Translate

Jumapili, 25 Novemba 2018

Risaalah fiy Sujuudus-Sahw (Sijda ya kusahau) - Sehemu ya 3

                                             Risaalah fiy Sujuudus-Sahw (Sijda ya kusahau) 


                                   Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn 

                                                      Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush



Naam,tunaendelea na sehemu ya tatu


                                              Sababu ya pili an-Naqsw 


Kupunguka kwa nguzo Mwenye kuswali pale ambapo atapunguza nguzo katika Swalah yake, ikiwa ni Takbiyrat-ul-Ihraam, basi hana Swalah, sawa ikiwa ameiacha kwa kusahau au kwa kukusudia. Kwa kuwa Swalah yake haikusimama.


Ikiwa ni kitu kingine (ambacho ni nguzo) kisichokuwa Takbiyrat-ul-Ihraam na akawa amekiacha kwa kukusudia, basi Swalah yake inabatilika.


>>Endapo atakuwa ameiacha kwa kusahau, akifika mahala pake katika Rakaa ile ya pili, ile Rakaa ya kwanza (ambayo kulikosekana nguzo) itakuwa imefutika (haihesabiki) na ile Rakaa (aliyomo sasa) itasimama mahala pa ile ya kwanza.


>>Endapo atakuwa hajafika mahala pale alipoacha ile nguzo, itamuwajibikia kwake arudi katika ile nguzo alioacha na ailete tena na kuendelea kuanzia hapo. Katika hali zote mbili ni wajibu kwake yeye kusujudu Sujuud-us-Sahuw baada ya Salaam.

Mfano wa hilo


Mtu amesahau Sijda ya pili katika Rakaa ya kwanza.

>>Akakumbuka hilo wakati amekaa baina ya Sijda mbili katika Rakaa ya pili, ataifuta ile Rakaa ya kwanza na ile Rakaa ya pili itasimama mahala pake (pa ile ya kwanza) na ataizingatia kuwa ndio Rakaa ya kwanza.

>>Atakamilisha Swalah yake halafu atatoa Salaam kisha atasujudu Sujuud-us-Sahuw na kutoa Salaam.


Mfano mwingine

Mtu amesahau Sijda ya pili na kukaa kabla yake, katika ile Rakaa ya kwanza. Akakumbuka hilo baada ya kusimama katika Rakaa ya pili.

>>Katika hali hii anatakiwa kurudi na kukaa, kisha asujudu kisha aendelee Swalah yake kwa kujengea hapo.

>>Baadaye atatoa Salaam, halafu atasujudu Sujuud-us-Sahuw na kutoa Salaam.


 Naqsw al-Waajibaat (kupunguka wajibu wa Swalah)


Mwenye kuswali akiacha jambo la wajibu katika mambo ya wajibu ya Swalah kwa kukusudia, Swalah yake inabatilika.


>>Endapo itakuwa ni kwa kusahau na akakumbuka hilo kabla ya kutoka mahala pake katika Swalah, hivyo ataileta na wala hana juu yake kitu.


>>Na endapo ataikumbuka baada ya kutoka mahala pake, lakini kabla ya kufika kwenye nguzo inayofuata hivyo anatakiwa kurudi. Ataleta jambo hilo la wajibu, kisha atakamilisha (ataendelea) na Swalah yake, halafu atatoa Salaam, kisha atasujudu Sujuud-us-Sahuw na kutoa Salaam.


>>Na endapo atakumbuka baada ya kufika katika nguzo inayofuata, itakuwa imebomoka na wala hatorejea kwayo, isipokuwa ataendelea Swalah yake. Atasujudu Sujuud-us-Sahuw kabla ya kutoa Salaam.


Mfano wa hilo


Mtu ameinuka kutoka katika Sijda ya pili katika Rakaa ya pili ili asimame kwenda katika Rakaa ya tatu hali ya kuwa amesahau Tashahhud ya kwanza.

>>Akakumbuka hilo kabla ya kuinuka, anatakiwa kubaki hapo na kusoma Tashahhud kisha ataendelea Swalah yake na hana juu yake kitu.


>>Ikiwa atakumbuka hilo baada ya kuinuka kabla ya kusimama wima, hivyo atarudi na kukaa na kuleta Tashahhud.


>>Kisha ataendelea na Swalah yake na kutoa Salaam kisha asujudu Sujuud-us-Sahuw halafu atatoa Salaam. Endapo atakumbuka hilo baada ya kusimama wima, itambomokea yeye Tashahhud (yaani hana Tashahhud tena) na wala asirejee kwayo, isipokuwa atakamilisha Swalah yake na kusujudu Sujuud-us-Sahuw kabla ya kutoa Salaam.


Dalili ya hilo 

Ni yale aliyopokea al-Bukhaariy na wengineo kutoka kwa ´Abdullaah bin Buhaynah (Radhiya Allaahu ´anhu), ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Swalah ya Dhuhr, na akasimama katika Rakaa mbili za kwanza na hakukaa katika Tashahhud ya kwanza na watu wakawa wamesimama. Wakati alipomaliza Swalah na watu wakawa wanamsubiri Mtume atoe Salaam, akapiga Takbiyr hali ya kuwa amekaa na akasujudu Sijda mbili (Sujuud-us-Sahuw) kabla ya kutoa Salaam, kisha ndio akatoa Salaam.


Inaendelea, Usikose sehemu ya 4 In Shaa Allaah...........................

from fisabilillaah.com https://ift.tt/2PQcqgG
via IFTTT

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah

  إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم   Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!   20 - Isti’aadhah  (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah   ...