Kuwasaidia makafiri dhidi ya waislamu chini yake kuna mafungu mengi:
1- Fungu la kwanza: Kuwasaidia dhidi ya waislamu pamoja na kupenda yale mambo ya ukafiri waliyomo, shirki na upotevu. Fungu hili haina shaka yoyote kuwa ni shirki kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Atakayewasaidia dhidi ya waislamu pamoja na kupenda dini yao waliyomo na kuridhika nayo, sambamba na hilo akafanya hivo kwa kutaka kwake mwenyewe na si kwamba amelazimishwa, hii inakuwa ni kufuru kubwa inayomtoa mtu katika Uislamu. Hivo ndio udhahiri wa maneno Yake (Ta´ala):
فَإِنَّهُ مِنْهُمْ
“… basi hakika yeye ni miongoni mwao.”
from Firqatu Nnajia http://bit.ly/2SaJzjB
via IFTTT
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni