Risaalah fiy Sujuudus-Sahw (Sijda ya kusahau)
Mwandishi: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Himidi zote ni Zake Allaah, Mola wa viumbe. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad – ambaye kafikisha ujumbe wa wazi – na ahli zake, Maswahabah zake na watakaomfuata kwa wema hadi siku hiyo ya Mwisho.
Amma ba´ad:
Hakika wengi miongoni mwa watu wanakuwa ni wajinga (wasiojua) Ahkaam kuhusiana na Sujuud-us-Sahuw katika Swalah. Miongoni mwao kuko ambao wanaacha Sujuud-us-Sahuw mahala ambapo ni wajibu kusujudu. Na miongoni mwao kuko ambao wanasujudu mahala ambapo sio mahala pake.
Na miongoni mwao kuko ambao wanasujudu Sujuud-us-Sahuw kabla ya Salaam wakati mahapa pale Sujuud-us-Sahuw inatakiwa kuwa baada ya Salaam.
Na miongoni mwao kuko ambao wanasujudu Sujuud-us-Sahuw baada ya Salaam wakati mahapa pale Sujuud-us-Sahuw inatakiwa kuwa kabla ya Salaam. Kwa ajili hiyo, ndio maana ikawa kujua Ahkaam zake (Sujuud-usSahuw) ni jambo muhimu sana, na khaswa kwa maimamu ambao watu wanawafuata wao na wakabeba majukumu katika kufuata yale yaliyowekwa katika Swalah zao na wakawaongoza Waislamu katika hayo.
Kwa ajili hiyo, nikapendelea kuwaandikia ndugu zangu baadhi ya Ahkaam kuhusiana na mlango huu nikitaraji kutoka kwa Allaah Awanufaishe kwayo waja Wake waumini.
Ninasema na huku nikimtaka msaada Allaah na nikitaraji kutoka Kwake Atuongoze katika Tawfiyq na usawa.
Sujuud-us-Sahuw
Sujuud-us-Sahuw ni ibara ya Sijda mbili ambazo anasujudu mwenye kuswali ili azibe kosa (pengo & upungufu) lililopatikana katika Swalah yake kwa ajili ya kusahau.
Sababu zake ni tatu:
1- az-ziyaadah (kuzidisha kitu katika Swalah).
2- an-Naqsw (kupunguza kitu katika Swalah).
3- as-Shakk (kuwa na shaka juu ya Swalah).
Sababu ya kwanza
az-ziyaadahPale atakapozidisha mwenye kuswali katika Swalah yake kisimamo, kukaa (Rukuu) au sijda (Sujuud) kwa kukusudia, Swalah yake inabatilika.
Hata hivyo ikiwa ni kwa kusahau na hakukumbuka kuwa amezidisha ispokuwa mpaka alipomaliza Swalah, hana juu yake isipokuwa kusujudu Sujuud-us-Sahuw na Swalah yake ni sahihi.
Endapo atakumbuka kuwa amezidisha katikati ya Swalah, itamuwajibikia kwake kurudi na itamuwajibikia kwake kusujudu Sujuud-us-Sahuw na Swalah yake ni sahihi.
Mfano wa hilo
Mtu ameswali Swalah ya Dhuhr Rakaa tano na wala hakukumbuka kuwa amezidisha isipokuwa katika Tashahhud.
>>Anatakiwa kukamilisha Tashahhud na kutoa Salaam, kisha atasujudu Sujuud-us-Sahuw kisha atoe Salaam.
>>Ikiwa hakukumbuka kuwa amezidisha isipokuwa baada ya kutoa Salaam, anatakiwa kusujudu Sujuud-us-Sahuw.
>>Ikiwa atakumbuka kuwa amezidisha katikati ya Rakaa ya tano, pale pale atarudi na kutoa Tashahhud, halafu atatoa Salaam kisha atasujudu Sujuudus-Sahuw na kutoa Salaam.
