Translate

Jumatatu, 18 Februari 2019

Je ni lazima mwanamke kufunika miguu yake wakati wa Swalah?

Swali

Je, ni lazima kwa mwanamke kufunika miguu anaposwali?

Jibu

Ndio ni Wajiib kwa Mwanamke kufunika Miguu yake wakati wa Swalah.

Umm Salamah alimuuliza Mtume Muhammad (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam):

“Mwanamke anaweza kuswali na kanzu pasi na sketi?” Akasema: “Ndio, ikiwa kanzu hiyo inafunika miguu.”
↪Imepokelewa na Imaam Abu Daawuud (1/149).

Ibn Qudaamah amesema: ”Wanachuoni wengi wanasema haya ni maneno ya Umm Salamah, ilihali ´Abdur-Rahmaan bin ´Abdillaah bin Diynaar anaonelea kuwa ni maneno ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”
↪Rejea Al-Mughniy (2/329))

Rejea Kitab  Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (35)

Na Allaah anajua zaidi



http://bit.ly/2tqb6n7 i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...