Translate

Jumapili, 17 Februari 2019

Ardhi ambayo ilipigwa Jua kwa siku moja tu na haitopigwa tena mpaka siku ya Qiyamah

Swali

Ni Eneo gani ya Ardhi ambayo Jua lilipigwa kwa Siku moja na halitopigwa tena Mpaka siku ya Qiyamah...?

Jibu

BismilLaahir Rahmaniir Rahiim

Naam ama Sehemu iliyopigwa jua siku moja na haitopigwa tena jua mpaka siku ya Qiyamah ni Eneo katika Bahari ya sham ambapo Nabii Mussa (Aleiyhi Sallaam) Alipokuwa akifuatwa na jeshi la fir-'aun.

Ndipo Allaah (Subhaana wa Taala) Akamuamrisha Nabii Mussa (Aleyhi Sallaam)  kwamba⤵

   فَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنِ اضْرِبْ بِعَصَاكَ الْبَحْرَ ۖ فَانْفَلَقَ فَكَانَ كُلُّ فِرْقٍ كَالطَّوْدِ الْعَظِيمِ

Mara tulimletea Wahyi Musa (Tukamwambia): ''Piga bahari kwa fimbo yako''. Basi ikatengana, na kila sehemu ikawa kama jabali (mlima) kubwa.
↪Surat Ash-Shu'ara Aya ya 63

Kwahiyo ndugu zangu katika Imaani,  Baada ya Nabii Musaa (Aleyhi Sallaam) kuipiga ile Bahari kwa Fimbo yake kama alivyoamrishwa na Allaah (Subhaana wa Taala) ile Bahari hii ilipasuka sehemu mbili, ikafanyika njia katikati yake kwa maana ya Kwamba Allaah (Subhaana wa Taala) alilileta Jua na pakakausha sehemu ile ya katikati ili Nabii Mussa (Aleyhi Sallaam) apite na Wati wake.

Kwahiyo Nabii Mussa (Aleyhi Sallaam) akapita na watu wake, Firaun kuona vile akajitia na yeye na jeshi lake, Lakini Ilipomalizika tu kuvuka Nabii Mussa(Aleyhi Sallaam) na watu wake, bahari ilijifunga palepale, ikamfunga Firaun na watu wake.

Kwahiyo Allaah (Subhanahu wa Ta'ala) Aliliamlisha jua kupiga kwa Nguvu sehemu ile ili pakauke Watu waliombatana na Nabii Mussa (Aleyhi Sallaam) wapite bila shida.

Na baada ya Watu wa Mussa kuvuka katika Bahari ile Watu wa Fir-'aun pamoja na Fir-'aun Mwenyewe walipoingia Bahari kupitia njia ile ile Aliyopitia Nabii  Mussa (Aleyhi Sallaam) kama nilivyosema hapo juu na watu wake, basi Allaah (Subhanahu wa Ta'aala) Akaifunika Bahari ile na watu wa Fir-'aun wakaangamia.

Kwaiyo tangia siku hiyo Eneo lile halikuwai tena kupigwa na jua mpaka siku ya Qiyamah.

Na Allaah anajua zaidi



http://bit.ly/2N9WrFx i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...