*Swali*
Hukmu ya Kufukia au Kuchoma Karatasi za Qur'an?
*Jibu*
✅Inafahamika vyema kuwa Qur-aan ni Kitabu kitukufu chetu na Aayah zake ni Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na (Tabaaraka wa Taa’la).
➡Kitabu hiki ambacho hakina shaka ndani yake, na ni mwongozo wa wamchao Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kinafaa kitukuzwe kwa kusomwa, kuhifadhiwa na kufuatwa maagizo yaliyomo ndani yake.
➡Hivyo, Aayah hizo zikiwa kwenye kalenda, fremu, picha, ukuta ni lazima ziwe ni zenye kupatiwa taadhima inayostahili. Ifahamike kuwa Qur-aan haikuteremshwa ili kutiwa katika kalenda bali inatakiwa itiwe ndani ya vifua vya wana Aadam na kusomeshwa kama inavyotakiwa.
➡Zikiwa Aayah hizo tayari zipo katika kalenda ambayo umepatiwa na muda wake umeisha inafaa uzihifadhi sehemu ambayo ni nzuri au uzichome moto kurasa za kalenda hiyo ili zisiwe ni zenye kukanyangwa, kuchezewa au kutupwa ovyo bila ya kuwekewa heshima inavyopaswa.
➡Au kuziweka hizo karatasi hizo zenye Aayah za Qur-aan au jina la Allaah ('Azza wa Jalla) katika nidhamu ya urejelezaji (recylcing) ya karatasi n.k. Kwa kuzipa heshima zaidi, ni bora kuziweka katika mfuko wa karatasi pekee kuliko kuzichanganya na makaratasi mengineyo na waziweke juu ya hizo zote nyingine.
قال ابن بطال: " وفى أمر عثمان بتحريق الصحف والمصاحف حين جمع القرآن جواز تحريق الكتب التي فيها أسماء الله تعالى ، وأن ذلك إكرام لها ، وصيانة من الوطء بالأقدام ، وطرحها في ضياع من الأرض ". انتهى من " شرح صحيح البخاري" (10/226) .
*Amesema Ibn Battwaal (Allaah Amhifadhi) :Na katika (tukio) la 'Uthman (Allaah Amhifadhi ), kuchoma sahifa na Misahafu wakati alipoikusanya Qur'aN, kuna dalili ya kujuzu kuvichoma vitabu ambavyo ndani yake kuna majina ya ALLAH Mtukufu.na kwamba jambo hilo huzingatiwa ni ikramu ya hivyo vitabu na ni jambo la kuvihifadhi kutokana na suala la kukanyagwa kwa nyao na kutupwa hovyo ardhini"*
↪Rejea Kitab Fat-hulbaariy 10/ 226.
قال السيوطي: " إذا احتيج إلى تعطيل بعض أوراق المصحف لبلى ونحوه ، فلا يجوز وضعها في شق أو غيره ؛ لأنه قد يسقط ويوطأ ، ولا يجوز تمزيقها لما فيه من تقطيع الحروف وتفرقة الكلم ، وفي ذلك إزراء بالمكتوب ... وإن أحرقها بالنار فلا بأس ، أحرق عثمان مصاحف كان فيها آيات وقراءات منسوخة ولم ينكر عليه ". انتهى " الإتقان في علوم القرآن" (2 / 1187)
*Amesema Imaam Suyuutwiyy (Allaah Amhifadhi):Kama itahitajika kuharibiwa kwa baadhi ya nyaraka (za Qur'an) kwa uchakavu na mfano wake, basi haitofaa kuziweka kwenye nyufa (za nyumba au jengo) na mfano wake, kwasababu huenda zikaanguka na kukanyagwa. Na wala haijuzu kuzichana na kuzipasua kwani kwenye hilo zitakatika herufi kutoka katika mpangilio wake na katika hilo kutapatikana hali ya kukipunguza hadhi kilichoandikwa...Lakini kama atazichoma kwa moto hakuna ubaya , kwani alishawahi kuchoma 'Uthmaan Misahafu ambayo ndani yake kuna Aayah na kisomo ambacho ni Mansuukh (kimefutwa), na hakupatikana wa kumpinga"*
↪Rejea Kitab Al-Itqaan 2/1187.
وقال شيخ الإسلام ابن تيمية: "وأما المصحف العتيق والذي تَخرَّق وصار بحيث لا ينتفع به بالقراءة فيه ، فإنه يدفن في مكان يُصان فيه ، كما أن كرامة بدن المؤمن دفنه في موضع يصان فيه ". انتهى "مجموع الفتاوى" (12/599).
*Amesema Ibn Taymiyyah (Allaah Amhifadhi):"Ama Msahafu ulio mkongwe ambao umepasuka ukawa hauna manufaa (kwa hali uliyo) kwa namna ya kuwa haunufaishi kwa usomaji, msahafu huo utafukiwa sehemu ambayo utakuwa umehifadhika. kama ambavyo kuukirimu mwili wa wa Mu'mini ni kuuzika sehemu yenye hifadhi (kadhaalika msahafu msahafu mkongwe).*
↪Rejra Kitab Al-majmuu 12/599.
وقال الشيخ ابن عثيمين: " ولكن ينبغي بعد إحراقه أن يدق حتى لا يبقى قطع من الأوراق ، لأن الإحراق تبقى معه صورة الحرف كما يشاهد كثيراً ، فإذا دق وصار رماداً زال هذا المحذور ". انتهى من "فتاوى نور على الدرب" (16 / 148).
*Amesema Ibn 'Uthaymiin (Allaah Amhifadhi ):Lakini itapasa baada ya kuuchoma atazame kwa makini ili visibakie vipande vya karatasi, kwasababu hali uunguzaji hubakisha (pia) sura za herufi (baada ya kuchoma) kama ambavyo hushuhudiwa hilo kwa wingi. kwahiyo kama atamakinika kwa hilo na akaona kwamba zimekuwa jivu basi kile kinachochelewa (khofiwa) kitakuwa kimeondoka".*
↪Rejea Kitab Nuurun 'alad-darb 16/148''.
✅Kwahiyo kwa ujumla ya kauli ni kuwa hali zote mbili za kuchoka au kufukia ni Sahihi.
Na Allaah Anajua zaidi
http://bit.ly/2SDRcEe i live islam
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni