa nywele kumeitwa na Mtume Muhammad(Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ni udanganyifu.
↪Imepokelewa na Imaam Al-Bukhaariy.

✅Kwa ufupi, kuunga nywele ni haramu zikiwa za kweli au za bandia nao ni udanganyifu uliokatazwa.

✅Ama kuunga nywele kwa vitambara au nyuzi kama ulivyosema  na vitu kama hivyo si katika vilivyoharamishwa kwani imepokewa na Sa‘iyd bin Jubayr kuwa: “Kutumia nyuzi za hariri au sufi katika kuunga mwanamke nywele zake – au kusukia mikia yake – si vibaya”. Haya yamethibitishwa na Imaam Ahmad kuwa yanajuzu kwa kuwa vitu viwili hivyo havifanani.

✅Na Wapo wanazuoni wenye muelekeo kuwa kuunganisha ni kuunganisha ikiwa ni kwa nyuzi, nywele zako au za mwingine, za kweli au za bandia ni sawa kabisa bila kutofautisha. Kwa hiyo, nasiha yetu kwa dada zetu ni afadhali muachane na kuunganisha nywele kwa chochote kiwacho.

Na Allaah Anajua zaidi

from fisabilillaah.com http://bit.ly/2Sqv3ZL
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...