Translate

Jumamosi, 16 Februari 2019

Aina za Shirki

AINA ZA SHIRKI

Assallaam Aleykum WarahmatulLaah Wabarakatuh

1.SHIRKI  KUBWA.

Ni kama kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah, kumuomba asiyekuwa Allaah, kusujudu kwa ajili ya asiyekuwa Allaah, kama kuamini asiyekuwa Allaah anaweza kunufaisha au kudhuru badala ya Allaah. Mwenye kufanya hivyo anatoka katika dini.

2.SHIRKI  NDOGO.

Ni kama Riyaa ndogo.

Mtu Mwenye Riyaa hii hatoki katika Dini, lakini inawajibisha kutubia kwayo.

3.SHIRKI  ILIYOFICHIKANA.

Ni mtu kufanya ´amali nafasi ya mtu, nayo ni shirki ndogo lakini ni dhambi kubwa.

Miongoni mwayo ni Riyaa. Shirki hii haimtoi mtu katika Uislamu lakini inawajibisha kutubia.

Ama  Kuhusu shirki kubwa inamtoa mtu katika Uislamu.

4.SHIRKI. YA I'TIQAAD.

Ni mtu kuamini ya kwamba asiyekuwa Allaah anaumba, anaruzuku, anahuisha, anafisha au anajua yaliyofichikana isipokuwa Allaah.

Hii ni shirki kubwa nayo inamtoa katika Uislamu.

5.SHIRKI  YA  KIMATENDO. 

Ni kila tendo lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki.

Shirki hii kuna kubwa na ndogo.

6.SHIRKI  YA  KIMATAMSHI

Ni kila tamshi lililohukumiwa na Shari´ah ya kwamba ni shirki.

Kwa mfano kuapa kwa asiyekuwa Allaah, kama wasemavyo baadhi ya watu: ´Sikuwa mimi isipokuwa kwa ajili ya Allaah na kwa ajili yako`, ´namtegemea Allaah na wewe`, ´lau bila ya Allaah na fulani kusingelikuwa kadhaa`, na matamshi mengineyo ya shirki. Shirki hii kuna kubwa na ndogo.

7.SHIRKI  YA  KUTUNGA  SHARI'AH 

Ni mtu kuipuuza Qur-aan na Sunnah au akapuuza baadhi ya hukumu zake.

Badala yake akachukua maoni na kanuni za watu. Allaah (Ta´ala) amesema: أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ “Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah Hakuyatolea kwayo idhini?” (42:21)

8.SHIRKI  YA  MAPENZI.

Ni kule mtu kumpenda asiyekuwa Allaah kama jinsi anavyompenda Allaah au zaidi.

Anasema Allaah (Ta´ala): وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ “Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah kuwa ni wanaolingana [na Allaah] wanawapenda kama mapenzi ya kumpenda Allaah.” (02:165)

9.SHIRKI  YA  KHOFU NA KUOGOPA

Tutalizungumzia katika “Vigawanyo vya khofu” - Allaah akitaka.

10.SHIRKI  YA  MAKUSUDIO NA MATAKWA

Ni mtu afanye ´amali na huku asimkusudii na wala asifanye kwa ajili ya Allaah.

Hii ni shirki ya makusudio na matakwa.

11.SHIRKI  YA  UTIIFU

Ni kule mja kumtii mtu katika kuhalalisha haramu au kuharamisha halali.

Amesema (Ta´ala): اتَّخَذُوا أَحْبَارَهُمْ وَرُهْبَانَهُمْ أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ “Wamewafanya marabi na watawa wao kuwa ni miungu badala ya Allaah.” (09:31)

MAREJEO : Al-Qawl Al-Mufiyd fiy Adillat-it-Tawhiyd 

NA. ALLAAH ANAJUA ZAIDI



http://bit.ly/2SB3vB4 i live islam

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...