Dalili ya hilo
Hadiyth ya ´Abdullaah bin Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anhu): “Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali Dhuhr Rakaa tano. Akaambiwa: “Je, kumezidishwa Swalah?” Akasema: “Kwa nini?” Wakasema: “Umeswali Rakaa tano.” Pale pale akasujudu Sijda mbili baada ya kutoa Salaam.”
Katika Riwaayah nyingine:
“Akaelekeza miguu yake Qiblah na akasujudu Sijda mbili kisha akatoa Salaam.” (al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, an-Nasaa´iy, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah)
Kutoa Salaam kabla ya Swalah kumalizika
>>Kutoa Salaam kabla ya Swalah kumalizika huzingatiwa ni katika kuzidisha katika Swalah. Mwenye kuswali akitoa Salaam kabla ya Swalah kumalizika kwa kukusudia, Swalah yake inabatilika.
>>Ikiwa ni mwenye kusahau (akaswali Swalah pungufu) na asikumbuke hilo isipokuwa baada ya muda mrefu, anatakiwa kurudi kuswali upya.
>>Endapo atakumbuka baada ya muda mfupi, kama dakika mbili au tatu, anatakiwa kukamilisha Swalah yake na kutoa Salaam, halafu atasujudu Sujuud-usSahuw kisha atoe Salaam.
Dalili ya hilo
Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anhu): “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalisha Dhuhr au ´Aswr, akatoa Salaam baada ya Rakaa mbili. Kisha akatoka haraka kwenye mlango wa Msikiti na huku wakisema (Maswahabah) ya kwamba Swalah imefupishwa (imepunguzwa). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasimama katika ubao wa Msikiti na akaushegamia kama kwamba amekasirika. Akasimama mtu na kusema: “Je, umesahau au Swalah imepunguzwa?” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Sikusahau na wala Swalah haikupunguzwa. Yule mtu akasema: “Ndio, umesahau.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia Maswahabah: “Ni kweli ayasemayo?” Wakasema: “Ndio.” Hivyo akatangulia mbele na akaswali zile Rakaa zilizokuwa zimebaki halafu akatoa Salaam, kisha akasujudu Sijda mbili kisha akatoa Salaam”.” (al-Bukhaariy na Muslim)
>>Imamu akitoa Salaam kabla ya Swalah yake kumalizika na miongoni mwa maamuma kuko ambao wamepitwa na baadhi ya Rakaa. Kisha Imamu akakumbuka ya kwamba Swalah yake ina upungufu, hivyo akasimama kukamilisha zile Swalah.
>>Wale maamuma ambao wamesimama ili kukidhi (kulipa) zile Rakaa zilizowapita wana khiyari, ima wataendelea kukidhi zile Rakaa zilizowapita na watasujudu Sujuud-us-Sahuw kivyao au wanaweza kurudi na kuungana na Imamu na wakamfuata. Atakapotoa Salaam (Imamu), hao maamuma watakidhi zile Rakaa zilizowapita.
>>Kisha baada ya hapo watasujudu Sujuud-us-Sahuw baada ya kutoa Salaam na hili ndio bora na lililo na usalama zaidi.
Inaendelea, Usikose sehemu ya 3 In Shaa Allaah........................
from fisabilillaah.com https://ift.tt/2RiR9J2
via IFTTT
Translate
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
20-Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! - Isti’aadhah Kwa Asiyekuwa Allaah
إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيم Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno! 20 - Isti’aadhah (Kuomba Kinga) Kwa Asiyekuwa Allaah ...
-
Dalili 18 zinazoashiria una ujauzito wa mtoto wa kiume Awali ya yote nitoe pongezi kwa mama K na Baba K wote popote walipo kwa kazi nzuri ...
-
SWALI: Assalaam alaykum Naomba maana ya majina yeyote tuwapao watoto wetu AU mnielekeze wapi naweza kupata labda katika kitabu cha fas...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni